MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
NAITUPIA LAWAMA SIMBA "WEKUNDU WA MSIMBAZI" KWA KUMLIZA MESSI HADHARANI.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Hispania na Argentina vimedai kama Leonel Messi wa PSG angekubaliwa kujiunga na Simba SC "wekundu wa Msimbazi" hakika kile kilio chake tusingekiona. Lile chozi ni baada ya kukosa nafasi ya kujiunga na mabingwa wa nchi na wala sio huzuni za kuiacha Barca.
Watu wa karibu na Messi wamewatupia lawama Uongozi wa Simba zaidi kwa kulileta kinda Peter Banda Simba wakati hata Messi alikuwa anataka kumwaga wino Msimbazi. Banda ndiye aliyeziba nafasi ya Messi. Benchi la ufundi limetoa hoja ya kwamba tayari umri wa Messi ni mkubwa sana hivyo hawezi kuleta matokeo chanya pale msimbazi. Labda ajiunge na veterani wa Simba.
Mchangiaji mmoja aitwaye Thiago aliyejitambulisha kama rafiki wa Messi alimshushia lawama kali msanii Diamond kwa kutoa ma-song makali ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa bwana Messi kutaka kuja bongo ili awe anafaidi ma-live shows ya Dangote platinumz.