Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Wakati sajili zinaenda kutamatika kwa timu mbalimbali, hadi sasa kwenye mpira wa kimtazamo ( mpira wa makaratasi) Simba na Azam wananda kuipa wakati mgumu Yanga kwenye mbio za ubingwa wa NBC na Azam Federation cup. Hakuna shaka kuwa msimu uliopita, Simba ndio timu yenye safu bora ya ushambuliaji na ulinzi, lakini pamoja na kuwa na safu bora ya ushambuliaji lakini bado wameongeza watu wa maana katika maeneo ya idara ya ushambuliaji..
Yanga mpaka sasa hakuna mshabiki yeyote anaweza kutamba kwa lolote, kwasababu bado kuna giza kubwa sana imetanda hasa kutokana na kuondoka kwa benchi nzima la ufundi na wachezaji kadhaa huku replacement zao haijulikani wataleta kipi.
Azam msimu huu wamesajili na wanaonesha wako serious kama ilivyo kwa Simba ambapo wao msimu uliopita ilikuwa na kikosi imara cha first eleven ila wakaponza na ufinyu wa wachezaji wenye quality katika substitution na wachezaji kutokuwa na mwendelezo wa viwango.
Hali naiona tofauti sana kwa msimu mpya Simba wameamua kuweka watu wengi wa kuuwasha moto, ni kazi ya kocha tu iliyobakia.
Wana Yanga wenzangu tunasubiria siku ya mwananchi ili tujue tutavuna kipi. Tumekuwa kama yatima sasa baada ya kuzoeshwa vibaya na Nabi kujiamini, sasa wale mashujaa wetu waliotufanya tutambe na turinge hawapo tena