Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana

Pole sana ndg. Kumwambia mkeo jambo kama hilo inataka moyo. Na hujui atareact namna gani. Hata hivyo, utauficha ukweli mpaka lini?? Na kama unavyosema, tayari dhamira inakusuta. Ushauri: tafuta mtu mzima unayemwamini, amweleze mkeo jambo hili na akuombee msamaha. Matokeo ya hatua hii, hayajulikani. Atakusamehe, ataamua kuachana nawe, atakusamehe lkn ataretaliate, atarevenge namna gani—haya yote hayajulikani. Tegemea huruma tu.

Kuna mzee namfahamu alizaa nje kama hivyo. Aliweza kuficha siri mpaka mtoto anamaliza form four. Ilibd mkewe akubaliane tu maana alikuwa ameshakuwa mtu mzima sana. So unaweza kuvuta kasi kidogo, mpaka mkeo atakapofika umri usio sumbufu. POLE SANA
 
kwanza, chukua muda kumwambia mkeo kutegemea na taratibu zenu, wengine hutumia wanafamilia kama wazazi au nduguze wengine wanasema wao wenyewe.

Hatua ya kuanza kutuma angalau pesa ni hatua, lakini inaweza hitajika kujihusisha zaidi. Hapa kama una ndugu zako huko anakoishi huyo dada wanaweza kwenda on ur behalf au kama unaweza kwenda mwenyewe na kuweka situation kwamba wewe ndio baba wa watoto, ila una familia yako kwa hiyo hapo utatinza wanao.

Huyo dada mweleze fika huoi ila anaweza endelea na maisha yake ila unawatambua watoto.

Itakupa uhuru wa kutembelea wanao unapokuwa na nafasi na wakiwa wakubwa watakuwa na uhuru wa kukutembelea.
 
Pole sana mkuu, u sound like u r a honest man, anyway the weird thing kuhusu secreats ni kwamba they always find a way out, na the way u sound kwamba u cant hide it anymore then ni sign kuwa siri yako inaweza isiwe siri tena, out of frastruation unaweza sahau hiyo line wife akaipata, unaweza ukafanya kitu kingine unconsiously kikamu-alert wife kwamba kuna somethng wrong. So my point is, ni vyema ukasema na wife mapema before its too late.
 
mkuu mleta mada kwanza pole sana pili hilo tatizo siyo kubwa kiasi hicho kama unavyo taka kulichukulia...naomba ufate ushauli wa the boss hapo juu..
 
Tatizo dogo hilo na majuto ni mjukuu mwambie tu mkeo hakuna jinsi kwani unaweza kukwepa leo ukapambana ukiwa na mzee kipindi hicho mtoto wako amechakachua nje ya ndoa sijui utafanyaje
 
Nimeipenda hapo kwenye bold. Mpaka mkewe awe mature enough siyo?

 
Duh! hi kali!..Anyways ngoja mi niseme yafuatayo:
1.Anza na upande wa watoto mapacha..Fanya unavyoweza ujue jinsi walivyojipanga huko ukweni kwa mapacha wako na ujue wanataka nini?..Unaweza kukuta wanataka umuoe binti yao cuz hawakujui..Jitahidi uwafahamu na ujue matarajio yao..Na usiishie hapo tu tafuta mtu wa makamo uongozane naye na uwaeleze kuhusu ndoa yako..naamini utaelewa upande wao.

2.Njoo kwa mkeo: Ukimaliza upande wa kule kwa mapacha wako..fanya vile vile umpate mtu mwenye busara zake mumweleze mkeo kuhusu hili jambo...vyovyote atakavyo'react' ndio ujue ujumbe umefika.

3.Mwishoni jaaribu kubalance mambo ya ukweni kwa mapacha na majibu ya mkeo..hii itakupa nafasi nzuri ya kuamua namna bora ya kuwatunza wanao na kuanzia hapo haitakuwa siri tena.

MY TAKE: Kwa kila hatua utakayoifikiria kuifanya kumbuka kuwa hakutakuwa na wepesi na ndio ubaya wa dhambi..Ila likishakuwa wazi angalau unaweza kuwa huru kwa kiasi fulani!
 
Mtihani mkubwa ila ni mwepesi ukiamua kujiweka huru kwa mkeo
Ni bora nusu shari kuliko shari kamili siku ukijisahau aifume simu yako au hiyo line halafu akumbane na hizo sms utaona rangi zote
Sio kwamba utamkasirisha bali utamfanya ahisi na ambayo hayapo
Kuwa jasiri na muombe Mungu sana akuongoze katika hekima ya kulisema hili na utafute namna nzuri ya busara ya kumuingia mkeo umwambie wazi
Ukweli utakuweka huru sana kuliko njia hii unayotumia sasa ya kujificha.
 
Mueleze mkeo kama anakupenda kwa dhati atakasirika lakini lazima akusamehe so mwambie ukweli
 
mkuu mleta mada kwanza pole sana pili hilo tatizo siyo kubwa kiasi hicho kama unavyo taka kulichukulia...naomba ufate ushauli wa the boss hapo juu..

Ni rahisi sana kutoa ushauri kama wewe hauhusiki...japo hukutueleza mkeo bt I guess mkeo na kind of women ambao wako loyal, honestly n loving!ni ngumu sana if u have got some-one like huyo kumueleza mambo ya kuzaa nje!
Ushauri wangu,usiharakishe sana kumwambia mkeo,nenda taratibu katika hili..sasa cha kufanya,maadamu una number ya bint,then mpigie umwambie ukweli wako kwamba una familia/umeoa na kuwa uko tayari kuwatunza watoto na nafasi/mazingira yakiruhusu utafika kwao kujitambulisha. After that tupa hiyo line ya simu na tumia wakala wa Mpesa/tigo/airtel kutuma hizo hela!kwa nin utupe line?
Tupa line ili uepukane na mazingira ya kuwa confused,meanwhile endelea kuangalia namna ya kumwambia mkeo!usifiche hili jambo bt nenda slowly!pole sana mkuu!
 

Pole sana bro, dhumuni la wazazi wa binti wa huyo binti wanataka wakukamate wakuozeshe kwa nguvu. Kwani ni imani iloyojengeka ktk jamii kwamba "BINTI ALIYEZALISHWA HAWEZI KUPATA MUME WA KUMUOA ISIPOKUWA YULE ALIYEMZALISHA". Na vilevile ni aibu kwao wazazi binti yao kuzalia nyumbani.


Kwasababu tayari uko kwenye ndoa na ni dhahiri kwamba huwezi kuoa tena labda kama we ni muislam ufunge ndoa ya pili, fanya utaratibu uwaeleze wazazi wako au wazee wowote wa hekima ambao utaenda nao kujitambulisha kwa wazazi wa binti, halafu utawaeleza wazazi wa binti kuwa huwezi kumuoa binti yao kwasababu uko kwenye ndoa ila uko tayari kuwatunza mama na watoto mpaka pale watoto watakapoweza kujitegemea ikiwemo kumtafutia nyumba atakayoishi huyo binti na watoto.

HALAFU JIANDAE KWA FAINI, HAWEZI KUKUBALI UMUARIBIE MTOTO WAO MAISHA YAKE HIVYO WANAWEZA WAKATAKA CHOCHOTE.

Halafu ktk suala la MKE WAKO WA NDOA, hapo huna ujanja maana ni lazima umwambie ukweli. Na hapo inategemea na reaction yake ikoje, ila kama alivyokushauri THE BOSS;

Ongea na mkeo taratiibu
nenda nae kwa step......

1. hatua ya kwanza mwambie kuwa ulitoka nje.....na uombe msamaha

2.hatua ya pili jifanye huna uhakika kuwa huyo binti alizaa watoto wako au la
unataka ku find out

3.hatua ya tatu....unamwambia intention yako ya 'kulea watoto kama ukithiitisha ni wako'
 
aisee walee wanao vizuri kwasababu haya uliyataka mwenywe
maana ngono zembe kuna ukimwi,mimba na mengine na ninaamini
ukimwi ungekupata ungejitibu sasa hujapata ukimwi umepata watoto
walee,mweleze mkeo ukweli japo najua mwanzoni \ipatachimbika bora hivyo
yataisha tu kuliko hao wazazi wa mtoto wa kike wakumbane na wewe siku moja
utakiona kilichomnyima kanga manyoya aisee
 
dah this mkasa of uaz umenitoa machoz for 2 reasons....
kwanza sikulelewa na na baba kwa sabab hakuwa a man enough kufanya hlo
Pili mwenzi wangu ana mtoto wa nje...................

back 2u
Inapunguza sana machungu mkeo akiujua ukweli kutoka kwako kuliko kuambiwa na mtu mwengine au kuja kugundua mwenyewe
Itamuua sana mkeo ila muda utaheal.......ingawa itakuhtaj ufanye kaz ya ziada kumfanya akuamin tena....

hao mapacha ni wanao, wana dam yako hawana hatia yoyote, wana haki kabisa ya kukufaham na kupata huduma zote kutoka kwako ikiwemo kufahamiana na wenzao(hao uliowazaa na mkeo) pamoja na ndg zako wengine
huyo uliyeza nae na familia yake wana haki ya kujua ukweli kuhusu ww............

Usiwafanye hao mapacha wakue waje wakuchukie the way I hate my dad.......

pole sana, Mungu akupe ujasir wa kukabiliana na hili kwa busara...................
 
Pole sana Mkuu. Utakuwa unamfahamu mkeo vizuri sana hivyo unajua fika ni jinsi gani atakavyoumia pindi ukimwambia habari hii ambayo inaweza kabisa kusambaratisha ndoa yako. Uko katika wakati mgumu sana lakini ndoa yako inastahili uipe kipaumbele, kama unaona inaweza kusambaratika basi minya kwanza kwa sasa huku ukiendelea kutafakari kwa kina ushauri wote uliopata hapa kabla ya kufanya maamuzi ya kipi cha kufanya. Pole sana.

 
Wakati unafanya uzinzi ulituomba ushauri nenda kamuombe mke wako atakusaidia kwa hili

nilijua tu watu wenye mitazamo hasi kama huyu watacoment tu, kabla sijamaliza kuwaza, comment ya kwanza ndo mulemule..........
sasa wewe Zipuwawa ndo umemsaidiaje na iyo comment yako.........?
 
Last edited by a moderator:
i love sukuma men, they stand for their kids no matter what.

Ndoa ya kusambaratishwa kwa sababu ya watoto jua haikuwepo toka mwanzo.

I love you and your comment pancrease.......lol,YEAH SUKUMA FOR LIFE......
 
i like how most of the comments kwenye hii thread are +ve as compared to ile ya aliyezaa na mke wa mtu na mtoto wa rafiki yake. wanaJF mkiamka vizuri mnakuwa +ve sana, thumbs up.
paulss umeona kosa, umekiri na unajaribu ku-correct it hongera 4 that. mwambie mkeo na hao wazazi, mwanzoni utakuwa mgumu kidogo but in the long run u'll make na mtaendelea kwa amani
 
Last edited by a moderator:
Funguka hapo tatizo lako ni kutokua mkweli na uoga....mficha maradhi kifo humuumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…