Perpe
Member
- Jul 28, 2022
- 5
- 2
Kwanza kabisa, wengi wanaweza kutokubaliana na mimi kwamba bado Tanzania inayowainua walemavu kwa vitendo zaidi na sio kwa maneno na sera haijatenengenezwa, tunaishi kwenye nchi ambayo mengi huongewa kuliko kutimizwa haswa kwa upande wa kuwezesha walemavu.
Mlemavu ni mtu yoyote mwenye changamoto ambazo zinamfanya atofautiane na yule binadamu wa kawaida, iwe viungo, ngozi, uoni,usikivu na hata akili, japo jamii yetu inachukulia zaidi watu wenye ulemavu unaoonekana ndio walemavu na sio wengine, hivyo kupelekea makundi mengine ya ulemavu usioonekana kutengwa, kutopewa kipaumbele na kudharauliwa kwenye jamii
Kila siku ya leo tumekuwa tukisikia sera mbalimbali kuhusu kuwainua walemavu ili waweze kuishi kwenye jamii bila kujiona tofauti na watu wengine ikiwa na pia kupata huduma zote za kijamii kwa usawa bila ubaguzi, moja kati ya huduma ya kijamii inayopewa kipaumbele zaidi ni ELIMU, elimu kwa watoto wenye ulemavu ili waweze kutimiza ndoto zao bila kujali ulemavu wao.
Kwa jicho la juu tunaona ni jinsi gani serikali yetu ilivyofanikisha lengo lake la elimu kwa walemavu kwa kiasi kikubwa, ikiwemo kuanzisha shule za elimu maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, kuanzishwa kwa vitengo na idara maalumu za kusaidia wanafunzi wenye ulemavu ngazi za shule na hata vyuo na vyuo vikuu, hizo zote ni hatua za kupongezwa lakini mabadiliko yanahitajika zaidi kwani yanayoendelea kwenye taasisi hizo za elimu ni kinyume na sera ya kuwawezesha walemavu kutimiza ndoto zao.
Wapo wengi wanakatiza masomo yao kutokana na kutopewa nafasi, kukatishwa tamaa kunapopolekea kuathirika kwa saikolojia, mfano halisi ni kisa cha msichana mmoja( ambaye ni mimi), nilipata ulemavu wa kusikia nikiwa darasa la sita, japo ilileta ugumu masomoni kutokana na usikivu hafifu lakini sikukata tamaa nkaendelea kupambana hadi kufika kidato cha sita,wakati huo nilikuwa napambania ndoto yangu ya kuwa daktari
Nikafaulu na kwenda chuo kuchukua shahada ya kwanza ya udaktari, lakin nilipofika mwaka wa tatu niliwekewa changamoto zilizopelekea kuachishwa kwa sababu ambayo ni huwezi kuwa daktari kama haupo mzima, iliniathiri kisaikolojia, na kwakuwa nilipambana sana kufika pale ukiangalia nilitoa taarifa ya tatizo langu tangu naanza na kuahidiwa kuwezeshwa na kusapotiwa nikikwama, nliiamini serikali na taasisi ile kwamba nitapewa nafasi nifikie ndoto yangu kwani uwezo nlikua nao lakini haikuwa vile.
Leo hii nimepoteza miaka mitatu ya maisha yangu, na mwaka mmoja niliotumia kupambana mpaka ngazi za juu za elimu kusudi nirudi kupambania ndoto yangu, huko nilizidi kuumizwa kwa kupewa ahadi feki, kutiwa moyo na kuachwa njiani, na wengine walidiriki kuniambia kwamba kwakuwa sina milango ya fahamu mizima yote mitano siwezi kuwa daktari, na hata nikimaliza sitoweza ajiriwa kutokana na ulemavu wangu.
Kauli kama hio kwa alieitoa ni rahisi kuzungumza bila kujua uzito wa maneno yaliyobeba na mpokeaji atajisikiaje, nlihisi kutengwa na jamii nzima kisa tu nina ulemavu ule, miaka mitatu ya maisha yangu, ndoto yangu vyote vimepotea vile, furaha yangu ilikomea pale, nlipatwa na sonona nkaanza mpaka kuhudhuria matibabu, nilifikia wakati nataka kujiua maana ni elimu na kusoma tu ndio nilichojua kufanya maisha yangu yote, niliiamini nchi yangu kuwa itaniwezesha itaninyanyua na kunipa moyo kwa juhudi zangu na kutaka kufika mbali.
Japo nliamua kuanza upya kabisa kitu kingine, ndoto yangu ilisimama hivyo, nipo nasoma kwa hofu, kama niliwahi kuambiwa maneno kama sitoweza kuajiriwa kutokana na ulemavu wangu, ni nini hiki nafanya? Nisije kuwa napoteza zaidi miaka yangu mengine, kilichotokea kimeacha doa kubwa maishani mwangu, kimenifanya nashindwa kwenda hospitali maana kunanifanya nikumbuke ndoto yangu ilioshindikana kwa sababu tu ni mlemavu, kimenifanya nipoteze kujiamini na kupunguza morali ya kusoma.
Rai yangu kwa serikali, taasisi zinasosimamia elimu nchini hasa elimu ya vyuo vikuu, na vyuo vikuu vyote nchini, kama mwanafunzi mwenye ulemavu fulani ama changamoto fulani hatakiwi kusoma kitu fulani ni bora aambiwe mapema, ni bora akataliwe wakati wa udahili, ni bora waweke sheria ama kanuni za kwamba mlemavu au mtu mwenye changamoto fulani hapaswi kusomea kitu fulani, kwa njia hio itapunguza maumivu tunayoyapata, itaokoa muda tunaopoteza kwani si ubinadamu kumpotezea mtu miaka mitatu ya maisha yake na kuja kumkataa katikati ya elimu yake na wakati uwezo wa kufanya hivyo tangu mwanzoni walikuwa nao.
Japo ni ngumu kufanya hivyo kutokana na sera za kuwezeshwa kwa walemavu zilizokuwepo, lakini hawawezeshwi kwa kiwango kinachostahili, wengi wanaangaliwa juu ya ulemavu wao na sio uwezo wao, kwamba mwenye ulemavu hawezi kuwa kama yule, zipo nchi zenye madaktari vipofu,viziwi na wasiosikia kabisa, zipo nchi zenye wanasheria wenye Autism na ulemavu mbalimbali sio kama hawawezi bali walipewa nafasi na msaada na kuwezeshwa ipasavyo.
Mabadiliko yanahitajika katika sekta ya elimu, walemavu nao ni watu, wawezeshwe,wainuliwe,wapewe nafasi wasionekane kwamba hawawezi kitu, wazungu wanasema "DISABILITY IS NOT INABILIT", huwezi jua ya kesho, huwezi jua kupitia wao ni nini kitanufaisha jamii na taifa kwa ujumla.
Naandika makala hii kuelezea hali halisi wengi wetu wanapitia, mimi ni mmoja ya walemavu waliopitia hali hii, bado naishi kwenye maumivu, na naumia zaidi nikiona wapo wengine wanapitia niliopitia mimi, naitamani Tanzania ambayo itakubali kwa moyo wote kuwa ulemavu sio kushindwa,bali wakiwezeshwa,wakipewa msaada wa kuonesha uwezo wao nao wanaweza, natamani pia mabadiliko yafanyike ili baadae wasitokee wahanga kama mimi, ili baadae kwenye Tanzania hio mpya niweze kuendeleza ndoto yangu iliokatizwa.

Upvote
0