Tangia Tundu Lisu alihutubie Taifa, nimejikuta nimepoteza Amani na furaha ya Moyo wangu.
Hotuba ya Tundu Lisu imenigusa mno. Najiona ni mtumwa ndani ya Taifa langu.
Mimi Kama raia katika Taifa huru, napaswa kujitawala, kifikra na kimaamuzi.
Napaswa kuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi ya namna ninavyotaka kuongozwa, na Nani ninamtaka kuniongoza. Maskini mimi, na raia wenzangu, mamlaka hayo hatuna hata kidogo. Kuna watu wamehodhi madaraka hayo kwa hila na hawako tayari kuyaacha. Wapo tayari kupiga raia yoyote mabomu na risasi ili wasipokonywe madaraka hayo ambayo ni haki ya raia wote.
Tundu Lisu amejitokeza kuongoza pambano hilo la kurudisha mamlaka mikononi mwa raia. Na kwa kweli ninapomtazama namuona kabisa yupo serious!
Lakini napowatafakari raia wa Tanzania, naiona kesho ya Lisu. Kesho ya kushindwa pambano, na wale aliojitolea kuwapigania watakuwa wanamdhihaki.
Nawaangalia Taasisi za dini, sioni tumaini la wao kufanya chochote. Nawaona kabisa wakikaa mezani kumpuuza Tundu Lisu, wakiamini kuwa wao wana hadhi maalumu kwenye jamii na hivyo kufuata maoni ya Lisu ni kuonekana Kama wanaburuzwa na Lisu.
Baadhi yao wanaelekea kutoa mawazo kuwa, kumfuata Lisu ni kujenga uadui na serikali, hivyo watashughulikiwa directly au indirectly.
Baadhi yao wanaelekea kujisemea moyoni mwao kuwa, vibuyu vya asali kutoka serikalini vitakauka!
Sioni pia tumaini la vyama vya siasa kuunga mkono hoja.
Nawaona kabisa wakisita kwa kuamini kuwa kumuunga mkono Lisu ni kuzidi kumpa umaarufu.
Nawaona kabisa wakitamani ashindwe na aaibike mbele ya umma wa Tanzania ili umaarufu wake ufifie.
Nawaona kabisa wakitamani harakati za Lisu ziishie katika kukiharibu chama ili wao na vyama vyao wapande daraja.
Kwenye harakati za Lisu, muungano wa vyama vyote pinzani ungekuwa ni silaha kubwa sana,
Najaribu kufikiri iwapo vyama vyote vingesema No reform No election, hii serikali ingepumuaje!
Najaribu kufikiri, iwapo Uchaguzi ungekuwa na wagombea wa CCM peke yao, hawa CCM wangepumuaje!
Hebu fikiri, CCM walivyolazimisha covid 19, ili kuleta dhana ya Demokrasia, unafikiri wangefanyaje kwenye Uchaguzi ambao umekataliwa na vyama vyote?
Kuhusu asasi za kiraia za Tanzania, sizifikirii hata kidogo. Hizo asasi karibu zote zina viongozi wenye kadi za CCM
Nikigeuza macho kwa Raia wenyewe, sioni tumaini hata kiduchu.
Ni ukweli japo mchungu, hakutakuwa na raia atatokea kupambana na serikali hii kuishinikiza mageuzi. Raia wenye element za ujinga ni wengi.
Wengi wao wanaamini CCM ni chama Cha amani na wapinzani ni watu wa vurugu.
Wengineo wanaamini harakati za Lisu ni uroho wa madaraka na anapigania tumbo lake.
Maskini Raia hawajui mateso mengi wanayopitia kwa kukosa mamlaka ya kuwawajibisha viongozi wao
Wapo raia kadhaa wanajua upo umuhimu wa kutafuta mageuzi, lakini wakikumbuka hizo harakati zinaweza kuwafikisha mbele ya bunduki na mabomu ya polisi, wanabaki kuwa wapole!
Hata hivyo, bila kujali Lisu atashindwa au la, harakati zake ni muhimu ziendelee.
Waswahili wanasema, mwanzo wa ngoma ni lele.
Pia wanasema dalili ya mvua ni mawingu.
Haya Mambo ndo yameanza, maana Kuna nyakati hazikuwepo kelele, Sasa zimeanza. Ukimya hautarudi Tena. Kelele hizi zitazidi kupazwa mwaka huu, mwakani na miaka mingine.
Leo Lisu na Chadema, kesho Taasisi za dini ama Asasi za kiraia, ama watumishi wa serikali na hata vyombo vya ulinzi na usalama!!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Tundu Lisu na wanamageuzi wote wa Taifa la Tanzania!