Taratatibu tu tutajenga taifa la waafrika lililoungana na lenye nguvu ya kutosha.
Mwafrica wa kike, I respect you..hahaha. heshima mbele mtu wangu. Nilikuwa nimefurahi ulivyosema kuwa"tutajenga taifa la africa siku moja", mawazo mengi yakanijia kujiuliza kama hicho kinawezekana. Kitu nilichojifunza ni kwamba, mtu ukiwa nje ya africa, ukiwa umezungukwa na mawazo ya wazungu ambao hata hawajui vizuri africa ikoje na matatizo yake yakoje etc, unaweza ukashangaa unaathirika na mtindio wa ubongo wa akili za wazungu. ukajawa na ushauri wa wazungu ambao ni wa juu juu tu, ambao haujafanyiwa research kiundani. hii kitu ogopa sana. Nikiwa huko, watu wengi huwa wanasema"jengeni africa iwe moja"hasa federation. lakini hawaijui africa vizuri, cha kwanza wanaongea hivyo wakiwa biased halafu ni wapungufu wa mawazo yanayotoaga majibu sahihi.
Fikiri, nchi moja, inayogombaniwa na makambare kama manne hivi,(Arabs, chinese, Western countries,etc), ambazo kila kambare lina interest zake, ziungane kuwa nchi moja. wakenya wana mawazo yao, wasudan wana mawazo yao, wasomali ndo kabisaa, south na mawazo yao ya kuua waafrica wenzao, west africa ndo kabisaa, waarabu wa africa kaskazini ndo mpaka leo huwa wanajitambulisha kuwa wao sio waafrica hata wakiwa nje...wasije wakaonekana kama maskini. maendeleo ya hizi nchi ni tofautitofauti, kila nchi ina historia yake mpaka hapo ilipofikia na ina malengo yake iliyojipangia kufikia. kuna uneven development and distribution of natural resources sana hapa africa. Je, hao ambao ni ahueni, watakubali wawabebe hawa ambao ndo mahututi?, hao wenye ardhi kama tz watakubali hao ambao hawana kama wakenya?, Je, hao ambao wameendelea kidogo kama s.africa, si kila mtu atahamia kule na kusababisha fujo kama zile za kuuwa wahamiaji?, nchi zingine ndo zitakufa kabisa badala ya kuendelea.
nchi zingine ndo zitakosa kabisa wataalam, kwasababu ile free movement itasababisha watu waende kule wanakolipa zaidi. mimi kama lawywer, nitaende sehemu yenye mzunguko mzuri wa hela sehemu nitakayo pata clients wengi kuliko sehemu ambayo watu wana matatizo lakini wananyambaza kimya bila kumtaka lawyer kwasababu hawana hela ya kulipa.
Kilichobaki hapa mkuu, ni kila mtu aendelee kivyake tu, labda cha kufanya ni kushirikiana kimachale tu kwa regional organisations ili kwa groupings kama hizo, kodi zipunguzwe kibiashara nchi na nchi, kutembeleana nk. ila halitakuja liundwe taifa la afrika, kama lilishindwa kuundwa kipindi kile cha kupigania uhuru. Kama una swali uliza.