Nairobi to host US’s Power Africa project

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
65,136
Reaction score
91,917
POSTED WEDNESDAY, NOVEMBER 20, 2013 | BY- YVONE KAWIRA


Nairobi to host US's Power Africa project

Nairobi will host the regional headquarters of an initiative led by US President Barack Obama to





By YVONE KAWIRA



Nairobi to host US

MY TAKE
Hii imekaa vipi? au Kikwete anaendelea tu kukosa maarifa bila kuwekeza kwenye elimu na miundombinu? Ni wakati wa Kikwete kujiuliza Nairobi inaipita wapi Arusha au Dar es salaam kwenye kuvutia taasisi hizi muhimu za kifedha?

Jibu ni serikali ya Kikwete haina mbele wala nyuma katika kuwekeza katika kuifanya Dar kitovu cha ukanda huu haswa kwenye rasilimali watu na miundombinu haswa shirika la ndege madhubuti litakalorahisisha muingiliano mzuri unaotokana na shughuli za taasisi zenye utegemezi nje ya nchi!

Tutaendelea kukirimu Marais waje wapige saini magogoni lakini ofisi zipelekwe nje tukibaki kukosa fursa zitokanazo na uwepo wa ofisi hizo! Au tutaendelea kutumika katika kuiringishia Kenya na kubaki watupu maana hatujui ku-lobby ilitakiwa baada ya saini ya Obama on Power Africa Kikwete atume ujumbe kuhakikisha na ofisi zinakuwepo hapa Tanzania na si kuridhika na ujio tu!

Kiukweli Arusha inaweza kwenda sambamba na Nairobi kama jiji lile likiwezeshwa ipasavyo kimiundombinu maana mbali na hali ya hewa (kigezo cha Wamagharibi kuipenda Nairobi), ukaribu na Nairobi uoto asili vinaweza kuiweka Arusha katika nafasi bora zaidi ya kiushindani ukilinganisha na Dar au Mwanza. Hime sasa tuamke tujaribu kufanya Arusha kuwa kitovu cha biashara na fedha !
 
NOTHING BAD;mwandishi vyone kawira ametumia vyema taaluma yake ktk kuandika lugha nzuri yenye kuvutia,haipaswi kuona wivu,KWANI FEDHA ZOTE ZIMESHAPANGIWA MIRADI YAKE
 
NOTHING BAD;mwandishi vyone kawira ametumia vyema taaluma yake ktk kuandika lugha nzuri yenye kuvutia,haipaswi kuona wivu,KWANI FEDHA ZOTE ZIMESHAPANGIWA MIRADI YAKE
elewa nilichoandika na si unarukia bila kupata nilichomaanisha, Tanzania haishindwi kuwa na taasisi kama hizi kama kunakuwa na mikakati na mipango maalum
 
Sisi tunafurahia kupiga picha na hawa jamaa. Wenzetu Wakenya wapo kimaslahi (uchumi na maendeleo) zaidi!

Kama hii habari ni kweli; wengi watasema ni bora Obama hasingekuja kuzindulia huo mradi wake nchini Tanzania. Lakini tujue kuwa serikali yetu ni dhaifu sana na wakuu wa mataifa mengine wanalitambua hilo!

Tunatamani vitu viwepo lakini tunakosa utashi na maamuzi stahiki! Sote tunajua Arusha ni mji unaopendwa na wengi na unavuma sana duniani.
Nairobi ikipata shida wazungu wengi ukimbilia Arusha! Arusha ni kitovu cha utalii ndani ya EAC! Sasa ujiulize huo mjini umekuzwa vipi kimiundombinu na huduma za kijamii?

Sisi tunachojua ni Dar! Kila mtu anaiwaza Dar, serikali inaiwaza Dar hadi tumesahau umuhimu wa miji mingine! Kila kitu kinawekwa Dar. Tunasahau kuwa wageni wengi hawapendi mazingira ya Jiji la Dar! Dar yenyewe ishafurika! Huduma zote muhimu ulazimisha muelekeo wa watu na magari uwe ni upande mmoja!

In short Dar is not condusive for any serious and sustainable investor!

Laiti serikali ingejua kuna umuhimu wa kuendeleza miji mingine kimkakati badala ya kuipa hiyo miji hadhi ya majiji kwa sababu tu ya ongezeko la watu na magari!

Tujipange upya!

<Jp>
 
tusipende kukuza mambo, kenya wametuzidi tangu kabla hatujapata uhuru, tangu tukiwa koloni walikuwa wametuzidi mpaka leo, sio tu kwa mazingira au vijana kwenda shule hata fedha/uchumi yao inaonekana.

Wazungu miaka hiyo tukiwa koloni walishaichagua kenya kuwa hub ya africa na east africa,maofisi mengi ya nchi yako pale tangu utumwa.

Kwa hiyo hilo halina haja ya kumlaumu kikwete,maana itatuchukua muda kulingana nao,unaposema elimu bora vyuoni au sekondari unazungumzia vifaa na maabara za uhakika na ukumbwa wamiundombinu pamoja na waalimu bora ambavyo vyote ni pesa.

Tunachoweza kufanya ni kuinua sector moja moja kama tunavyojaribu sasa katika utalii,miundombinu,kilimo na nishati.

Ni mtazamo tu wapinzani msijenge chuki.
 
kwa maana hii kwa hiyo unapasisha serikali ya Kikwete kutokuwa na mkakati wa kubadili hilo sio? Kweli una fikra mgando, amka...! yawezekana tukashindana vilivyo angalia Qatar inavyoshindana na UAE tutumie mbinu zile kushindana pia hapa Afrika Mashariki
 


Mkuu Geza Ulole raisi wetu amefurahia tu kuitwa kaka mzuri.

Lakini hiyo akili ya kulobby ili Tanzania kuwekwe ofisi ya makao makuu ya huo mradi wa umeme hatuna na hatutakuwa nayo under this regime.

Sisi tulifurahia ujio wa Obama mwezi June wakati huo wakenya walikuwa wamenuna lakini sasahivi wao ndio watafurahia na kufaidika na mpango huo ambao ulitiwa saini nchini kwetu wakati sisi tunabaki kukodoa macho tu. Bila shaka walijua udhaifu wa serikali yetu na wakautumia kufanya lobbying ili ofisi za mradi huo ziwekwe Kenya na wamefanikiwa. Wamejipatia ajira kwa watu wao na bila shaka watalipwa vizuri na serikali kwa upande mwingine itajiokotea kiasi Fulani cha kodi.

Wasawahili wanasema achekaye mwisho ndiye hucheka zaidi, sasa ni wakati wetu wa kununa watanzania wakati wenzetu wakenya meno yote thelathini na nje yako mbili.
 
Last edited by a moderator:
Kikwete alipotoa hotuba bungeni juu ya jumuia ya Africa mashariki wengi walimpongeza, mimi niliuliza humu (nilichangia uzi fulani) kwamba hivi sisi tunauzaga nini kwenye hi jumuia? Kenya walituma ujumbe haraka sana Tanzania kama kuomba msamaha hivi, Uganda hali kadhalika, issue iko hivi, kuanzia viongozi wetu wa juu, wasomi (mfano Sospeter Muhongo) na wananchi, tuko visionless hasa kwenye mwelekeo wa nchi yetu, wenzetu hawafurahi kupata wageni, wanajua jinsi ya kuzitumia nafasi, kama hata maji ya kunywa yanaingia nchini toka nje ya nchi, sisi tunaweza nini? Tumekalia sifa za kijinga tu, kwetu cha muhimu ni ccm kua salama hata kama nchi itaangamia!
 
Binafsi mie sijaona jipya hapo zaidi ya hilo la kwamba Regional HQ itakuwa Nairobi!! Hii Power Africa ni project ya nchi zaidi ya moja kwahiyo ni lazima HQ ingekuwa kwenye moja wapo ya nchi hizo! Nairobi ina some competitive advantage compared to Dar es salaam! Kwanza, kwa ukanda huu nchi zilizotajwa ni Tanzania, Kenya na Ethiopia! Kenya ni kama centre ya hizo mbili na vilevile ni rahisi kufikika kutoka Nigeria na Liberia; other partners in business!

Kwa upande mwingine, makao makuu yatakuwa kwenye US Embassy, so kama ilionekana US Embassy in Nairobi inaweza ku-accomodate vizuri hizo operation then there's no way uwaambie waje Dar es salaam! Aidha, hiyo ofisi kuwa Ubalozini ni kwamba itakuwa just for administrative purpose. Ingekuwa ni ofisi inayohitaji pilikapilika nyingi with several workforces, basi hiyo makao makuu ingekuwa na eneo lake.

But all in all, bado naona Tanzania ndio tuna nafasi kubwa zaidi ya kufaidika na huu mpango hata kama HQ ipo Nairobi. Tayari Tanzania kuna mipango inayoonekana kutoa dalili za kuwa na umeme wa ziada; ambao unaweza kutumika kwenye hiyo program ya Power Africa for Kenya ambayo bado hawana mipango iliyo tayari inayoashiria kuwa na surplus in electricity unless kama project itajikita kwenye off-grid power supply alone!
 
Kwanza, kwa ukanda huu nchi zilizotajwa ni Tanzania, Kenya na Ethiopia! Kenya ni kama centre ya hizo mbili na vilevile ni rahisi kufikika kutoka Nigeria na Liberia; other partners in business!

Mkuu NasDaz hapa ndipo unaona umuhimu wa kuwa na National Airline. Nairobi inafikika kirahisi kutoka Nigeria na Liberia kwakuwa kuna direct flight za Nairobi-Lagos na Nairobi-Monrovia.

Kama ATCL ingekuwa alive ina ndege za kutosha na ina route za kutosha katika nchi zilizoko kwenye hiyo project ya power Africa pengine Dar es salaam ingeweza kufikiriwa kushindana na Nairobi katika kuwa host. Sasa ukiangalia KQ inavyotamba barani Africa na duniani kwa ujumla basi hiyo inawapa advantage kubwa wakenya kunufaika na miradi mingi kuliko neighboring countries.



Mkuu there is no way Tanzania inaweza kunufaika na project hii kuliko Kenya, sisi Tanzania tuna mipango mingi sana kwenye makaratsi wakati wenzetu wana mipango mingi inayotekelezeka on the ground.

Hapa tukubali tukatae nchi yetu inakosa kabisa visionary leaders katika utawala huu wa Kikwete na ndio sababu hata maraisi wa nchi majirani wanaweza kuthubutu kumchezea sharubu bila wasiwasi wowote.

Mkuu Profesa Muhongo ameahidi nchi yetu kuuza umeme kwa majirani by 2015 lakini ndani ya kipindi kifupi tumeingia kwenye mgao, sasa hapo ndipo utakapoona tofauti ya watanzania na wakenya.

Kwamuda mrefu sana wakenya hawana mgao wa umeme wakati sisi tuna vyanzo vingi na vikubwa zaidi vya umeme kuliko wao. Kwa taarifa yako sasahivi wakenya wana mipango kabambe sana ya miradi ya umeme katika kila county hasa zile ambazo hazijaunganishwa kwenye national grid.

Ili tuweze kupata kafanisi japo kadogo katika sekta ya umeme ni lazima shirika la TANESCO livunjwe. Kama viongozi wetu wangekuwa makini na visionary hadi wakati huu tunapoandika hapa suala la kuligawanya shirika la TANESCO ingeshakuwa historia.

Kenya walikuwa na matatizo ya mgao wa umeme kama sisi miaka ya nyuma. Lakini walipobaini tatizo lao kuwa ni Tanesco yao waliamua mara moja wakaligawanya shirika lao na sasahivi kwao mgao wa umeme ni historia na hakuna kukumbushana historia ya mgao wa umeme kama anavyotufanyia sasahivi Profesa Muhongo.

Kenya wana mashirika makubwa mawili yanayoshughukika na umeme, wana shirika la KENGEN ambalo kazi yao ni kuzalisha umeme tu. Na wana shirika la KPCL ambalo jukumu lake ni kusafirisha na kusambaza umeme tu. Sasa kama tutaendelea kujidanganya kuwa sisi ndio sisi bila kutaka kuuangalia ukweli ni dhahihiri na hakika kuwa tutaendelea kuwa wasindikizaji hata mbele ya majirani zetu kila kukicha.
 
Last edited by a moderator:
Yaani mkuu wangu mjadala wa National Airline unau-force uje huku? Hapana bana, tukamalizane tu kulekule lakini labda niseme kidogo tu kwamba wala haileti maana kwamba Nairobi imechaguliwa kwa kigezo cha kuwa na Kenyan Airline! Naamini kuna factors nyingi zimehusika. Kwa mfano, hii Power Africa Initiative ipo pamoja na Trade Africa Initiative. Hakuna asiyefahamu ni namna gani Nairobi walivyopiga hatua kibiashara as compared to Dar. Hiyo inaweza kuwa ni moja ya sababu including the fact kwamba as for now Nairobi ndiyo East and Central Africa Gateway(sio wana shirika la ndege la serikali) na vile Nairobi ipo Centre kwa Ethiopia na Tanzania!
Mkuu wangu unaweza kunipa maelezo kuhusu implementable power/energy program in Kenya? Ukiniuliza kuhusu Tanzania, nitakujibu kwamba kwa sasa tunajenga Bomba la Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. What about Kenya?
Mkuu Profesa Muhongo ameahidi nchi yetu kuuza umeme kwa majirani by 2015 lakini ndani ya kipindi kifupi tumeingia kwenye mgao, sasa hapo ndipo utakapoona tofauti ya watanzania na wakenya.
Mkuu wangu ikiwa base yako ya kuhoji uhalali wa kauli ya Muhongo inaegemea kwenye mgao wa sasa; basi ningependa kukukumbusha kwamba kauli ya Muhongo inategemea mambo makuu mawili; time (by 2015) and completion of ujenzi wa bomba la gesi! Hayo yote mawili bado hayajifikia muda wake! Mosi, 2015 bado haijafika na wala hilo bomba halijaisha(construction inaendelea)! Hata hivyo, nakiri wazi kwamba Tanzania tuna tatizo kubwa la umeme; halina mjadala! Lakini katu siwezi kujitia upofu na kujiaminisha kwamba ni tatizo linaloweza kwisha over night! Neither CCM nor CHADEMA can finish power problem in the country within few years. Hii nchi tulishabugi toka zamani inagwaje wengine ukiwaambia hivi wanakuja juu! Yaani kwa sasa ni kama tunaanza karibu kila kitu! mambo ambayo yalitakiwa kufanyika 30 years ago yanafanyika sasa....hili ni tatizo!
Hongera yao ingawaje sio muda mrefu kihivyo! Nairobi pale kulikuwa na mgao wa umeme just two years ago! Au hii miaka miwili ndiyo unaita muda mrefu sana? If so, inawezekana upo right na labda tatizo lipo kwangu! Binafsi nimesoma Agricultural Economicsna unaposoma Credit Management, unakutana na masuala ya Short Term Credits, Medium and Long Term Credits! Kama kiswahili changu kinaendana na kidhungu basi hiyo "Kwamuda mrefu sana" uliyoisema wewe naweza kuitafsiri kama Long Term ambayo ni beyond 15 years lakini hiyo miaka miwili haijafikia hata kwenye medium term...ni hayo tu katika hili!
Hilo la TANESCO ni tatizo, ukiona mtu anakataa ubovu wa shirika hili basi huyo mtu atakuwa anapaswa kuchunguzwa vizuri; inawezekana ana matatizo makubwa. Ndani ya TANESCO hakuna kabisa efficiency, ni full matatizo kutoka utosini hadi nyayoni.
 
ina maana mkuu hujui kivp kukua kwa biashara na uchumi hurahisishwa kama nchi ikiwa na superb logistics na pia strong financial institutions au una-pretend kutojua kwamba easy connectivity ilikuwa criteria ya kuamua wapi headquarters za power Africa ziwepo?
 
Kaka huwezi kuwa na nafasi kwenye kupokea miradi mikubwa kama hii kama nchi haina wataalam.Tanzania kila kitu ni siasa
 

Kama tungekuwa serious hii miaka 52 ya uhuru tungekuwa tumepiga hatua zaidi ya Kenya ukichukulia kuwa tuna ardhi kubwa, rasilimali nyingi na population kubwa kuliko ya Kenya. Wa kulaumiwa hapa siyo Kikwete basi ni CCM!!!
 
Hamjayajua mataifa makubwa nyie...hapo utakuta US imekasirika ...kuna kitu tu ...hasa hii ya kuwachanganya na mahasimu wao China...

To me waende zao....Kenya alikuwa best wa mabepari long time kitambo...nothing new....
 

Matarajio yote tuliyokuwa nayo kwenye mradi huu wa OBAMA tunaishia kupata; Tanzania- 10 MW, Poor Tanzania
 

Dah, hii imenigusa sana! Yaani pamoja na mradi kuzinduliwa hapa Bongo tumezubaa hadi makao makuu yanapelekwa Nairobi!? Yaani inakera na kuumiza mno!!
 
Mkuu wangu nitakuwa mtu wa ajabu nisifahamu umuhimu wa hayo mambo! What am saying ni kwamba decision of where to HQ was US decision...am certain hawa watu ni very smart; they can only make decision favorable to their interest not to someone's! Nairobi has favorable condition than Dar es salaam; various business firms, and some being Americans firms, operating in TZ are HQed in Nairobi! So, why should Power Africa HQ Dar and then communicating with these firms remotely while there's great chance to work with them physically if they HQ in Nairobi? Why should US make the decision to favor Tanzania at their expenses?! No lobbying here, this's all about business! Don't forget, even USAID, Regional HQ ipo Nairobi, showing that key HR are already in Nairobi! Hii Power Africa nayo ipo chini ya USAID. Key partner in this initiative ni African Development Bank Group ambayo Regional Resource Centre nayo ipo Nairobi! Unless we'd some leverage, but Nairobi had all it take to be the HQ of Power Africa Regional HQ! You and I, both would prefer it to be in Dar es salaam, na kama vipi iwe Lindi kabisa nyumbani kwetu but this ain't no political game where some irrational decision may be made to favor this or that! Ni ukweli mchungu but we need to accept it hata kama itabidi kuushushia kwa kitu milk! Tusione taabu kukubali kwamba as for now, Nairobi tayari wana necessary infrastructure na ndio maana since then it'd been the HQ of various International Organisation.
 
Dah, hii imenigusa sana! Yaani pamoja na mradi kuzinduliwa hapa Bongo tumezubaa hadi makao makuu yanapelekwa Nairobi!? Yaani inakera na kuumiza mno!!
Ungekuwa unafuatilia miradi ya wazara ya nishati under BRN,( ipo 29) ungejua kuwa Kenya hawana cha kutuzidi. Mradi wa Mtwara ambao ni wa TANESCO na Symbion (ya Marekani) ni 600 - 800MW. Bomba la gesi 2015 na miradi ya uzalishaji Dar ni karibu 3000MW. Ngoja bomba la gesi likamilike utasema. Utawasikia kenya wanataka bomba liende kwao.
 
Nairobi itaserve vizuri na Ethiopia na hizo nchi za west africa zilizo kwenye hiyo project kuliko Dar (relative long distance) na Arusha( udogo wa mji)..hii program tuseme infekua inaserve zaidi nchi za kusini kama zim, zambia, malawi, etc nafikiri Dar ingekua kitu kizuri zaidi ya Nairobi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…