article
Senior Member
- Sep 10, 2016
- 186
- 344
Nawasilimu wote!
Wana Jf nimepitia mijadala ,Maoni na uzi mbalimbali zinazohusu Katiba ya URT ya mwaka 1977 humu ndani na nimeguswa kusema kitu.
Nafahamu Katiba husika ina mapungufu mbalimbali lakini mapungufu husika hayaendani na uzito yanayopewa kwa maoni yangu.
Katiba hii ni miongoni mwa katiba bora zaidi ulimwenguni ukizingatia mafanikio ambayo nchi yetu imeyapata chini ya mwongozo wake pia kwa jinsi ambavyo Katiba husika imeandikwa kimaono na kwa utaalamu mkubwa na wa kipekee.
Naomba nitoe mfano mdogo kwenye upande wa uandishi wa katiba husika kimaono.Katiba hii imeweka katazo la kumshitaki Rais kwa lolote utakalolitenda kama Rais wa URT katika kipindi chote cha uongozi wake.Kwa wale wanaotaka haki bila ya kuongozwa na busara na maono watataka sehemu husika ifutwe ili kuwepo nafasi ya kumshitaki Rais.Siku ikifika ya kuondoa sehemu hii nawashauri wahusika warejee kiini cha Machafuko yanayoendelea kwa sasa nchini Afrika ya Kusini baada ya mashtaka dhidi Rais wa zamani wa nchi hiyo kwa matendo aliyoyafanya akiwa Rais wa nchi hiyo.
Mafanikio ni mengi ambayo nchi na watu wake wamepata chini ya katika ya mwaka 1977 na kubwa zaidi ni udumishaji wa Amani,Utulivu ,upendo na mshikamano miongoni mwetu pamoja na ushirikiano na nchi nyingine ulimwenguni bila ya kuhatarisha uhuru wa nchi yetu tokea mwaka 1977. Mambo haya tokea mwaka 1977 yameenda sambamba na ongezeko la watu,ukuaji wa uchumi ,udumishaji wa tamaduni za kitanzania na utokomezaji wa ubaguzi wa aina zote ikiwemo ubaguzi wa rangi,kabila,dini,elimu na jinsia(na hapa nitoe mfano?)
Mapungufu yapo kwenye Katiba hii kama zilivyo katiba nyingine kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni lakini hayafanani na mapungufu yaliyomo kwenye katiba hizo pia hayotoshi kusema kwamba katiba husika haifai na hivyo ibadirishwe.Mapungufu husika yanaweza kuondolewa kwa kufanyiwa marekebisho madogo pale inapobidi kwa maslai makubwa ya Taifa na si kwa kundi au kikundi cha Watu fulani kwa maslai yao binafsi.
Nahitimisha kwa kuwashurukuru na kuwapongeza wote wanaojivunia,wanaona na kuamini kwamba Katiba ya URT ya mwala 1977 siyo kikwazo cha Utamaduni, Demokrasia na Maendeleo ya Watanzania kwa sasa na siku za mbeleni.
Naomba kuwasilisha,
ARTICLE.