The predicted
New Member
- May 28, 2024
- 1
- 1
NAITAMANI TANZANIA MPYA
Ni zaidi ya miaka 60 sasa tangu Tanzania ipate uhuru kutoka kwa mkoloni mwingereza. Hali zote za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na maisha ya kijamii zimebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Kuna mabadiliko mengi mpaka sasa ambayo serikali katika awamu tofauti tofauti zimekuwa zikijaribu kutengeneza mazingira wezeshi kwa wananchi wake waweze kuendesha maisha yao bila kikwazo. Kwa upande mwingine maendeleo hayo hayaendani na umri wa taifa hili tangu kupatikana kwa uhuru wake mnamo mwaka 1961.
Kama kijana na raia mwema naitamani Tanzania mpya katika nyanja zote za kimaisha kama ifuatavyo;
Naitamani Tanzania yenye mfumo bora wa Elimu ambao utampa kijana uhuru wa kuyatumia mazingira anayoishi kuwa ni fursa ya kiuchumi, kukuza ujuzi na kutatua changamoto zote katika mazingira yanayomzunguka. Kwanza kabisa, Elimu ya msingi natamani iishie darasa la nne na itumike kumpima mtoto uwezo wa kujua kusoma na kuandika pekee. Baada ya hapo watoto kulingana na wepesi wao wasambazwe katika maeneo ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatakuwa yameandaliwa na serikali wakishirikiana na sekta binafsi yakiaksi kipaji na maarifa ya mtoto husika ili wakakuze ujuzi na kumuongeza ubunifu. Kwa mfano, mtoto akipelekwa katika kituo cha mafunzo ya kutengeneza magari, madawa, utafiti wa mbegu za kilimo, uvuvi bora, TEHAMA n.k, Kwa miaka 6 atakua akiwa na ujuzi mkubwa na pia itamfanya awe mdadisi na mbunifu zaidi kwani eneo hilo atakuwa amebobea vya kutosha kwa kuwa atakuwa amelelewa katika mazingira ya kitaaluma husika.Hii itaondoa wahitimu wanaohitimu pasipo kuwa na ujuzi, ubunifu na wenye moyo wa kufanya makubwa kwa kutumia elimu zao.Hii pia itaaksi malengo ya Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamini katika elimu ujamaa na kujitegemea katika kutengeneza taifa lenye nguvu kiuchumi na kisiasa, kuzalisha wahitimu walio tayari kwa kazi sera ambayo aliianzisha miaka kadhaa tu tangu tupate uhuru.Elimu ya juu itatumika kuwaimarisha zaidi vijana hawa ambapo tutakuwa tayari na maprofesa waliobobea katika taaluma husika na kuondoa utegemezi wa nchi za nje yanapotokea majanga kama Covid-19 katika kutafta tiba na kinga za magonjwa hayo na majanga mengine
View attachment 3003284
Pichani ni mwalimu Julius Nyerere akiwa na vijana waliounga mkono azimio la Arusha
Naitamani Tanzania isiyo na changamoto ya chakula. Tanzania tumebarikiwa kuwa na maziwa, mito na bahari ambavyo ndicho kichocheo mhimu katika kilimo cha umwagiliaji. Kuifanya mikoa inayozungukwa na maziwa na mito kuwa mikoa inayotegemewa kwa chakula na hivyo kuwapa uhakika wananchi kulima nyakati zote pasipo kusubiria masika. Ikumbukwe kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hili hivyo hakipaswi kutegemea mvua tu kwani mara nyingi mabadiliko ya tabia ya nchi huathiri pia mifumo ya upatikanaji wa mvua. Kwa sasa mikoa ya Mwanza, Mara, na Kagera siyo mikoa inayotegemewa kwa chakula licha ya kuwa na ardhi yenye rutuba na kuzungukwa na ziwa Victoria.
Naitamani Tanzania yenye umoja wa kijamii, kidini,kiutamaduni na kisiasa. Tanzania yenye viongozi ambao wanawaona wapinzani wao kuwa ni wananchi wenzao, wenye haki ya kusema wanachoamini kuwa kina msaada kwa taifa na serikali ikawasikiliza na kuwaheshimu badala ya kuwachukulia kama maadui kumbe ni wananchi wenzetu wenye haki na nchi hii kama wengine. Ikumbukwe kuwa utawala bora humpa heshima mwananchi na humfanya aionee fahari nchi yake. Natamani upinzani wa kisiasa unaounga mkono mema na kukosoa mabaya huku tukizingatia kuwa sisi siyo wa mwisho kuishi nchini bali kuna watoto wadogo, walio tumboni na watakaozaliwa mbeleni hivyo kuwapenda wao kutatufanya tuwe waaminifu kwa taifa letu leo tukiamini kuna warithi wetu wanaostahili mema zaidi. Natamani wananchi wanaoiheshimu Tanzania kama wanavyozipenda nyumba zao. Wakijua kuwa nyumba hutunzwa kwani ikibomoka tutahangaika sote. Hivyo Tanzania ni nyumba yetu sote.
Naitamani Tanzania yenye fursa nyingi za kiuchumi. Tanzania ambayo ina miundombinu mizuri ya kujiajiri, mazingira wezeshi kwa wawekezaji, mafunzo rasmi ya ujasiriamali, na mikopo isiyo na riba kwa wanafunzi wote wanaohitimu chuo kikuu na diploma. Hii itapunguza idadi ya watu wanaoitegemea serikali katika suala la ajira. Hisia za ukosefu wa ajira ni lazima zituumize zaidi leo kwani kadri siku zinavyoongezeka ndivyo na idadi yetu inavyokua. Tujiulize kama leo tupo takribani watu milioni 60 ajira hakuna vipi baada ya miaka 10 ijayo? Serikali ni lazima iwajengee uwezo sekta binafsi kwani ndiyo sekta pekee inayoweza kutibu tatizo la ajira. Natamani kuona mtanzania asiyekwamishwa na ukosefu wa miundombinu na mazingira wezeshi ya kujiajiri ama kuajiriwa. Inawezekana iwapo tu kila mmoja atauchukia umaskini kwa vitendo
Mwisho japo si kwa umhimu, Naitamani Tanzania ambayo kila raia atafurahia huduma ya bure ambayo itamaanisha serikali inarejesha kwao wananchi mbali na kujenga huduma za kijamii kwa wananchi wake. Kutenga walau wiki moja kwa mwaka watanzania kupewa Huduma ya bure mfano umeme au maji ikiwa ni ishara ya kurejesha kwa umma na ikiwezekana iitwe "wiki ya serikali na wanchi wake". Hali hii itajenga uzalendo na kuwafanya wananchi waipende serikali yao na wafurahie kuwa watanzania. Japo ni kama inachekesha lakini wananchi wanastahili kustareheshwa na serikali yao kwa kuonyeshwa tendo la moja kwa moja la upendo. Kama watumishi wa serikali wao huwa wanapeana motisha kwa kazi nzuri pia haiondoi thamani itakapowapa motisha wananchi kwa zawadi ya kuwa watanzania na kwa kazi nzuri ya kulipa kodi. Na hii hakika ndiyo Tanzania ninayoitamani.
Kwaujumla Tanzania inahitaji mabadiliko mengi na ya kasi. Rai yangu kwa watunga sera za taifa ni kuwa, wajikite zaidi katika kuusoma ulimwengu unavyobadilika na hivyo kutunga sera zitakazomsaidia mwananchi kuendana na mabadiliko hasa ya ulimwengu wa leo wa "Akili mnemba" (Artificial intelligence)

Upvote
4