Naishukuru sana serikali kupiga marufuku tabia hii mbaya ya wakuu wa shule

Naishukuru sana serikali kupiga marufuku tabia hii mbaya ya wakuu wa shule

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Wiki iliyopita niliandika uzi hapa kuhusu tabaia ya walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi eti kwa sababu hawajamaliza kulipa michango ya shule. watu wengi hawakuunga mkono hoja yangu, wakitumia kisingizio kuwa serikali imezitelekeza shule hizi za kata ,wengine wakasema walimu ni watekelezaji tu maagizo hutoka juu.
Nilichowaambia wadau ni kwamba siyo kwamba sijui udhaifu wa serikali ya ccm katika kuzihudumia shule hizi,ninafahamu na siyo tu serikali kuu hata malmashauri zetu pamoja na bodi za shule nazifahamu kwa sababu nimekuwa kwenye shule hizi kwa mda mrefu.Ukija huku shuleni kuna madudu mengi sana yanafanyika kuna michago mingi sana imeanzishwa ,swali ni je yote haya ni maagizo ya serikali. Kwa mf ni lini serikali iliwagiza walimu wawatoze pesa wanafunzi wa kidato cha pili wanapotaka kujua matokeo yao ya mtihani wa taifa kwenda kidato cha tatu.Niambieni ni wakati gani serikali iliwaagiza walimu wauze limu ,majembe,pamoja na ndoo zinazochangwa na wanafunzi? .Ni waakati gani serikali hii pamoja na mapungufu yake iliwaambia walimu wawafukuze wanafunzi wanapochelewa kulipa michango ya shule?.Tujiulize swali hili mwanafunzi ana kosa gani, wengi wao hawa ni watoto wadogo wasioweza kujitafutia kipato chao wenyewe.Kwanini isitafutwe njia nyingine ya kuwabana wazazi walipe michango hiyo wakati wanafunzi wakiendelea na masomo?.

Miezi michache iliyopita rais kikwete alikuwa ziarani mkoani Geita akijionea mwenyewe jinsi elimu ilivyopolomoka katika mkoa huo ,akapiga marufuku wanafunzi kurudishwa nyumbani kisa hawajakamilisha michango ya shule. Jana mkuu wa wilaya ya mbogwe mkoa huo wa geita ameendelea kusisitiza agizo hilo la rais. Mimi nasubili nione ni nani mwingine ataendelea kupingana na agizo hili la wakuu wa inchi.Tatizo kubwa ninaloliona katika inchi yetu ni watu kufanya mambo watakavyo wenyewe. kila mtu ni mungu mtu kwenye sehemu yake .Wapo watendaji ambao hawataki kabisa kutii maagizo ya viongozi wao wakiwemo baadhi ya walimu. Mwisho naomba kuwakumbusha walimu kuwa tusisahau tulikotoka hata sisi tulisoma kwa umaskini mkubwa .
 
tutawarudisha nyumbani waende wakafate wazazi wao... Elimu ni kwa faida Yao na wazazi wao afu unataka mwalmu nianze kuwaza napataje chalk..... na sasa ni undava undava mtaelewa tu si mnaingiza Siasa kwenye Elimu na Sisi tunafanya kazi kisiasa
 
Back
Top Bottom