Naishi na virusi vya ukimwi natafuta kama mimi

kuishi na virusi vya ukimwi si tatizo ukishajifunza, mwenye cancer hata malaria yuko kwenye risk kupita mimi.

Kil la kheri dada, maana kwa hali jinsi ilivyo ni wachache kama wewe wenye moyo kama wako.
 

mkuu hebu soma vizuri tena hamanishi hivyo
 
Soma uelewe amesema anataka kama yeye hongera dada
 

Saint Ivuga, hata kama unaishi na mwezio ambae ameathirika ili kupunguza maambukizi mapya unashauriwa kutumia condom, kwani virus vinatofautiana. Kwa hiyo anaweza kumpata aliyeathirika, lakini akawa na virus ambavyo vinaweza kuwa kwake ni maambukizo mapya; mimi sio daktari, nazungumzia general knowlledge.
 
Mi nkupongeze kwa uamuzi wa busara uliotumia tofauti na wale ambao wanajtambua lakini wanajificha ilhali haja ya mwili wanaihitaji.
Mimi kwa vipimo mara ya mwisho yanonyesha si muathirika lakini napenda na kuheshimu sana wanaojitambua na kutambua tatizo. Hongera kwa uamuzi wa busara
 
Alikua bayana kua anatafuta mwenzie wa kumtoa upweke(muathirika) kwa sharti la kutumia zana kuepusha maambukizi mapya! Tuwe makini tunaposoma post @ Saint Ivuga
 
Hiyo saffi sanna dada angu,ila acheni mambo yenu wakware mtajifanya mnataka kumuoa,then mkishamuonja kwa kutumia mipira yenu halafu muingie mitini,yaani sijui mkoje hamna hata aibu maana najua kuna michafuzi itakua imeshaanza kum-pm.
 

Ubarikiwe kuwa wazi kiasi hiki!
 
Daa virusi kweli vinaheshimika yaani watu wanachangia kwa adabu namna hii! Nakutakia Kila la kheri dada.
 
Katika maisha huwa nafurahi sana kuwa na watu wakweli na ambao hawalichukulii tatizo kama tatizo,so kwa moyo safi,naomba nikupongeze dada kwa ujasili wako na uamuzi mzuri uliouchukua wa kutousambaza na kutulia,kwani ni wachache sana wenye huo moyo na mtizamo chanya kama wako,yangu mie ni hayo,MUNGU AKUBARIKI NA AKUZIDISHIE MINGI YENYE HERI HAPA DUNIANI.
 
Aisee, I wish ningekua na qulify! Vipi huitaji negative(asiemuathirika)?
 

hakika umekurupuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…