Najuta kulipandia........

Kama gari si la kwako, vipi linakusumbua
Lirejeshe litokako , spea zako chukua
Gari hilo ni kituko, halifai kutumia
Tafuta lililo lako , ila hadhari chukua

Gari zima walijua , ufunguo ukitia
Mvumo huwa murua, gia laini kuingia
Resi ukikanyagia , moshi si wa kupalia
Oili kiangalia , ni nzito ilokozea.

Chungulia na mashine, uione gasketi
Zinavujisha nyengine , eneo lake la kati
Rejieta ni chengine, ujue halichemshi
Otaneta isiwe nene, ifiti na breketi

Ingia barabarani, lijaribu kwa safari
Anza spidi ya chini, kuiepuka hatari
Likanyage thamanini, ukiliona lishwari
Uzamie mvunguni , njiani likikuadhiri

Njiani likikuadhiri, uzamie mvunguni.
Kwanza urudi safari, ukatulie nyumbani
Ila ujue tayari , hilo gari si makini
Ni vyema ukaghairi, ukalitupa jaani
 
Ulosema ni sawia, ya gari kujipatia
Hapa nina ridhia, nipate kusafiria
Ila hebu fikiria, ni mengi yamefojiwa
Hakuna gari jipya, mengi yameshatumika

Watuambia jipya, japani lishatumika
utajapatwa na haya, injini yachuruzika
Sisemi yote mabaya, ila mengi patashika
Hakuna gari jipya, mengi yameshatumika

Ukiliwasha lawaka, washukuru umepata
Ila haufiki mwaka, gari laleta matata
sasa ya nini mashaka, mwisho wake ni kudata
Hakuna gari jipya, mengi yameshatumika

Mchina kaleta mambo, injini kuchakachua
Nimechunguza kitambo, zitazame utajua
zimepoteza na umbo, na nyingi zinacheua
Hakuna gari jipya, mengi yameshatumika


Mkuu kloro unanikimbiza kweli, but it is good b'se that is how i'm going to grow


 

Big up kaka! nimeamini hata ije mseto, metakefini au fansida, klorokwini iko palepale :dance:
 
Much respect kwa huyu mtu he is in his own class, lakini ukumbuke ana twin brother wake Asprin ambaye nae pia ni mtaalam mkubwa wa hii fani


Big up kaka! nimeamini hata ije mseto, metakefini au fansida, klorokwini iko palepale :dance:
 
Gari usiangalie bodi ijaribu injini kaka, ni ngumu kupata gari mpya kwanza mimi sipendi hizo.
 
Much respect kwa huyu mtu he is in his own class, lakini ukumbuke ana twin brother wake Asprin ambaye nae pia ni mtaalam mkubwa wa hii fani

Nawaona kaka mpo vizuri tulivimiss sana vitu hivi, asante kwa kutupa uhondo huu.
 
Much respect kwa huyu mtu, he is in his own class, lakini ana twin brother wake Asprin ambae nae pia ni mtaalam mkubwa wa hii fani, watch the space......


Big up kaka! nimeamini hata ije mseto, metakefini au fansida, klorokwini iko palepale :dance:
 
Kuna injini za kichina, unaangalia iko saaaaaafi, gari ipe miezi sita injini haifai, wachina wametuletea mambo


Gari usiangalie bodi ijaribu injini kaka, ni ngumu kupata gari mpya kwanza mimi sipendi hizo.
 
Kuna injini za kichina, unaangalia iko saaaaaafi, gari ipe miezi sita injini haifai, wachina wametuletea mambo

haya kaka nimekubali, Mimi nilikuwa naangalia muziki lakini wachina wametuwekea muziki mpaka kwenye bodaboda.. 'wabana pua kibao' usitafute spea usiku wafwa
 
Sasa hapo ndo utajua mchina ni balaaa muziki mpaka kwenye bodaboda, hata mimi ile gari niliyoshindwa kusafirika nayo nafikiri kulikuwa na mikono ya wachina, maana kwa jinsi ilivyokuwa inaonekana usingedhani kama mashine iko vile

haya kaka nimekubali, Mimi nilikuwa naangalia muziki lakini wachina wametuwekea muziki mpaka kwenye bodaboda.. 'wabana pua kibao' usitafute spea usiku wafwa
 

Kutumika sio hoja , haya ni yangu mawazo
Kama kwako lina tija, sahau hao wa mwanzo
Na kama la reja reja, sisumbue akilizo
Jipya ukilingoja, labda la maigizo.

Hata kama metumika, muhimu lisiwe bovu
Kama safari wafika , pamoja na uchakavu
Ni vyema ukaridhika, dharura litakusevu
Dunia meharibika , mbovu zinaitwa mbivu

Hadaa ni nyingi sana, kwenye haya magari
Weka begani spana , kukagua kwa hadhari
Utaibiwa mchana , watu walivyo hodari
Toyota ya Dyna , eti nayo yaitwa Lori

Kama ni lgari la chama, wala halinisumbui
Njiani likisimama , boneti silifungui
Kama ni la kuazima, taukwepa uadui
Talirejesha salama, ila tena sichukui
 

mkuu haha hahaha,lete lako kwangu gari,
mimi ndio kima raha,kwangu si kitu magari,
kama li jipya na daha,nitakupa hadi mwari,
hilo gari li mkweche,kamwe usipande tena,

bado naweza mkuu...
 
Hahaha mkuu kloro nachapa usingizi nitarudi kesho tuendeleze hii mada

 
Nina wasiwasi na derevea...

Dereva e ndugu yangu, eleza ulikosoma,
Elmu yatoa ukungu,sharti uishike vema,
Ni kama wa ndizi mkungu, hakika utasimama,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Vyuo vya uchochoroni, na NIT hapo ubungo,
Vingine vya redioni, havichemshi ubongo,
Hawapo barabarani, kuonesha kwa vitendo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Leseni kila aina, wewe yakwako ni ipi,
Ulipata kiaina, eleza lipata vipi,
Tupe ujumbe kwa kina, sije lipata ka pipi,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Kuna za makaratasi, leo zipo za kuswapu,
Karatasi ka patasi, lazima pige pushapu,
Najua hata wa Nkasi, lifika zama kishapu,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Alikuletea mjomba, jasho hata hukutoa,
Ukiendesha ka komba, kote kote unayumba,
Hata nyepesi ka pamba, wasiwasi nakushika,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Lengo kukuelimisha, haya mambo ni mafunzo,
Naona ulichemsha, mtaani meacha gumzo,
Jaribu kubadilisha, mbinu kuondoa mzozo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
 
Usirudie kupanda magari ovyo utanyonyeshwa kobe siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…