Nairobi yaanzisha sheria ya nidhamu na usafi wa Umma

Nairobi yaanzisha sheria ya nidhamu na usafi wa Umma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kulingana na sheria hiyo mpya, ni hatia kuendesha pikipiki au magari kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu, kupiga muziki wa kelele au hata kuvuta sigara kwenye maeneo ya umma ambayo hayakutengewa hilo. Thomas Lindi ni mratibu katika shirika la kupambana na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake KETCA na huu ndio mtazamo wake.

Atakayepatikana akifuta pua bila ya kutumia kitambara maalum anaweza kutozwa faini au hata kufungwa jela kwa miezi sita au mwaka mzima. Watakaopatikana wakijisaidia haja ndogo kwenye maeneo ya umma yasiyokuwa ya msalani, kutema mate ovyo njiani, kulala jikoni au kwenye vyumba vya kuhifadhi chakula vya mikahawa nao pia watakuwa wanakiuka sheria. Anna Oyoo ni mfanyabiashara jijini Nairobi na anaelezea umuhimu wa kuwa na sheria kama hii.

Sheria hii pia inawabana watakaopatikana wakimwaga maji machafu barabarani, kumimina maji, mafuta na uchafu kwenye mabomba ya maji taka au hata kuweka vizuizi barabarani. Huku yote hayo yakiendelea, Waziri wa Maji nchini Kenya Sicily Kariuki, anasisitiza kuwa wako mbioni kujenga na kuongeza idadi ya mabomba ya maji taka kuuondoa uwezekano wa wakaazi kuvunja sheria.

Kadhalika wamiliki wa nyumba na majengo wanapaswa kuhakikisha kuwa miti na maeneo ya bustani kamwe hayazibi njia au barabara. Kulingana na Mwanasheria Mkuu wa serikali ya kaunti ya Nairobi Lydia Kwamboka, sheria hiyo itafuatiliwa kwa makini hivyo basi wakaazi lazima wadumishe nidhamu. Mswada huo wa usafi na nidhamu uliwasilishwa kwenye bunge la kaunti ya Nairobi na mwakilishi wa wadi ya Riruta Kariuki Kiriba.
 
Dar es Salaam waweke pia hizi sheria, kila siku nasumbuliwa na vibajaji ktk njia ya watembea kwa miguu, boda boda ndio vinara wa kuvamia hifadhi za watembea kwa miguu
 
Nairobi wanatushinda pakubwa wa dar es salaam,
Na tatizo ni usimamiaji na ufuatiliaji wa hizo sheria,
Hembu jaribu kupita leo kariakoo uone jinsi malori yalivyozuia barabara kiasi cha kuzuia watumiaji wengine, hilo mamalaka inalipuuzia lakini iko siku madhara yake yatakuwa makubwa sana,
Malori ni kero kubwa sana hasa kwa wakazi wa kariakoo sembuse sie wapita njia,
Ni kama vile mamlaka hazipo
Hopeless,
Big up Nairobi
 
Back
Top Bottom