Nairobi: Shule ya Jamhuri yafungwa baada ya kuibuka vurugu zilizosababishwa na ubaguzi wa kidini

Nairobi: Shule ya Jamhuri yafungwa baada ya kuibuka vurugu zilizosababishwa na ubaguzi wa kidini

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Takribani wanafunzi 35 wa Shule ya Sekondari Jamhuri jijini Nairobi wamejeruhiwa vibaya katika ugomvi uliohusu madai ya ubaguzi wa kidini na kupelekea Shule hiyo kufungwa kwa muda usiofahamika.

Baadhi ya wanafunzi walichomwa visu katika ugomvi huo ulioanzia siku ya Jumanne ambapo mwanafunzi wa Kikristo(form 4) na wa Kiislam(form 1) walitofautiana katika bwalo la chakula.

Suala hilo lilifikishwa mbele ya Mkuu wa Shule, Fred Awuor ambaye alisuluhisha lakini ugomvi ukaanza tena mapema leo(Jumatano) baada ya (inavyosemekana) mwanafunzi mwingine wa Kiislam kutolewa katika mstari wa chakula baada ya kuwapita wenzie.

Wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo wanamshutumu mkuu huyo wa shule kuwa anawabagua Waislamu na kupendelea Wakristo ambapo mmoja alieleza kuwa masomo yanafanyika hadi saa kumi na nusu jioni na kuwazuia kuswali na pia kuwekwa kwa ulizi mkali eneo la msikiti wakati wao si magaidi.

Ugomvi huo umetulizwa baada ya Kamanda wa Polisi wa Nairobi, Japeth Koome kufika shuleni hapo na majeruhi wamekimbizwa hospitali.
Jamhuri-Boys-III.jpg

===========

At least 35 students were seriously injured during a fight over unfair treatment at Jamhuri High School in Nairobi.

Some of them were stabbed during the chaos that started on Tuesday when a Muslim and a Christian reportedly differed in the dining hall.

Students who spoke to The Star on Wednesday said the Muslim was in form one and his schoolmate in form four.

The matter was reported to principal Fred Awuor who calmed the students but trouble started again on Wednesday.

This was reportedly after another Muslim student was taken off a queue to the dining hall for getting ahead of his schoolmates.

"The matter worsened and even escalated to the classrooms. The principal came but he was roughed up by our Muslim schoolmate," one of the learners said.

Muslim students accused Awuor of discrimination and favouring their Christian counterparts.

Learner Mohammed Gulled said: "He is the person diving us. Christians are favoured. We have lessons until 4.30pm so we cannot pray. He has brought guards who are now in charge of the mosque. That is not right. We don't carry bombs to this place."

But Awuor reported that the problem began last evening when the two students fought outside the school compound. He said matters escalated today.

Several security officers led by Nairobi police commander Japeth Koome rushed to the school and contained the situation. Those injured were taken to hospital.

Religious leaders, education officials, parents and teachers went to the school to counsel students.

Source: Star.co.ke
 
Hekima inahitajika, msipokuwa makini hii inaweza kutapaka mpaka kwenye mashule mengine.
 
Kenya sio sehemu salama ya kuishi ndio maana walipotoa nafasi madaktari wa tz waende nilimzuia mdogo wangu kuaply bora tu tuendelee kufua vyuma huku tz.
 
Ila alievuka wenzie dinning ni mgomvi. Hapo walikua wanatafuta tu sababu ya kutolea hasira zao.
 
Nilikuwa napendaga sana wakinivuka kwenye foleni nikiwa shuleni. Zangu zilikuwa tu kutaim ili niwai ule ukoko wa wali sufuria ikifika level ya chini kabisa. Yum yum. 🙂 Nikikupa nafasi univuke udinde hapo nakumark kama adui yangu nambari wani. Yatayokukumba baada ya hapo lawama inakuwa ni kwako tu. Wanafunzi wa siku hizi ni vilaza sana.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Vyote kwa pamoja!
waende seminary...kusali hakutakiwi kuingilia ratiba ya masomo rasmi, na masomo yasiingilie uhuru wa kusali.
mimi mkatoliki, natakiwa kusali sa sita kamili mchana, na nipige magoti...kama nipo darasani nitamwambia mwalimu aondoke au?
 
Ila hawa wenzetu wanapenda kulalamika sana kwa kila kitu, wanasema wanaonewa na "m.akafir"
 
Hiyo ni dhambi ya ubaguzi inaendelea kuwatafuna wakenya, mkishaanza kubaguana kwa kabila, mtaendelea tu, ni sawasawa na kula nyama ya mtu, hamuwezi kubaki salama.
 
Back
Top Bottom