Naililia afrika nakupenda afrika

Naililia afrika nakupenda afrika

mabuba

Senior Member
Joined
Dec 5, 2006
Posts
133
Reaction score
90
Waasisi wamesalitiwa

afrika nakulilia.

Afrika umekuwa mtumwa wa wb

afrika umekuwa kuhadi wa imf

afrika zobe la usa,

afrika umekuwa simango la watu wako

nakulilia afrika.



Afrika ndoto iwapi,

matumbo yetu yamepoteza ndoto afrika,

viongozi wetu wamekuwa wasaliti wetu,

wametutwisha zigo,

zigo la umasikini na ufukara zamivu,



nyerere, kwame amukeni,

azikiwe, ben bella njoo,

hubert maga na maurice yameogo sijawasahau,

njooni mchape wazandiki wafikra zenu

pia mwambieni mwami mwambusta asikose



ahamadou ahidjo huko mtafute david dacko,

mwambie francois tombalbaye ninalilia afrika,

fulbert youlou usichelewe, njoo na minyororo,

gamal abdel nasser sijakusahau, nyumbi kwako hapakaliki,

njooni muone fikra ufisadi zimetanda.



Haile selassie mfalme, jirani zao wauana,

leon m'ba nakwambia ninalia,

viongozi wetu wametusaliti hakuna umoja tena,

afrika imebaki jina, naumia.

Nakulilia afrika.



Sekou toure uko wapi, houphouet boigny anakutafuta,

william tubman ninaumia, njoo upesi,

king ldris nakupasha, gaddafi amesalitiwa,

philibert tsiranana, dj kachukua nchi wananchi wanacheza muziki,

modibo keita na kenyatta sisemi uongo,



mokhtar 0uld daddah nakulilia,

king hassan pale kwa jirani yako hapakariki,

hamani diori usimcheke, burundi sasa amani imerejea,

nakuambia wewe groire kayibanda,

leopold sedar senghor nazani umeumia,

mwambie milton margai akufute machozi,



abdella osman mwambie obote,

museveni sio yyle tena,

marshal farik lbrahim abboud hapa ninafikia,

msalimie habib bourguiba,pia sylvanus olympio.



Afrika huna jipya,

umekuwa mlalamikaji,

mwenye kujipendekeza,

ukiambatatana na fikra mfu,

huna mashiko tena.



Nawalilia waasisi,

walifikiri kwa akili,

walifanya kwa utashi mantiki,

waliona katika maono,

walibeba wafrika



viongozi leo wanafikri ki imf,

wanaona ki wb,

wanasikiliza ki usa,

wanaonja ki ulaya,

wanahisi kichina



uafrika leo ni,

ubeberu,

umangimeza,

unyonyaji,

ufisadi

upapa

unyangumi



naililia afrika nakupenda afrika
 
Back
Top Bottom