Najiuliza ni lini magonjwa mengine yaliacha kuua? Mbona kila kifo sasa ni Corona?

Najiuliza ni lini magonjwa mengine yaliacha kuua? Mbona kila kifo sasa ni Corona?

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
Najua tumepoteza wandugu wetu kadhaa kutokana na ugonjwa huu wa COVID-19. Mungu awarehemu marehemu na atupe faraja wafiwa.

Lakini najiuliza kwanini kila kifo kinachotokea sasa kinahusishwa na Coronavirus, hasahasa kikitokea kwa watu mashuhuri. Naamini watu wengi mashuhuri waliokufa kabla ya COVID-19 wangekuwa wamekufa kipindi hiki ingetajwa sababu ya kifo kuwa ni COVID-19.

Hivi ni lini saratani, kiharusi, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa nyemelezi na magonjwa mengine mengi sugu na yasiyo sugu yalisimama kusababisha kifo?

Kuna kitu hakiko sawa.
 
Ujinga ujinga ujinga ndio jambo pekee mungu aliliona ( maarifa)
 
Hayajaacha ila Corona kayaongezea speed. Kutana na corona wakati una hayo magonjwa, huchomoki tofauti na zamani.
 
Najua tumepoteza wandugu wetu kadhaa kutokana na ugonjwa huu wa COVID-19. Mungu awarehemu marehemu na atupe faraja wafiwa..
Upo sahihi kabisa pia matumizi ya ARV kwa muda mrefu husababisha complications za aina mbali mbali ikiwapo na vifo vya ghafla au mtu kufariki na afya yake nzuri tu
 
Kesi Yako Mleta Thread Inatakiwa Iwe Utakatishaji Fedha, Unajua Watanzania Siyo Wajinga!

Usijitoe Ufahamu, Muombe Mungu Yasikukute
 
Ndio kile ninachouliza kila mara wanapoleta Tanzia na kuhusisha na Corona, magonjwa mengine yalienda likizo lini?!
 
Upo sahihi kabisa pia matumizi ya ARV kwa muda mrefu husababisha complications za aina mbali mbali ikiwapo na vifo vya ghafla au mtu kufariki na afya yake nzuri tu
Lengo hapo ni nini hasa, tuwe na huruma jamani siasa hizi zitapita tujali maisha ya watu. Ukweli utatuweka huru hatutahangaika kama hivi.
 
Upo sahihi kabisa pia matumizi ya ARV kwa muda mrefu husababisha complications za aina mbali mbali ikiwapo na vifo vya ghafla au mtu kufariki na afya yake nzuri tu
Tuseme ukweli, ARV ni dawa za kifo, kutumia ARV ni suicide.
 
Najua tumepoteza wandugu wetu kadhaa kutokana na ugonjwa huu wa COVID-19. Mungu awarehemu marehemu na atupe faraja wafiwa...
Kwanza hakuna corona Tanzania ila PNEUMONIA, ukiweka sawa hii tuendelee na mjadala
 
Najua tumepoteza wandugu wetu kadhaa kutokana na ugonjwa huu wa COVID-19. Mungu awarehemu marehemu na atupe faraja wafiwa....
Mimi nadhani tungewekana sawa.

Tukubaliane kitu kimoja. Kwamba kuna Mungu, na Ndiye aliyeumba kila kitu.

Hivyo dunia ni mali yake, Shetani alifanya kuipora. Mungu aliachia jambo hilo, kwa sababu mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wake aliamua kumuunga mkono mporaji. Ajitawale.

Ni sawa na kumwachia mtoto wako duka kubwa la spare za magari hata elimu ya bookkeeping hana!

Unapoona duka linafilisika unaamua kulichukua mwenyewe.

Sasa jiulize, kama kwako ni hivyo, namna gani kwa yule aliyekuumba wewe?

Corona is one of the many symptoms that the Creator wants His Dunia black! It's Over!! Another Gharika is at the doorsteps!! It is not a jock friends!! It is there!!!! Very soon the bomb will explode!!!
 
Wewe endelea kumuomba mungu.kula limao zako tangawizi zako.
Hao wabishi waache
 
Back
Top Bottom