Najuta kutembea na binti wa kirangi

Najuta kutembea na binti wa kirangi

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wakuu siandiki thread hii Kwa lengo la kukashifu au kutweza mtu au kabila la mtu.

Iko hivi
Miaka 10 au zaidi kidogo iliyopita nilijikuta kwenye huba zito na binti mmoja pale Arusha mjini.
Bint huyu alikuwa mzaliwa wa Arusha lakin wazazi wote wawili ni warangi.
Kwa sababu za hapa na pale mahusiano yetu yaliisha rasmi mwaka 2015 .

Ajabu ni kuwa bint huyu aliolewa miaka hiyo hiyo ya 2015 ila kila mara akipata changamoto basi mama yake anamwambia mwanaye kwamba ameenda Kwa mganga kaambiwa mwanae karogwa na Mimi.

Hii imekuwa kero kubwa Sana kwanga na suala hili linanifedhehesha Sana.

Je naweza kuchukua hatua gani kukomesha tabia hii?
 
Ndugu zangu waganga watu wabad sanaaa we wasikie hivi hivi anko wangu tunapoelekea ataambiwa dunia nzima inamroga yeye mana inasikitisha sanaaa
Unakuta mtu tatizo lake linaonekana kabisa linahitaji uchunguzi wa kina hospital Ila Kwa sababu ya ujinga anakazania vilingeni ambako anaishia kujazwa ujinga na kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom