Najuta kuuza kuku wangu ili kuomba kazi katika kampuni ya madini

Najuta kuuza kuku wangu ili kuomba kazi katika kampuni ya madini

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu,
Babu yangu ambaye ni kaka yake marehem bibi ni mwanajeshi mstaafu na mkurugenzi mtendaji ktk kampuni moja wapo ya uchimbaji madini huko Ushirombo mkoani Geita.

Nilipomaliza shule (CSEE)nilikaa home kama miaka miwili hivi nyumbani nikijishughulisha na kilimo cha kujikimu hapa nyumbani nilianza ufugaji wa kuku wa kienyeji hapa nyumbani.

Siku moja tulipata ugeni,na mgeni huyu ni babu yangu alikuja kutusalimia, si nikamwambia kuwa nataka kazi katika kampuni yao,babu akakubali,akaniambia inatakiwa niandae pesa kiasi cha sh.elf10 kwa ajili ya form ya maombi nikampa na form zikaja

ikabidi nijaze form hiyo,nikajaza yote, ila kwenye nida,ndipo kulinifanya niuze kuku wangu wote kwa ajiri y a kufuatilia nida bila mafanikio,ilifika mahali nilikuwa nikienda ofsi za nida wakinipga danadana naanza kulia hapohapo,mpaka mzee akaniambia nitume hiyo baru hivyo hivyo bila nida.

ikabidi nitume tu hiyo barua na akaniambia nisubiri majibu, nadhani kukosekana kwa nida ndio kunanifanya nisubr majibu mpaka leo inaendele
 
Endelea......... Nimesubiria majibu huku ufugaji wa kuku ukiwa umekufa,mpaka leo miaka mitatu imepita bila majibu jambo ambalo najuta sana ktk maisha yangu! Mwisho
 
Usilie wala usinung'unike! Wewe bado ni kijana hujachelewa maisha! Chukulia hayo kama chalenge ya kukufungua akili zaidi.
Anza na kuku wawili utatoka upya.
 
Usilie wala usinung'unike! Wewe bado ni kijana hujachelewa maisha! Chukulia hayo kama chalenge ya kukufungua akili zaidi.
Anza na kuku wawili utatoka upya.
sawa mkuu
 
Back
Top Bottom