Naishukuru JF, nimepata mchumba!

Status
Not open for further replies.

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,659
Habari wakuu,
Kama mtakumbuka mnamo tarehe 10 mwezi mei mwaka huu mnamo saa tisa na dakika 50 nilipost thread ya kutafuta mchumba. Ingawa zoezi lilikuwa gumu sana lakini napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatie mchumba bora. Taratibu zote kwa mujibu wa mila nimezifuata na napenda kusema kuwa tutafunga ndoa katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Napenda kuishukuru JF kwa kuniwezesha kupata mchumba bora ambaye natarajia atakuwa mke bora.
Nawashukuru wadau wote walionipa ushauri kupitia jamvini humu na wale waliojitokeza kutaka niwe mume mtarajiwa wao.
Mwisho: Mitandao ya kijamii ni mitandao inayoweza kuleta mapinduzi makubwa sana katika nchi yetu. Tuitumie vema ili tupate maendeleo na tupinge kwa nguvu zetu zote ubeberu wa aina yoyote wenye lengo la kuifungia au kuiwekea vikwazo mitandao ya kijamii, na hapa nazungumzia JAMII FORUM.
Nawasilisha.
 
hongera mkuu usisahau kuniweka m/kiti kamati ya vimiminika
 
Hongera Mkuu. Usisahau pia kutuwekea namba yako ya mpesa ili tukutumie zawadi mida ikiwadia!
 
Angalau hata umekumbuka,ukipata mtoto usisahau kumpa jina mojawapo za avatar humu jamii forums.
 
Siamini macho yangu aisee hebu ni Pm jina la wifi nimpongeze wifi yangu khaa kumbe inawezekana.
 
Angalau hata umekumbuka,ukipata mtoto usisahau kumpa jina mojawapo za avatar humu jamii forums.

hongera wewe kidume mtandao umekulipa hongera usisahau kuweka no ya M.PESA ikibidi naaa.......pasward tukuongezee Baraka zaidi
 
paka kipofu hula panya waliokufa
hongera sana huyo mchumba umempata hukuhuku jamvini au?
 
Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details

Mi sina uhakika kama hela yangu wataipokea kutokana na kazi ninayoifanya, ndo mana sijachangia.
 
Hongera sana, huyo shemeji umempata humuhumu? id yake please....!
 
ukitaka mtoto pia weka tangazo
 
Kumbe? Aisee na mimi nitaanzisha thread baada ya mfungo mtukufu.
 
Wale uliowachuja........................ nawakaribisha kwangu!
 
Hongera bwana mkubwa..
Usisahau kuja MMU tena kama shemeji ataleta rabsha..
 
Hongera sana hebu tupe maujanja hivi nae yumo humuhumu JF au alisoma tu na mkawasiliana, Ok hayo yote NI MAPENZI MEMA
 
dah hivi kumbe inawezekana aisee mbona watu wengine wakija na hizi topic watu huwaponda sana mara utapata magumegume mara ooh walioshindikana duh hongera sana ndugu yangu ila usifanye haraka hivyo ndoa zoeaneni kwanza please kama miaka miwili hivi maana huwezi jua watu hubadilika jamani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…