Naipenda Simba SC, ila kwa hapa nawapa heko Yanga.

Umeona ehhh! Ukichambua soka ktk upande wa kushabikia mar zote utashindwa kuleta maana.

Zimebaki wiki chache tu kabla ya Ligi kuanza.. Tutaona Tofauti kubwa sana kipindi hiki.

Jamaa wataanza ligi wakiwa fresh_cold, sisi mpaka wachezaji waweze kuclick na formation ila take time, na uvumilivu wa fans sote tuna ujua.
 
Yanga mbona timu mbovu tuu
Mkuu kuna Tofauti kati ya Kipofu asiyeweza kuona kupitia jicho moja, na kuna yule asiyeweza kuona kupitia macho yote.

wa pili hasimcheke wa kwanza.
 
Unazungumzia kupata uzoefu kwa Yanga kweli? Aisee hatukuelewi ungezungumzia Azam kupata uzoefu tungekuelewa,,

Yanga imeanzishwa 1935 ina umri wa miaka 81 hadi jana ilipokuwa inapelekwa mpera mpera na kitimu kidogo tu cha mwaka 1997 kutoka pale Ghana,,

Labda ulitaka kuelezea issue ingine lakini siyo uzoefu ,, Yanga ni wazoefu wa kufungwa ktk michuano ya aina hii ktk umri wao wa miaka 81.
 
Sasa bahati mbaya hilo wenzetu wengi hawataki kukubaliana na uhalisia, ukisema ukweli unaonekana mamluki kitu ambacho sii kweli

Labda niseme hivi,
Mimi naamini falsafa inayosema adui muombee njaa
Siwezi support yanga KAMWE kutoka moyoni.
Hata siku ya match na TP pale taifa walivyo pigwa nilishangilia sana tu.

Lakini mimi kutoipenda yanga, wala kutoishabikia hakuipunguzii yanga uwezo wake

Hata nikiisuport team yangu wekundu , kama club haijajipanga support yangu haitaongeza any efficiency.

Ifike mahali tukubali kubadilika,
Mpira ni zaidi ya ushabiki nazi na zomeazomea..
 
Ni kweli aisee. Inaonekana sisi Mashabiki wa SSC tumeridhika kuizomea Yanga pale inaposhiriki michuano yao, na wala hatujiulizi ni vipi na sisi tutashabikia cha kwetu.

Ili chetu kiwe bora yatupasa kunyanyua sauti na kukisema kisicho sawia.

La sivyo kila kabla ya msimu tutakuwa watu wa kuamini kuwa "Msimu ujao ni wa kwetu"
 

Ulimsikia lakini kocha wa madema na timu captain. Au unahorojoka tu. Wamesema kwenye huu ukanda wa africa mashariki na kati wanazijua timu mbili tu. Nayo ni Simba na Gormahia ya kenya. Nenda huko wewe huwezi kuwa wa msimbazi wewe ni wajamgwani tu unataka kujifariji.
 
KWA HIVYO KOCHA WA MEDEAMA AKISEMA KWAMBA ANAITAMBUA SIMBA SC & GOR MAHIA TU...

KUTAIFANYA SIMBA SC ICHUKUE UBINGWA MSIMU UJAO?

KUTAIFANYA SIMBA IONGRZENGE UBORA WAKE?

KUTAIFANYA SIMBA SC ILE YA MIAKA YA AWALI ITUDI TENA.?

KUTAIFANYA YANGA IPUNGUE UBORA WAKE ULIO NAO SASA?

Fikiria sana! Tumia akili.... Itakusaidia.

 
Kuwalazimisha Simba wasizomee Yanga ni kupoteza muda. Ajenda hapa ni kufanya vibaya kwa Yanga kwenye mashindano haya tofauti na matarijio ya Watanzania. Tatizo nini? Nini kifanyike?

Huu ni mwaka wa 18 tangu Yanga ilipocheza hatua za makundi ya klabu bingwa Afrika. Matarajio yalikuwa makubwa, kwamba wamejifunza mengi lkn inaelekea wanaweza wasivunje rekodi ya mwaka uke walipoishia pointi 2 tu. Hii ndio ajenda kubwa badala ya mtoa mada kujifariji na kuboronga kwa Simba ktk ligi msimu uliopita alipaswa kujiuliza haya ndio ya muhimu kwa sasa
 
Simba itachukuaje ubingwa wakati Tff na Marefa woote wanataka Yanga ishinde tu,,

Kila mechi lazima ipewe penati au timu pinzani ichapwe red Card,,

Huku kwenye makundi ujinga huu hakuna,, kwa kuionea sn Simba ndiyp maana ikienda huko inapasua sn.
 
Wewe unaumwa Minyoo ya Ubongo. Ama sivyo unaugua kifafa kama alivyo wa jina wako Lil Wayn
 
Simba itachukuaje ubingwa wakati Tff na Marefa woote wanataka Yanga ishinde tu,,

Kila mechi lazima ipewe penati au timu pinzani ichapwe red Card,,

Huku kwenye makundi ujinga huu hakuna,, kwa kuionea sn Simba ndiyp maana ikienda huko inapasua sn.
Dah! Uwezo wa Kufikiri umegota ukuta?

Kusema Marefa wote na Viongozi wote wa TFF ni Mashabiki na wanaipendelea Yanga ni 'Umama'
 
Kuwalazimisha Simba wasizomee Yanga ni kupoteza muda. Ajenda hapa ni kufanya vibaya kwa Yanga kwenye mashindano haya tofauti na matarijio ya Watanzania. Tatizo nini? Nini kifanyike?

Sijasema kuwa Mashabiki wa Simba tusiwazomee Yanga. Ila wewe Kipofu usiyeona kupitia macho yote 2 utamchekaje yule Kipofu asiyeona kupitia jicho 1?

Ninachomaanisha ni kwamba sawa tuendelee kumcheka Yanga kwa nguvu zote ila tusisahau na sisi kujicheka.

Kwani Ubora wetu Simba unafanana na Yanga kqa sasa! Jibu ni hapana. Hata ikiletwa mechi kesho tu... Nina imani kuwa kampuni za kubashiri zitampa point nyingi Simba na kidogo kwa Yanga. (Kama utakuwa umenielewa)

Nilichozungumza awali ni kuwa wenzetu wamesajili vyema zaidi ya sisi ndio maana wapo hapo walipo na sisi tupo kule tulipo (licha ya wao kufanya vibaya), bado wana nafasi ya kufanya vyema zaidi msimu ujao kwa kuwa wamejifunza kutikana na kushindwa kwao leo. [/b][/B]
 
Huu ni mwaka wa 18 tangu Yanga ilipocheza hatua za makundi ya klabu bingwa Afrika.

Unapo sema hilo pia usisahau kuwa hata sisi tuna Miaka 13 tangu mara ya mwisho tucheze hatua ya makundi CAF

Na tuna Miaka 8 pia tangu tushiriki michuano yoyote ile inayo ratibiwa na CAF.

Tuna Tofauti gani na wao wa miaka 18? Au ndi hiyo miaka 5.
 

Naona bado tunapishana kiswahili. Ajenda hapa ni Yanga ya kimataifa dhidi wa wakimataifa wenzao. Simba haishiriki michuano hii. Kujadili kwa kulinganisha mafanikio ya Yanga dhidi ya Simba kwa sasa ni kupoteza uelekeo.
 

Bado hoja zako hazijibu hali halisi ya kwamba Yanga ifanye nn kuvunja rekodi ya pointi 2 za miaka ile. Nadhani hiyo ndio hoja ya msingi kuliko kuzungumzia timu hiyo unayoita yenu ambayo haipo kwenye mashindano haya
 
Nyinyi wanasimba jamani tuache ushabiki tuongee soka yanga kwa sasa sio saizi yenu msijisifie ujinga wanamsimbazi tengenezeni timu
 
Acheni unazi wanasimba mnaposema yanga anapendelewa ni sawasawa na Tania ya mwanamke ya kulamika eti tunapendelewa kwanni nyinyi msipendelewe jiulizeni,yaani wanasimba inaonekana hamjakomaa kisokacnimegundua nyie ni washabiki ila sio wanasoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…