NAITAJI KUWA mkulima Na nina MTAJI.ILA SIJAJUA PA KUANZIA.

NAITAJI KUWA mkulima Na nina MTAJI.ILA SIJAJUA PA KUANZIA.

Meek Mill

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
749
Reaction score
840
Kwanza nianze kwa kuwasalimu ndugu zangu.me kijana nimeitimu diploma.. Nimepata mtaji wa milioni 3 na naitaji kweli kuwa mkulima..ila sijajua niaze vp?wapi nitalima?kivipi nitavuna?wapi nitauza?na faida iko vipi...!!msaada nduguuuu.
 
Uko wapi na ungetaka kulima nini? Be specific.. Ngoja aje mkuu Kubota
 
Last edited by a moderator:
Nenda mkuranga kodisha eneo ulime matikiti maji huu ndio msimu wake mvua zimekwisha,mpm mkuu malila kwa maelezo zaidi.
 
Kwanza nianze kwa kuwasalimu ndugu zangu.me kijana nimeitimu diploma.. Nimepata mtaji wa milioni 3 na naitaji kweli kuwa mkulima..ila sijajua niaze vp?wapi nitalima?kivipi nitavuna?wapi nitauza?na faida iko vipi...!!msaada nduguuuu.

Uko wapi na ungetaka kulima nini? Be specific.. Ngoja aje mkuu Kubota

Kubota, Malila na Chasha inawahusu.

Mkuu Meek Mill, hongera sana kwa kuhitimu Diploma ambayo hujasema ni ya fani gani, mimi niachukulia siyo Diploma ya Kilimo! Ninakupa mawazo yangu hapa nikitarajia na nikizingatia kuwa shughuri hii utaifanya na kuisimamia wewe mwenyewe.

Ili unielewe vema ushauri wangu mimi nimejiuliza yafuatayo:
Baada ya kuwa umepata mtaji kwa nini akili imekutuma ufanye mradi wa kilimo? Kwa nini usifungue mradi wa kushona nguo, mradi wa kufungua zahanati, mradi wa kutengeneza computor, mradi wa kutengeneza radio na Televisheni? Kwa nini hukufikiria miradi kama hiii??

Ninahisi hukuwazia kufanya miradi hiyo mingine bali kilimo kutokana na fikra za wengi kuwa kilimo kila mmoja anaweza kufanya na akafanikisha ili mradi tu una mtaji! Kilimo ni fani ambayo inahitaji utaalamu, kilimo ni sayansi na ni biashara, na unaweza kufanya ukulima kwa uhakika sana iwapo utautafuta utaalamu kwanza. Kutumia njia ya trial and error unaweza kufanikiwa pia lakini hakuna haja upoteze nguvu na muda mwingi kwa mambo ambayo binadamu wengine walishayafanya na kufanikiwa, kwa nini na wewe uingie kwenye utafiti? Ingia kwenye kilimo cha kibiashara kwa nguvu huku ukijua nini unaenda kukifanya kama vile mtu anavyoingia kwenye biashara ya kushona nguo, zahanati, kutengeneza computor, tv n.k.

Kuifanya hadithi fupi sisemi uende chuo cha kilimo, la hasha siyo lazima, bali chukua hatua zifuatazo:
1)Popote utakapotaka kufanyia uzalishaji nenda ukazunguke bila kuchoka ukikagua na kutambua mazao mbali mbali yanayostawi vema eneo hilo, itambue misimu ya uzalishaji na changamoto mbali mbali.
2)Ulizia wakulima mbali mbali wa mazao uliyoona yakistawi juu ya changamoto mbali mbali za uzalishaji wa mazao uliyoona yakistawi sana ikiwamo na soko lake.
3)Funga safari nenda kwenye soko tarajiwa au wafanyabiashara wanaofahamika wa mazao husika ili uweze kutambua bei na jinsi zinavyobadilika ndani ya mwaka hii itakufanya utambue ni zao gani linalipa zaidi.
4)Chagua mazao yasiyozidi matatu endelea kuchunguza hadi ubaki na zao utakalovutiwa nalo zaidi liwe zao moja au zaidi!
5)Tafuta na uwatambue wakulima kadhaa mashuhuri waliofanikiwa kwa kulima zao ulilochangua kulilima, kisha poteza msimu mmoja kwenda kufanya kazi kwao kwa kujitolea, au kwa kulipwa, au wewe uwalipe ili mradi tu upate fursa ya kushuhudia na kujifunza kwa vitendo jinsi ya kuzalisha zao hilo na hatimae utajua wapi wanakouza zao hilo. Utapata taarifa hizi kutoka kwenye chungu cha kupikia kwa uhakika!! Uwe tayari hapa kupoteza msimu mmoja kwa ajili ya kujifunza tu!
6)Kama itakuwa vigumu kutumia njia hiyo juu (namba 5) fanya juu chini ulime maeneo karibu na wanakolima hao wajuaji, kamata mmoja wa hao wajuaji na fanya urafiki nae na tumia akili yako ya kuzaliwa umfanye awe Mentor (mshauri) mwangalizi wako, akushike mkono kukuongoza kwenye safari hiyo inayopita kwenye changamoto mbalimbali hadi akupeleke sokoni anakouzia mazao yake!!

Kilimo si kitu kila mtu anaweza kufanya na akafanikiwa, lakini kila mtu akijifunza anaweza kufanya na akafanikiwa, yapaswa kujifunza ili kupunguza changamoto zinazoweza kukukatisha tamaa mapema!! Wekeza kwanza kwenye kujiboresha kimaarifa zaidi kuliko kukimbilia kutifua udongo!!! Hiyo pesa iweke benki kwanza au izalishe kwa njia salama. Utakapojiridhisha kiutaalamu kata nusu ya mtaji wako anzisha kidogo kabla hujakanyaga full throttle!! Tuko pamoja Mkuu!!
 
Kwanza nianze kwa kuwasalimu ndugu zangu.me kijana nimeitimu diploma.. Nimepata mtaji wa milioni 3 na naitaji kweli kuwa mkulima..ila sijajua niaze vp?wapi nitalima?kivipi nitavuna?wapi nitauza?na faida iko vipi...!!msaada nduguuuu.

Kwanza ni kwa nini umesema unatamani kuwa mkulima na si bishara zingine? Jei ni kweli kwamba unataman kuwa mkulima ila hujui utalima? Hujui utavuna vipi? hujui utauza wapi? nahujui faida,

Ni bora kwanza ukaeleza watu Driving Force ya wewe kutaka kulima wakati unasema hujui hata wanavua vipi na wana lima vipi,
-Je huko Dodoma hakuna Mashamba ya kujifunza kulima au kuvuna?
-Je wewe umealiwa mjini make hata mjini kuna mashamba,

Mkuu unatakiwa kuwa siriazi make ukiongea haya sehemu nyingine watu watakushangaa sana, so ni bora ukajipanga na kuumiza kichwa,

TATIZO LETU SISI HATUTAKI KUUMIZA VICHWA MKUU, MAFANIKIOA SI ISHU NDOGO SANA, UNATAKIWA KUHANGAISHA UBONGO WAKO SANA,

Cha mwisho wewe ndo unaye jua ulipo, wewe ndo unaye jua mahitaji ya eneo ulipo, wewe ndo unaye jua wanalima nini huko, so ni vigumu sana mkuu mimi niko Arusha ni kushauri kwamba lima mchicha wakati sijui chochote kuhusu Demand ya Mchicha huko, hata kama ningekuwa najua labda kupitia habari sijui curent demand, Sijui bei, sijui chochote kile so wewe ndo unaye takiwa kuhangaikia haya hapo ulipo na si watu walioko Dar, Tanga ndo wakuambie lima kitu fulani, ndo kupotana huko
 
thnx XANA brodah..!!Ngoja niazie hapo.
 
Back
Top Bottom