Naitamani "katiba dikteta" kiasi kwamba hata Amiri Jeshi Mkuu hawezi wala kuthubutu kuikanyaga

Naitamani "katiba dikteta" kiasi kwamba hata Amiri Jeshi Mkuu hawezi wala kuthubutu kuikanyaga

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Udikteta si mzuri. Lakini demokrasia inayotokana na katiba lege lege nayo ni hatari.

Kwa kawaida, dikteta hapingwi kirahisi nchini mwake. Ni ama watu wake wampende, hata kama ni kwa unafiki, au kumwogopa kwa ajili ya usalama wao. Madikteta hawakubali kudharauliwa.

Imeshatokea mara nyingi, hasa nchini kwetu, viongozi wa Serikali n.k. kuapa kuilinda katiba lakini wakaishia kuiweka mifukoni mwao.

Hiyo ni ishara kuwa katiba si "mbabe" vya kutosha kuweza kumnyoosha yeyote, bila kujali hadhi yake.

Natamani, nchi yetu ipate katiba dikteta kiasi kwamba hata Amiri Jeshi Mkuu hawezi wala hatadhubutu kuikanyaga.

Natamani, tuwe na katiba dikteta itakayoweka wazi mamlaka na mipaka ya kila mhimili kiasi kwamba kila mmoja atatimiza majukumu yake penda asipende.

Natamani, katiba dikteta itakayofinyanga vyombo vyote vya dola na kuvifanya kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma na weledi na si kwa mihemko ya wanasiasa.

Natamani, katiba korofi itakayoirejeshea mahakama heshima yake ya kufanya maamuzi bila ushawishi wa maagizo kutoka juu.

Natamani, katiba dikteta amabyo hata rais ataiheshimu kama si kuiogopa.

Halafu Sasa hiyo katiba dikteta, itamke wazi kuwa ni marufuku kwa viongozi wa Serikali na watumishi wa umma kutumia magari ya kifahari kabla ya nchi kutajirika. Kama kuna ulazima wa kutumia magari, zitumike IST.

Mav8 yatumiwe na Viongozi watatu tu: Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu.

Natamani, katiba dikteta itakayofanya usalama wa Taifa kusimamia maslahi ya nchi na siyo matakwa ya wanasiasa. Katiba dikteta iwezeshe usalama wa Taifa, ikibidi, kusema hapana kwa yeyote yule atakayeonekana kuhatarisha maslahi ya Taifa, hata kama ni Raisi.

Natamani, katiba dikteta itakayolazimisha raia na viongozi wao kutimiza wajibu wao hata kama hawapendi.

Nafikiri, katiba ya aina hiyo inaweza ikatuvusha. Katiba dikteta inaweza kuwa suluhisho la mambo mengi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom