Najiulizaga swali hili

Najiulizaga swali hili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Kuna mambo yananishangazaga sana. Mpaka wakati mwingine najiuliza kwa NINI ipo hivyo.

Mimi ninatabia sijui niite ya ajabu au ya namna gani. Iko hivi;

Mimi sionagi shida mtu akiniita Mjinga, akiniona hamnazo, akiniita hata majina ya namna yoyote Ile. Kwangu sioni shida.
Yaani Maoni ya mtu mwingine au mitazamo ya mtu mwingine kunihusu Mimi sijajua kwa NINI hainiumizi.

Ila Mimi nikitoa maoni yangu kwa watu wengi. Yaani vile ninavyowaona au hata nikiwatania wengi huumia, huona kama ninawadharau, yaani ni kwamba wanajali.
Huwaga najiuliza kwa nini watu hujali na kuumizwa na maoni ya watu wengine.

Yaani mfano Mimi nikuone huna Akili Ati na wewe unaumia ILHALI unajijua unaakili. Hiyo inasababishwa na nini?

Mbona Mimi siumii?
Tabia yangu hiyo ilinifanya nisiwe na majina ya utani. Ila majina ninayojipa ndio yanashika na watu huyatumia.

Lakini pia ninakitu sijui ni karama, nikimtamkia mtu jina mtaani linashika na watu wanalitumia kumuita mtu kwa jina hilo. Hiyo inasababishwa na nini?

Karibuni wakulungwa
 
Tatizo la kuwa mjinga kila muerevu unamuona mjinga.

Athari ya ujinga ni mithili ya umauti. Maiti haihisi chochote, wanaoumia na kuombeleza ni wale walio hai.

Halkadhalika na ujinga nao, mjinga mwenyewe anajiona yupo sawa kabisa ila waliomzunguka ndio wanaoona upunguani wake.
 
Kwangu mimi ukiniona sina akili vita yangu ni kubwa mno kama kazi zimenibana siwezi kukutafuta naweza kukutumia nauli na posho ya kujikimu uje nilipo ili nikutie vitasa alafu nakukatia ticket ya kurudi ulipotoka ukiwa na ngeu

Kwamba hapo ndio utakuwa umejaribu kuonyesha au kuthibitisha jambo gani? Kwa sababu ipi hasa?
 
Kwangu mimi ukiniona sina akili vita yangu ni kubwa mno kama kazi zimenibana siwezi kukutafuta naweza kukutumia nauli na posho ya kujikimu uje nilipo ili nikutie vitasa alafu nakukatia ticket ya kurudi ulipotoka ukiwa na ngeu
Tatizo linakuja watazamaji watashindwa kutofautisha alie na akili na asie na akili kipindi unagawa dozi ya knuckles.
Ni kama kumkimbiza chizi aliekubia nguo zako ukiwa uchi wakati unaoga mtoni.

Ujinga wa kuwa na akili na kutokuwa na akili, kadri unavyojaribu ku kuconvince watu kuwa wewe una akili ndio unazidi kuonekana punguani😃😃
 
Sasa kwa nini wachukulie hiyo ishu personal.

Mfano, wazungu tukitoa maoni yetu juu yao hawaumii. Lakini wao wakitoa maoni yao juu yetu Waafrika wengi wanaumia. Hii inasababishwa na nini?
Hata wao wanaumia ni vile tu E.I yao ni kubwa.
 
Back
Top Bottom