SoC01 Naipenda nchi yangu

SoC01 Naipenda nchi yangu

Stories of Change - 2021 Competition

Geeh37

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
1
Reaction score
1
NCHI YANGU, UHAI WANGU!

Ndugu mpenzi msomaji wa stori hii , naomba usome kwa ufanisi mkubwa na wa hali ya juu ili uweze kukipata kitu kinachoweza kubadili mtizamo wako na kubadili maisha yako kwa manufaa yako, ndugu zako na jamii nzima kwa ujumla. Ndugu kijana mwenzangu, baba, mama unaesoma tungo hii naomba utambue ya kwamba dunia ya sasa inahitaji akili sana ili uweze kufanikiwa katika maisha yako, hasa kwako wewe kijana ambaye bado una muda mrefu kidogo wa kutimiza ndoto zako.

Asilimia kubwa ya kizazi cha sasa inaelekeza muda mwingi sana katika matumizi ya vifaa vya umeme, yaani Simu janja na kompyuta, na kibaya zaidi wanatumia vifaa hivyo kwa vitu visivyokuwa na faida sana katika maisha yao.Ndugu zangu naomba mfungueni macho juu ya swala hili.Nchi za Afrika tunakandamizwa sana na nchi za ughaibuni kwa siri sana, ni wachache sana wenye uwezo wa kulitambua hili.Fikiria... hivi sasa ni asilimia ngapi ya vijana wanatumia zaidi simu janja kushinda mitandaoni na kupoteza muda mwingi sana pa si kuingiza hata senti moja ya kitanzania?

Je, ni kwamba hawana kazi za kufanya mpaka wanapoteza muda mwingi kutumia simu hizo? Jibu ni kwamba kazi za kufanya kama kijana zipo nyingi sana, tena kwa kijana wa kitanzania kuna fursa nyingi sana zinawasubiri lakini kutokana na kitu kinachoitwa utandawazi wanajifanya kwamba baadhi ya kazi haziwafai.

Vijana wanapiga picha kutwa nzima wakapendeze katika akaunti zao za facebook na instagram, badala ya kushinda kazini na kupambana ili kujikwamua kimaisha.Kijana siku nzima anashinda akiwaza anapata wapi hela ya kufanya Photoshoot ili akapendeze na kujiuza katika macho ya watu katika mitandao ya kijamii.Ndugu zangu tutambue ya kwamba....teknolojia ni mbinu mbadala ambayo imefanywa na mzungu ili kuendelea kumkandamiza muafrika asiendelee kiuchumi.Waafrika wenzangu fungukeni akili tafadhali....ebu fanyeni upelelezi mfupi sana katika mitandao ya kijamii, pitia akaunti za watu kama ishirini(20) tu kutoka bara la ulaya.

Ukifatilia vizuri utakuta asilimia themanini(80%) katika akaunti zao hawana post za kujionesha miili yao na muonekano wao kama ilivo kwa vijana wetu wa kiafrika hasa watanzania...zaidi utakuta mtu kama ana post nyingi ni za biashara zake la sivyo utakuta ana post kama mbili au tatu na sio kama sisi watanzania wengi, hasa vijana unakuta mtu ana post hadi mia moja na zaidi. Ndo maana hata ukifatilia asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa hata watanzania, huwezi kukuta anaendekeza sana matumizi ya mitandao ya kijamii.

Mbinu hizi za kulihangamiza kabisa bara la Afrika, ni mbinu ya pili ya wazungu baada ya kufukuzwa kipindi kile cha ukoloni.Swali la kujiuliza ni kwamba....je, ni kweli ukoloni ulikwisha kama inavyosemekana? Ni kweli mzungu alikubali kushindwa na kuondoka kirahisi rahisi tu? Jibu ni hapana.Wazungu ni watu wasiokubali kushindwa siku zote. Sasa hivi tunatawaliwa kwa mfumo usio wa moja kwa moja(yaani indirect colonialism).Ukoloni huu ni hatari sana zaidi ya ule wa kwanza.Kwani ukoloni huu ni wa kiakili na sio wa miili kama ilivokuwa zamani. Kwa sasa tunatawaliwa akili na wazungu kupitia mitandao ya kijamii, mfumo wa elimu tulioachiwa n.k.

Sasa hivi tuna shida kubwa sana katika soko la Ajira hapa nchini..na hii yote ni malengo ya elimu iliyoanzishwa na wakoloni mwaka 1885 ambayo ilisemekana kukomeshwa 1960.Lakini wazungu waliitoa elimu hiyo kwa lengo la kuhangamiza uchumi na maendeleo ya waafrika.Ni malengo yaliyokuwa ya muda mrefu sana takribani miaka zaidi ya mia moja, hatimaye madhara yake tunayaona leo.Walianza kuihangiza afrika kwa kuifanya elimu ionekane na thamani sana....walimjali sana na kuonesha kumthamini sana msomi.

Basi waafrika wengi wakaamini sana katika elimu na kuajiliwa.Kipindi kile walitokomeza kabisa na kuwadhulu wale wote walio onekena kuwa na vipaji asilia wakilenga kuizika kabisa teknolojia ya kiafrika. Waliua waafrika wengi sana, wengine walifanywa walemavu na baadhi yao walichukuliwa na kupelekwa Ulaya ili wakaikuze sanaa yao na kuitangaza Ulaya badala ya Afrika.Na teknolojia ya kiafrika ilizikwa maksudi kama namna pekee ya kuandaa mazingira rafiki ya kuisambaza teknolojia yao.Ndugu zangu, fungueni fikra zenu tafadhali.

Vijana wengi sasa hivi wameaminishwa ukisoma basi wewe ni mheshimiwa huwezi kufanya kazi ndogo ndogo za kijasiliamali, kitu ambacho sio kweli kabisa.Ukienda kwa wachina utakuta karibia kila nyumba ina kiwanda kidogo kila mtu ni mjasiliamali bila kujali amesoma au la!.Kusoma ni kuongeza uwezo wa kufikiri tu na kutatua matatizo madogo madogo na sio kupata ajira.Elimu hii tuliyoachiwa ni ya madaftari na sio ya kivitendo. Mfumo huu wa elimu hauruhusu kabisa Mhitimu kujiajiri baada ya kuhitimu mafunzo yake.

Ndugu wazazi wekezeni sana katika utambuzi wa vipaji vya watoto wenu na sio kuvizika kwa kisingizio cha kusoma. Tusikubali kutimiza malengo ya wazungu. Ndio maana mpaka leo takwimu zinaonesha kwamba watu wenye mafanikio makubwa duniani ni wazungu. Na hii ni kutokana na kwamba wao wanawekeza sana katika utambuzi wa vipaji na muelekeo wa watoto na sio kuamini asilimia mia moja katika elimu. Fungueni macho watanzania wenzangu, jaribuni kulifikiria hilo kwa mara nyingine.

Naomba na nashauri Wizara ya elimu ifanye mabadiliko katika mfumo huu wa elimu tulioachiwa na watu weupe.Mfumo huu hauruhusu kabisa kuchochea maendeleo ya kitaifa, kiuchumi na kijamii, kwani unamjengea mwanafunzi mazingira ya kutegemea ajira serikalini.Kitu ambacho hakiwezekani wasomi wote kuajiliwa na serikali.

Watanzania wenzangu tushikamane na tupendane bila kujali dini zetu wala makabila yetu..tuiombee nchi yetu amani na utulivu...daima tuwaombe viongozi wetu ili waweze kutufikisha pale tunapostahili.

Tupambane na tuipende nchi yetu na kuienzi asili yetu kama waafrika na sio kuziruhusu jamii za ughaibuni kututawala kwa kila kitu. Nawatakia kila la kheri katika kuyatafakari hayo machache niliyowaambieni, kwa mafanikio na maendeleo ya nchi yetu.

Naipenda Tanzania, Nawapenda watanzania wenzangu, Mungu awabariki.Ahsanteni!

WATANZANIA TUAMKENI, TUIJENGE TANZANIA MPYA!
 
Upvote 1
Back
Top Bottom