Naishukuru sana serikali kupiga marufuku tabia hii mbaya ya wakuu wa shule

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Wiki iliyopita niliandika uzi hapa kuhusu tabaia ya walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi eti kwa sababu hawajamaliza kulipa michango ya shule. watu wengi hawakuunga mkono hoja yangu, wakitumia kisingizio kuwa serikali imezitelekeza shule hizi za kata ,wengine wakasema walimu ni watekelezaji tu maagizo hutoka juu.
Nilichowaambia wadau ni kwamba siyo kwamba sijui udhaifu wa serikali ya ccm katika kuzihudumia shule hizi,ninafahamu na siyo tu serikali kuu hata malmashauri zetu pamoja na bodi za shule nazifahamu kwa sababu nimekuwa kwenye shule hizi kwa mda mrefu.Ukija huku shuleni kuna madudu mengi sana yanafanyika kuna michago mingi sana imeanzishwa ,swali ni je yote haya ni maagizo ya serikali. Kwa mf ni lini serikali iliwagiza walimu wawatoze pesa wanafunzi wa kidato cha pili wanapotaka kujua matokeo yao ya mtihani wa taifa kwenda kidato cha tatu.Niambieni ni wakati gani serikali iliwaagiza walimu wauze limu ,majembe,pamoja na ndoo zinazochangwa na wanafunzi? .Ni waakati gani serikali hii pamoja na mapungufu yake iliwaambia walimu wawafukuze wanafunzi wanapochelewa kulipa michango ya shule?.Tujiulize swali hili mwanafunzi ana kosa gani, wengi wao hawa ni watoto wadogo wasioweza kujitafutia kipato chao wenyewe.Kwanini isitafutwe njia nyingine ya kuwabana wazazi walipe michango hiyo wakati wanafunzi wakiendelea na masomo?.

Miezi michache iliyopita rais kikwete alikuwa ziarani mkoani Geita akijionea mwenyewe jinsi elimu ilivyopolomoka katika mkoa huo ,akapiga marufuku wanafunzi kurudishwa nyumbani kisa hawajakamilisha michango ya shule. Jana mkuu wa wilaya ya mbogwe mkoa huo wa geita ameendelea kusisitiza agizo hilo la rais. Mimi nasubili nione ni nani mwingine ataendelea kupingana na agizo hili la wakuu wa inchi.Tatizo kubwa ninaloliona katika inchi yetu ni watu kufanya mambo watakavyo wenyewe. kila mtu ni mungu mtu kwenye sehemu yake .Wapo watendaji ambao hawataki kabisa kutii maagizo ya viongozi wao wakiwemo baadhi ya walimu. Mwisho naomba kuwakumbusha walimu kuwa tusisahau tulikotoka hata sisi tulisoma kwa umaskini mkubwa .
 
Reactions: kbm
Tatizo la kudharau maagizo ya selikali limekua sugu katika secter zote

Na watendaji wanaona et kila jambo c halisia bali ni siasa

Tujaribuni kuwajibika ipasavyo kwa maendeleo ya taifa letu

Walimu na wazazi tekelezeni wajibu wenu
 
Ada ya sh. 20,000/= inakutoa povu kama umemeza omo!! Ungejua shida wanazo pata wakuu wa shule kufuatia ukosefu wa fedha za kuendeshea shule unge jutia kwanini umeamua kuandika upuuzi huu ambao ni mwendelezo wa hujuma za kuidhoofisha secta ya Elimu IF YOU THINK EDUCATION IS EXPENSIVE TRY IGNORANCE
 
Wajinga ndo waliwao.

wewe usichangie..mtoto wako ndiye atakaa kwenye sakafu ndiye atashinda njaa shuleni..ndiye atajisaidia kichakani.n.k.


mnadanganywa..na mtu ambaye anachangia kila kitu atakachoambiwa achangie kwenye shule anayosoma mtoto wake.

ulishafikiria tangu serikali kupunguza ada hadi 20000/= na kuahidi kulipa 20000/= kwa kila mwanafunzi ni kweli wanatekeleza hilo na je ni kwa kiwango gani?


mpeleke mtoto shule then subiri serikali itakuja kujenga choo,kununua madawati, kujenga madarasa,kuleta waalimu, kununua vitabu, Chaki, kumwajiri mlinzi, n.k.
 
ndugu qualifier ,napenda kusema kuwa yote uliyoyataja yana ukweli fulani ndani yake, lakini je unadhani tiba ya matatizo hayo ni kuwafukuza wanafunzi wasisome.Hebu tulia ufikiri vizuri.
 
Mimi pia sikubaliani na hi tabia ya kuwafukuza wanafunzi kwa sababu sio wanafunzi wote, wasiokuwa na uwezo wa kulipa ada. Ktk darasa la watoto 40 ni 5 au 6 tu ndio wanakuwa hawana uwezo ina maana hakuna madhara yoyote yanayopatikana kama hawajalipa. Ni roho mbaya tu.
 
Wewe endelea kushukuru hivyohivyo na wakuu wa shule nao watashukuru kwa kulipwa mishahara yao bila kutimiza wajibu wao, halafu mwisho wa miaka 4 ya shule mwanao atashukuru kumaliza masomo akiwa na cheti cha divisheni 5. Wewe hujui kabisa hali ya uendeshaji wa hizo shule, ACHA SIASA KTK ELIMU ndugu yangu, Taifa linamegeka hili na kuleta matabaka kupitia Elimu. Hivi ni shule gani ya kata anasoma mtoto wa mbunge, waziri, au hata mkuu wa wilaya,? Nitajie japo shule tano wilayani kwako, TAFAKARI
 
"Double Beating" a poem by Richard Mabala
" ...when the hammer pounds the nail /and nail bites mercilessly into the wood,/who is the wood to blame?..."
 
(Tujiulize swali hili
mwanafunzi ana kosa gani,
wengi wao hawa ni watoto
wadogo wasioweza
kujitafutia kipato chao
wenyewe.Kwanini
isitafutwe njia nyingine ya
kuwabana wazazi walipe
michango hiyo wakati
wanafunzi wakiendelea na
masomo?.) mtoa mada ktk sehemu niliyoweka ktk mabano kwanini wewe usipendekeze hiyo njia mkuu hawajaona hiyo njia lengo la kufukuza ni kumjulisha mzazi mwenye uchungu na mwanae kumlipia ada acha kulalamika lipa ada elimu inagharamiwa hata shule za kata km ukishindwa basi kaongee na mkuu wa shule atakusikiliza sio kumwacha aende bila ada
 
Huyu mleta mada ni mtu mzima na ana akili ila anashindwa kudadavua mambo labla kwa faida yako na wengine ni kwamba serikali inakataa kuwafukuza wanafunzi kwa ajili hawana michango ya shule ila ILA IMERUHUSU NA INASISITIZA KUWATUMA WANAFUNZI KWENDA KUFUATA MICHANGO,hivyo ukiona watoto wamerudishwa nyumban ujue ni agizo la serikal la kuwatuma na si kufukuza kuwa mwuelewa na inaonekana umetoka kwenye idara hii siku nyingi
 
Mleta uzi.ungekua mkuu wa shule,usingeandika kama ulivyoandika.hujui lolote bora ukae kimya tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…