Naiuliza Serikali, huu 'uhaini' hautawatisha wawekezaji wakiwemo DP World?

Kwa Tanzania, uhaini na ugaidi inamaanisha kumpinga au kumkosoa Rais.

Itabidi sultani wetu Samia na watu wake waitangazie Dunia kuwa huku kwetu Tanzania ambako ubinadamu haujakamilika, hata maana ya maneno kama uhaini na ugaidi ni tofauti na wanavyorlelewa binadamu waliomaliza evolution. Hata maana ya Rais ni tofauti. Maana ya mahakama ni tofauti. Maana ya Bunge ni tofauti. Maana ya Polisi ni tofauti. Hayo maneno tunaiga tu kwa sababu tumesikia binadamu wakiyatamka.
 
Lakini kwanini raia tena kiongozi utishie kupindua serikali halili,? Katika usalama wanasema "never unders estimate any security threat:
Huna hoja fuatiria vyema yale mahojiano utaelewa
 
Kuna clip huko youtube inasema DPW kasingiziwa. Bandari zinapelekwa chini ya usimamizi wa Zanzibar, hivyo sidhani kama DPW wanasababu ya kutishwa😆😁
 
Huko duniani waache kuuliza mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wakuulize wewe?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna uhusiano kati ya suala la uwekezaji na kutenda uhalifu, km wao walitaka kutumia suala la bandari km uchochoro wa kutenda uhalifu basi wamegundulika. Wawekezaji ndio wataiamini serikali zaidi kwa umakini inaouonesha. Na kuwa Tanzania ni sehemu salama sana kuwekeza maana vyombo vya ulinzi na usalama viko makini sana, vinadeal hat na viashiria vya uvunjifu wa amani. Kwa kweli navipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa makini wao, Najisika fahari nchi yetu kuwa na vyombo imara km hivi. Hao wapumbavu washughulikiwe wakirudi wakiwa raia wema waheshimu na kutii sheria za nchi yetu.
 
Hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani tunaongozwa na akili ndogo. Madhara ya hizi kauli za reje reja za uhaini zitakimbiza hata hao tuonaoita wawekezaji maana wataona mitaji yao haiko salama.
we ndio una akili ndogo km K ya mjusi
 
we pumbavu kaa kimya km huna la maana la kuandika. Watu wameongea uchochezi live tunawasikia na kuwaona na macho yetu unakuja kuandika upupu wako huku? Wacha washughulikiwe wapumbavu wale.
 
Awamu iliyopita kesi zilikuwa ni ugaidi na uhujumu uchumi
Awamu hii kesi uhaini na uchochezi

Hawa watalii wanaokuja Tanzania hawajamsikia IGP
 
Congo kuna vita karibu asilimia 60 ya nchi ila bado kuna wawekezaji
Siyo kweli. Hayo unayoyaongea ni kwa kusikia au una uthibitisho? Sisi ambao tunaenda huko mara kwa mara, tunajua unachokiongea ni siyo kweli hata kidogo.

Ni eneo dogo sana la DRC lenye vita na machafuko, . Eneo kubwa la Congo hakuna vita. Tambua kuwa ukubwa wa DRC ni zaidi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda ukiziweka pamoja.

Eneo ambalo lina mapigano ya mara kwa mara ni Mashariki mwa DRC. Maeneo mengi yaliyobakia ni tulivu. Maeneo hayo yenye mapigano ya mara kwa mara, hakuna migodi ya makampuni makubwa.

Tambua kwamba DRC ina majimbo 26 kwa sasa. Zamani yalikuwa majimbo 11. Na katika hayo majimbo 11, mapigano ya mara kwa mara yalikuwa kwenye jimbo moja tu la Kivu. Migodi mingi mikubwa ipo jimbo la Katanga, na huko hakuna kabisa mapigano. Ukienda maeneo ya vijijini, jimbo la Katanga, wananchi wengi hawajui kabisa hata eneo ambalo kumewahi kuwa na na ebola au vita nchini mwao.
 
Dpw hawatishiki labda wengine, walishajiwekea kinga kwenye huo mkataba, kuwa ije mvua/jua wao hawataguswa
 
Mkuu mbona unakuwa na mawazo ya ajabu uhaini hauwezi kutisha wawekezaji bali wawekezaji wanatishwa na watu wazima kukataa makubaliano, kukataa utawala wa sheria na kuheshimu maamuzi ya mahakama na maandamano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…