Naishauri Serikali ifunge Uvuvi wa Samaki katika ziwa Victoria kwa muda wa miezi sita

Naishauri Serikali ifunge Uvuvi wa Samaki katika ziwa Victoria kwa muda wa miezi sita

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Samaki katika Ziwa Victoria kama vile wamekwisha kabisa. Wavuvi wanatumia gharama kubwa sana na mwisho wa siku hakuna faida wanayopata kutokana na ukosefu wa samaki.

Pili Ziwa Victoria imechafuliwa na kila aina ya uchafu na hivyo kupelekea kutozaliana kwa samaki. Kutokana na sababu hizo naishauri Serikali kufunga Ziwa Victoria kwa muda wa miezi sita ili kusiwe na uvuvi wa aina yeyote ili samaki wazaliane kwa wingi vinginevyo Ziwa Victoria itabaki kuwa ni jina tu bila manufaa yeyote.
 
Ziwa Tanganyika lilifungwa kwa miezi kadhaa hivi karibuni, limefunguliwa siku chache zilizopita.

Nadhani hata Ziwa Vikitoria nalo litafungwa siku za usoni.
 
Na ndio inavotakiwa, uvuvi ufanyike Kwa msimu. Kunakuwa na msimu wa kuvua na msimu wa kuacha samaki wazaliane. Miezi sita ni sahihi kabisa, ziwa sio bahari.
 
Mnajuwa kuvua tuuuu

Kutunza maZingira ya ziwa hamjuwi.....

Ova
 
Kweli kabisa samaki Kwa Sasa wamekuwa kipengele!!

Nadhani iwekwe ratio sawa yaani wanavua Kwa miezi3 na linafungwa Kwa miezi 6 hii itasaidia sana.

Pia uvuvi haramu umerudi Kwa Kasi sana.
 
Back
Top Bottom