Najuta kulipandia........

next time kabla hujapanda gari,angalia cc zake.Usikute mafuta uliweka lita 1 ili hali gari ina cc4700,aina hiyo ya magari yanaendeshwa na wakubwa tu.Usilaumu gari bana,rudi kwenye bajaji ,mafuta uliweka kidogo hayo yana wenyewe.
 
Yaani balaa ile iliyonikuta kweli ningepata nguvu ya kukodisha lingine, mmh na hata kukodisha lingine sidhani kama ni good idea

hahahahhahahahah lol
daahh haya bwana nilidhani utaniruka
mmhh

haya pole
kwa nini usitafute lingine
au kodisha mmmhh

maana kila mahali hili unalijutia
 
Hili gari mafuta lilikuwa linavujisha lenyewe, haya bana nitapanda bajaji maans injini yake pis kiduuchu

next time kabla hujapanda gari,angalia cc zake.Usikute mafuta uliweka lita 1 ili hali gari ina cc4700,aina hiyo ya magari yanaendeshwa na wakubwa tu.Usilaumu gari bana,rudi kwenye bajaji ,mafuta uliweka kidogo hayo yana wenyewe.
 
Yaani balaa ile iliyonikuta kweli ningepata nguvu ya kukodisha lingine, mmh na hata kukodisha lingine sidhani kama ni good idea

embu nidokeze kidogo
akili imechoka sana leo
hapa tunaongelea toyota haswa
au ni reverse physiology..
 
Mashairi yamekua yananivutia siku zinavyozidi kwenda....mmmh
nikazane kujifunza...
 
Hahaha AD bana, hebu rudia tena kusoma......... Umeniacha hoi, reverse physiology

dahhh
itabidi nikaukumbatie
mto wangu kwanza mmhh
ni recharge hii battery halafu ntarudi.

Nisije kujibu majibu amaboyo hayajachujika
vizuri akilini..
 

i guess the car should be recalled as it seems to have manufacturer's defects!
 
Ukiweka nia utaweza, mimi nilikuwa napenda sana mashairi lkn sikuwahi kuandika shairi hata siku moja, like 3 weeks ago klorokwini alitoa shairi from me to u, and that was my turning point nilijaribu kuandika beti chache, magulumangu nae akaja kutoa shairi dear mama, nae pia nilijaribu kumjibu, suddenly nimejikuta so much in love na haya mashairi, everything has happened in a space of 3 weeks

Mashairi yamekua yananivutia siku zinavyozidi kwenda....mmmh
nikazane kujifunza...
 

Khaaaa! magari mabovu bana!

Pole kwa hili janga, dereva yakuonea
Hiki kweli ni kisanga, kilichokuelemea
Heri hukula mzinga, njiani na abiria
Gari lipige mnada , halifai nakwambia

Magari ya siku hizi, rangi yanametameta
Nje jina Mitsubishi, injini yake toyota
Mengine nayo ya wizi, Polisi wayatafuta
Gari lipige mnada, halifai nakwambia.

Gari ukilichagua, ni vyema uwe makini
Mengine yasuasua, mithili mkokoteni
Kuna yanayocheuwa, katikati safarini
Gari lipige mnada, halifai nakwambia.

Raha ya gari ujue, ni dhamana ya safari
Utakapo ikutue , hii ndio yake siri
Maji ndio yapungue, hii wala si dosari
Gari lipige mnada, halifai nakwambia

Gari bovu lasumbua, heri wende kwa miguu
Mimi fundi nayajua, ya manjano na buluu
Gamba bora ungevua, katafute brand nyuu
Gari lipige mnada, halifai nakwambia


Hongera sindano ya ganzi.....aiseee mistari yako imetulia sana............ keep it up!
 
Wow...Yakuonea naona umechukua fani nzima nzima!!
Zaidi ya hapo sichangii maana mimi sio mtaalamu wa magari!
 
you are the reason behind this, shairi lako 'from me to you' was my turning point, much respect


Vipi nipige mnada, kwa gari lisilo langu
Nilitaka tu kupanda, linifikishe mwenzangu
Kwa miguu sitakwenda, sitaki kizungu zungu
Gari hili sio langu, siwezi piga mnada

vipi ningelijulia, kama ni gari makini
Waweza nisaidia, mwenzio sikubaini
Mafuta livujishiwa, sikuiona injini
Gari hili sio langu, siwezi piga mnada

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…