Naishukuru Serikali kwa chanjo ya Corona

Naishukuru Serikali kwa chanjo ya Corona

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Hii ndiyo kazi kweli ya Serikali na nitoe pongezi sana kwa Rais Samia kwa kujali Watanzania kwanza.

Wazee wangu na ndugu zangu wamepata chanjo ya covid 19.

Nashukuru imetutoa wasiwasi hasa kwa wazazi wetu ambao wapo 70’s.

Najua kuna mengi tunalaumu Serikali lakini tunashukuru sasa sana kwa kuokoa maisha na kutuondolea woga.
 
Huku kwetu ambao hatujafikisha miaka 50 tunakataliwa kuchanjwa.Kama Kuna watu hawataki kuchanjwa wengine tupo tayari ila ndio hivyo tunakataliwa
 
Hii ndiyo kazi kweli ya serikali na nitoe pongezi sana kwa Rais Samia kwa kujali Watanzania kwanza.

wazee wangu na ndugu zangu wmepata chanjo ya covid 19. Nashukuru imetutoa wasiwasi hasa kwa wazazi wetu ambao wapo 70’s . Najua kuna mengi tuna laumu serikali lakini tunashukuru sasa sana kwa kuokoa maisha na kutuondolea woga.
Unasemaje kuhusu Magufuli na Jafo mzee wa nyungu?
 
Pamoja na hiyo faraja na shukrani lazima ufahamu kwamba uwezekano wa wewe kupata corona ama kufariki kwa corona bado uko pale pale hata kama umepata chanjo. Hilo lisiondoke kichwani mwako.

Pili, ujiandae kwa chanjo ya 2 inayoitwa booster vaccine kwa ajili ya kuipa hiyo chanjo yako ya sasa nguvu, maana muda wake wa kupambana na variant ya delta sio muda mrefu.

Mwisho, hongera kwa chanjo, endelea kuchukua tahadhari.
 
Jansen Ni single doze
 
Back
Top Bottom