Naisi kuna mwanamke Anaishi nae

Naisi kuna mwanamke Anaishi nae

Mimi.

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
2,120
Reaction score
3,059
wapendwa!

Naitaji ushauli wenu boy friend wa rafiki yangu wa miaka mitano hajawahi kumpeleka kwake tangu waanze uhusiano wamekua wakikutana hotelini tu

Yeye anaishi Dodoma na rafiki yangu anaishi Moshi kwa muda wote huo wa miaka mitano

Kinachonifanya niisi anaishi na mtu akiombwa waende kwake uwa anamwmabia kua hatuwezi kwenda kwa sababu ya watoto wanaishi pale mpaka wakishaona ndio atampeleka kwake,hao watoto wawili alizaa na mwanamke mwingine alimuacha kwa sababu alimfumania huyo mwanamke akifanya mapenzi na mwanume mwingine nyumbani kwake

Akimwambia tuachane analia na hataki kabisa kusikia hilo swala

Afanyaje ili ajue ukweli? wanapendana sana na haipiti week bila ya yeye kusafiri kuja moshi kuja kumuona my friend na ameku ni msaada mkubwa sana wa maisha ya rafiki yangu (ki ushauli and financially) though hamtegemei sana kipesa maana yeye mwenyewe najiweza kipesa
 
unafahamu kwake? unataka kujua kama anaye ili iweje? nenda kwake bila taarifa[mshtukze]..utakalo likuta huko at your own risk....sometimes ni bora kutoujua ukweli utakao kuumiza..
 
Ujinga tu mtu kugawa K yake kabla ya ndoa hizo K mmepewa na mungu sio mziwache wazi kabla ya ndoa.

Eti tunakutana hotelini afu ananipenda na mimi nampenda ujinga mtupu, mwenye kukupenda anakuoa sio anakuchezea hotelini.
 
Miaka 5 du!
Peleleza kwake, nenda kama unashida naye, umetokea ofisini kwake halafu utajua kama ana mtu au la!

Au mwambie unaenda anyway halafu check reaction yake usoni.
 
Mmh miaka 5 hupajui kwake upo tu? We huitaji kuwa na familia yako dada!! suala la mustakabari wa maisha yenu ya kimapenzi mlishalizungumzia?
 
hivi kumbe hata kusoma alama za nyakati huwa ni ngumu eeeeee?? khaaaaa!
 
Hapo uliposema anakupenda sana,kidogo punguza ncha.Kwasababu,kama ingekua kweli,hao watoto angeweza hata kudanganya ni rafik yake wa kazini,au anything angalau ukapajue kwake,hata mkalala hotelin,au hata mda ambao watoto hawapo.Incase of anything,coz i believe ur all grown ups,besides you hav a 'us future'ahead of u,so no need to hide anything. Ata ivo hao watoto sindovizuri wakuzoee,au mkioana mtahama makazi muwaache watoto.
Pili,kuna mwenzio mmoja,alikuwa akikohoa,jamaa anatoka Mwanza anamfata Arusha hata kwa ndege,siku bibie alipoamua kufatilia,akamkuta mwenzie kajaa ndani tena mjamzito,na uzuri bibie alienda as a relative wakat jamaa yupo job,akapata ukweli woote..jamaa akadai eti, ni mke wa rafik yake,but mwisho wa siku ukwel ukajulikana na kila mtu life goes on!
Samahani kama nimekuwazisha,au cjaelewa ila muhimu uwetayari 4anything,na do not force,we mwanamke bana,mlainishe kwa kipaji ulichonacho..akuelekeze kwake akigoma,kuondoa doubt moyoni,mpandie uko uko,ila ujipange 4anythng.
Kwa upande mwingine,mhh labda anasababu zaidi ya iyo,nzuri kwa manufaa yako!em jitahidi muondoe vidoa moyoni,isijeathiri how u feel 4each other!
 
Duh pole sana dada yangu kwa mtazamo wangu mwambie ukwl unahitaji kwenda kujulikana kwa wazazi kuhusu swala la watoto utamua mwenyewe kuwalea usimwache mwenzako nakuomba.
 
He!
Hiki ni i kipaji....miaka mitano humjui kiasi hicho?
Yaani siku akiamua kukuzimia simu ndo imetoka sio....
 
Shosti mapenzi nikuaminiana sasa mpaka miaka mi5 bado kwake hukujui halafu eti excuse alimfumania mkewe nyumbani kwake,inamaana hana wazo la wewe kua ipo siku utakua mkewe?
 
Unadanganywa.....

Na umekubali kudanganyika......

Pole sana miakz mitano unacheza sindimba tu?

Usishangae kukuta mkewe hajamuacha........
 
mimi, kwanza naomba nikusute kidogo kisha nitakwambia cha kufanya, niliwah kuuliza hili swali hapa jamvini tena nakumbuka nilimention na kuquote post ya platozoom. hivi kweli mimi wewe ni mwanamke unayejipenda kweli? Hivi kweli ya Mungu juu ya upendo ipo? Kwanini kwenu mapenzi mpaka yatawaliwe na ngono tu? kwanini lakini kufanya haya mambo kabla ya wakati wake halafu mtu unakiri hadi hadharani? Hivi jamani hiki ni kizazi gani kisichoelewa maisha yanakwendaje? kwanini tunaharibu maana ya tendo la ndoa jamani?

narudia tena maneno yangu tendo la ndoa lipo kwa ajili ya kuendeleza uzazi na pleasure which comes out of it nature meant it to be a bait for men and women to accept parenthood obligations. sasa kwanini mnaiharibu maana hii? Yaani mmeifanya kuwa kama upumbavu na kitu cha kishenzi tena kisichokuwa na heshima lol? binafsi ningekuwa mim nisingethubutu kukiri hadharani kuzini na mtu miaka 5. wewe ni mwanamke unatupa picha ya kutumiwa tu tena mbaya zaid ya kukubali mwili wako kutumika pasi malengo.

hivi huyu kaka unajua anawaza nini nimeshapata liwazo langu na ndio maana akitaka liwazo he can just travel to moshi ama akakwambia uende Dom mkaishia kulala hotelini kisha ukarudi. yeye kwake ameshapata liwazo lake basi. anaish na nani kwanza kwako haikuhusu manake ungekuwa na akili wenzio hata kama watazini na wapenzi wao basi yawezekana ni mara chache sana labda hata 4 tu kisha ndoa inapita wewe miaka 5 halafu unasubiri ndoa? ingekuwa miaka hiyo kipapa hujatoa sawa, ila umekitoa with no focus for 5 yrs? sikuelewi tena naomba Mungu usiwe mdogo wangu manake ningekusema hadi ulie aisee.

hebu nenda jipange upya mambo ya kutoa uroda acha kabisa, tulia contain nyege zako. asipotangaza ndoa tulia fikiria alternative ila unakoendelea ni kupotea. nisamehe sana kama nimekuwa mkali sana kwako na yeyote atakayesoma nisameheni tu manake najijua mwenyewe kwangu mimi sindano ni dawa japo inauma jamani..............
 
Last edited by a moderator:
5 years, no formal commitment hata kabarua kwa wazee na unamegwa hotelini. Duuh huyo ni time waster, ungekuwa na mtu wa kuaminika kwa muda huo una watoto 2 na probably happily married na sio kuibana vichochoroni.

Tambaa taratibu aunt hakuna lako......wewe unapagawishwa na machozi hata Kanumba alikuwa analiaga akiwa kazini, simply huyo ni msanii.
 
Miaka mitano mingi eh?

yes mai hazbendi....
Miaka mitano ni mingi sana.....
Kuimbiwa nyimboza mapenzi tu....
Hujui anapoishi, hujui hata ndugu yake mmoja?
Kwa wapendanao wenye mapenzi ya dhati hii haiwezekani.....

Come on Asprin,
wewe mwanaume unajua....
Jinsi gani kigezo cha 'nampa talaka mke wangu'....
Au ' nimemuacha mke wangu'
au 'nitamtaliki mke wangu kwa ajili yako' inavyokuwa ni usanii mtupu....
Jinsi wanaume wanvyotumia maneno hayo ili kumlainisha mwanamke......
Ili mwanamke adhani kuwa atamilikwa yeye....

mimi shtukaaaa
hakuna kitu hapo...
Kuwa serious....kama anakuoenda atakupeleka...

Mpeleleze upajue kwake halafu uende wakati mwanaume hayupo.....
Ila hakikisha huna matatizo ya presha kabla ya kufanya hivyo....
 
Last edited by a moderator:
Ujinga tu mtu kugawa K yake kabla ya ndoa hizo K mmepewa na mungu sio mziwache wazi kabla ya ndoa.

Eti tunakutana hotelini afu ananipenda na mimi nampenda ujinga mtupu, mwenye kukupenda anakuoa sio anakuchezea hotelini.

sasa hapa ndo umeandika nini, watakatifu wenzio hawana kashfa hizi
 
Back
Top Bottom