najua watu IMTU, MUHAS, KCMC wote na wengine mpo humu JF doctor, nisaidieni hili jambo wenzangu

The Only Kilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Posts
352
Reaction score
87
kila nikila asali najiskia tumbo linauma sana maanake sjajua kitaalamu itakuwa inasababishwa na nini? najua madoctor mpo wengi na hata kama sio doctor wee toa uzuefu wako kwa nini tumbo liume ukila asali ya nyuki wakubwa wanaudunga kinauma sio wale wadogo
 
Mkuu.@nicolson unaseme ukila Asali tumbo lako huwa linaumasana je hiyo ni kweli Asali

unayokula?isije kuwa ni Asali iliyochanganywa na Sukari Guru Asali Feki? kwa sababu mimi nijuavyo

Asali ni dawa ya maradhi ya tumbo iweje wewe unywe hiyo asali tumbo likuume tena

sana? Ajabu hiyo mkuu, Unajuwa kuiangalia na kuijuwa Asali orignal? hebu soma hapa chini.


TUNAFAHAMU kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki.

Maana sehemu nyingi hasa Kariakoo, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru.

Njia ya kwanza. Chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua, kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli.

Njia ya pili. Dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya pamoja ujue hiyo nii asali orginal.

Njia ya tatu. Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili, ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.

Bado kuna njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali nzuri.

Pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho.

Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki.






 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…