VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Hili jambo la 'uhaini' lililoanzishwa na IJP Wambura na kuafuatia kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Nyagali na Dr. Slaa linanitafakarisha sana.
Inaripotiwa humu na kwingineko kuwa akina Wakili Mwabukusi wamehojiwa kwa kosa la uhaini. Kosa la kutaka kuipindua Serikali au kumuua/kumdhuru Rais. Kosa la kutisha la jinai.
Uhaini unatisha. Unamtisha anayeshtakiwa; anayeshtaki; wafuatiliaji na kadhalika. Anayeshtakiwa akikutwa na hatia mahakamani, anahukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Chimbuko la jambo hili ni Mkataba tata wa Bandari kati ya Tanzania na Emirati ya Dubai inayowakilishwa na Kampuni ya DP World. Ni katika harakati za kutoa maoni na 'kupambana' kuuzuia mkataba huo popote pale. Wengi tumeukataa mchana kweupe kutokana na mapungufu yake.
Katika kuukosoa na kuuzuia, watanzania wenzetu hao wamejikuta matatani. Matatani kutokana na kauli zao na matendo yao (labda kwa kughazibika na kughafirika). Wamehojiwa kwa uhaini. Polisi na DPP wnaujua ukweli. Watatuanikia punde kupitia Mahakama.
Lakini, hili suala la uhaini (ambalo linagusa mamlaka na uhai wa Rais na Serikali) halitawatisha na kuwarudisha nyuma wawekezaji wakiwemo DP World? Yaani, ikiwa Serikali itaamua 'kuendelea' na mkataba wa DP World, hao DP World hawatatishwa na kutikiswa na uhaini huu unaotajwatajwa hapa Tanzania?
Busara huzuia hasira na hasara!
Mzee Tupatupa wa Lumumba ( kwasasa Masasi, Mtwara)