Najigaragaza mavumbini kama shukrani kwa Rais wangu

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Leo nimeamua kujigaragaza mavumbini na baadae kwenye matope,mchanga,maporini kwasababu Rais wangu kipenzi anapiga mzigo wa viwango vya juu sana.

Nampongeza Rais wangu hali ya usalama wa Raia imeimarika sana,mambo ya kutekana kubambikiana kesi na ujinga ujinga umekwisha na kumalizika kabisa.Yule Mzee Kibao asitake sifa aliamua kujiua mwenyewe hana maana alitaka kuchafua taswira ya jeshi letu bora la polisi.

Nampongeza Rais amejenga madarasa,matundu ya choo,barabara kwa fedha zake binasfi ambao hawaoni ni majuha na wapumbavu vikodi vyenu vya kuunga unga si lolote si chochote Mama anaupiga nwingi ni lazima nigaregare mavumbini na ikibidi matopeni hakuna nanmna nani kama mama.

Nampongeza Rais kazuia maanamano yasiyo na maana kwani wapinzania wakifa kuna shida gani kwanini nani ambaye hatakufa?

Ngongo kwasasa London.
 
Tanzania hii hii utekaji umeisha, familia ya Soka, Mbise, familia ya Marehemu Ally Kibao. Ukiwa mwanachama wa ccm hasa mbele ya rais inaonekana common sense zao zinazima network.
 
Kuna nyakati nilimsoma sana Mahatma Gandi juu ya fikra zake kuhusu mambo mbalimbali ya kuikomboa jamii.

Nikamsoma sana Fidel Castro pia vile vile yeye alitazamia nini zaidi, nilikuja kugundua kuna muda busara na hekima ina nafasi yake na kuna nyakati hakuna namna inabidi nguvu pia itumike.

ILI KUIKOMBOA JAMII ila iwe kwa DHATI hasa.
 
Nampongeza Rais kazuia maanamano yasiyo na maana kwani wapinzania wakifa kuna shida gani kwanini nani ambaye hatakufa ?.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…