Najuta Kumsomesha

Najuta Kumsomesha

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
NAJUTA KUMSOMESHA

Najuta leo najuta
Majuto ni mjukuu
Mwenzenu yamenikuta
Nimeshavunjika guu
Wakubwa walinambia
Masikio nikaziba.

Hata ada nikalipa
Chuoni kumpeleka
Nikajiona kibopa
Kidume nimeshafika
Kumbe aniangalia
Atimize zake ndoto.

Leo chuo kahitimu
Hataki kunisikia
Kweli mi mwendawazimu
Tayari nimeumia
Mi mjanja wa mjini
Hadharani nimepigwa.

Bora bata ningekula
Kuliko nivyojinyima
Kweli mimi ni mbulula
Akilini si mzima
Kosa hili nilofanya
Daima nitajutia.

Nilijua akisoma
Maisha tutayajenga
Kidume nikajituma
Mihela kumtumia
Kumbe akiwa chuoni
Mwingine alimpata.

Leo kanitamkia
Mi siyo wa levo yake
Mrembo kanikimbia
Ameniacha mpweke
Najuta mimi najuta
Najuta kumsomesha.

Idd Ninga
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
NAJUTA KUMSOMESHA

Najuta leo najuta
Majuto ni mjukuu
Mwenzenu yamenikuta
Nimeshavunjika guu
Wakubwa walinambia
Masikio nikaziba.

Hata ada nikalipa
Chuoni kumpeleka
Nikajiona kibopa
Kidume nimeshafika
Kumbe aniangalia
Atimize zake ndoto.

Leo chuo kahitimu
Hataki kunisikia
Kweli mi mwendawazimu
Tayari nimeumia
Mi mjanja wa mjini
Hadharani nimepigwa.

Bora bata ningekula
Kuliko nivyojinyima
Kweli mimi ni mbulula
Akilini si mzima
Kosa hili nilofanya
Daima nitajutia.

Nilijua akisoma
Maisha tutayajenga
Kidume nikajituma
Mihela kumtumia
Kumbe akiwa chuoni
Mwingine alimpata.

Leo kanitamkia
Mi siyo wa levo yake
Mrembo kanikimbia
Ameniacha mpweke
Najuta mimi najuta
Najuta kumsomesha.

Idd Ninga
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Ndio maisha, endelea kuwawezesha, ipo siku utafanikiwa na Mwenyezi Mungu azidi kubariki kazi za mikono yako na kukurudishia mara dufu pale ulipotoa.
 
NAJUTA KUMSOMESHA
Usikate tamaa, maisha yanaendelea
Kila jambo lina sababu, jifunze kutokana na makosa
Majuto hayana faida, yaliyopita si ndwele
Fikiria yajayo, fanya mipango mipya
Mungu yupo, ana mpango mzuri kwako.
 
Ujumbe murua tena shatashata. Nakupa kongole malenga kwa ushahiri mseto usio na mawaa. Kwa wote wanaohusudu utwana wa kugharamia yasiyo hisani. Watambue bayana kigori hasomeshwi abadani.
 
Back
Top Bottom