Najuta kulipandia........

I salute mzee
 
Wadai mkokoteni, jamvini watuambia
Nami nakupa yakini, KIA lilifanania
Naomba uniamini, mimi nililipandia
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Itakuwaje safari, ndani ya mkokoteni
Kwa hizo zake kikiri, safari hutotamani
Mimi si kama tumbiri, najua nini thamani
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Utaendaje arusha, wapanda mkokoteni
Safari itakuchusha, bila fika kileleni
Hapa nakuhabarisha, na wengine sikizeni
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Kwa vipi waishangaa, rangi ya kahawia
Mbona yametapakaa, mjini wayasifia
Si kama nakuhadaa, jaribu kufuatilia
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Iweje mkokoteni, una injini kwa mbele
Hili kwangu ni geni, wakijiji tueleze
Uache yenye utani, na hoja usiibeze
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Mengi yana mifumuko, ni sifa yenye misingi
Na kwa nyuma mibinuko, angalia 'mashangingi'
Mbona wafanya vituko, au ushakuwa dingi?
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni


Sindano mwana wa ganzi



 
Ati....!!!!,nini?? Mkokoteni..!!!!!????ha ha ha ha ha ha ha!

Nguli kaja jamvini, jipya katuambia
Eti ni mkokoteni, labda sikuujulia
Hili sikubaliani, ni gari nimemwambia
Ni mzee wa kijiji, mkokoteni kanena.............
 
JAMANI EEH,HILO SIO GARI.ETI LIMEBINUKA,DOH!HAKUNA GARI LENYE MA BEHIND MAKUBWA,HILO NI UPANDE WETU WA PILI TU.LOL:becky:
 
Angalia hizi gari nyingi za sasa ( new model -face lift) nyingi utaona kwa nyuma zimebinuka na utapenda kuziangalia hasa zinapoendeshwa.........hahaha, hapa tunazungumzia magari bana, twende sasa.......


Magari haya ya sasa, si kama ya enzi zile
Yameongezwa anasa, dereva ufurahie
Na tena yana hamasa, kwa ndani usisusie
Magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa

Yale yasio binuka, machoni yanachusha
Na huwezi kusisimka, kuendesha yanachosha
Hutoweza kuridhika, ijapo umeendesha
Magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa

Ukiyatizama kwa mbele, nako nyuma yavutia
Waweza fika kilele, safari kidhamiria
Hayana nyingi kelele, raha utajisikia
magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa


Na sindano mwana wa ganzi



JAMANI EEH,HILO SIO GARI.ETI LIMEBINUKA,DOH!HAKUNA GARI LENYE MA BEHIND MAKUBWA,HILO NI UPANDE WETU WA PILI TU.LOL:becky:
 
Hongera kwa mashairi mazuri,pole mwanakwetu mbona kuna gari mpya zipo zinauzwa hayo ya zamani sisi tumeyaacha
 
Ewe mkulima mwema, nashukuru ulosema
magari haya ya zama, ni sawa vile kilema
Jipya nitatazama, nataka lenye neema
Mwenyezi akijalia, jipya ntajitwalia


Na sindano mwana wa ganzi

Hongera kwa mashairi mazuri,pole mwanakwetu mbona kuna gari mpya zipo zinauzwa hayo ya zamani sisi tumeyaacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…