Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana

 
Last edited by a moderator:
Pole kwakua na wakati mgumu lakini kwa mwanamme sidhani kama hilo nitatizo lakukunyima usingizi,wewe umeoa hujaolewa
chakuogopa kitu gani kwa mkeo? au ulipo fanya mapenzi na huyo bint bila kinga ulitegemea nini? usiwe mwanamme suruali
kua mwanamme mwenye mamuzi,kumbuka kua ha watoto wewe ndio baba yao kama walivyo hao wengine na wana haki
ya kua na wewe kwenye maisha yao kama wenzao, sikwambi kama nirahisi kumueleza mkeo lakini kama unania njia utaipata na mungu atakupa nguvu, kumbuka hujui nani atakufaa kwenye hii dunia kati ya watoto wako...
 
Mke wako naye ni wa huko ''home''? Kama si wa huko basi ujue mizimu haikupenda uowe kwingine. NENDA KATAMBIKE KWANZA!
 
Pole sana mpendwa nimejiweka upande wako na kujikuta nasikitika sana.
Cha msingi andaa mazingira mazuri ya kuongea na mkeo
Mwambie juu ya hili na pia umuombe msamaha kwa katika hali ya kujutia
Najua sisi wanawake huwa tunapanic kwa muda give her time..baada ya muda itamuingia akilini na atakuelewa bila shaka
Ni wewe unamjua mkeo yuko vip lina ana furaha na lini ana huzuni

Na akiwa na furaha anakuwaje ,pia akihuzunika anakuwaje
Lakini cha msingi mweleze kweli
Hata kama hataaccept fact leo au kesho baada ya muda ataelewa janga lipo .
Baada ya hapo utakuwa huru kuwatunza wanao
 
mkuu paulss nimekutumia pm.namna ya kulimaliza hili
 
Last edited by a moderator:
Ila usitume laki kila mwezi...........ni nyingi sana kule home............utajutia mkuu
 
Duh nimeamini JF kuna wataalamu wa kila fani Mkuu wangu paulss ushauri wa The Boss naona kama una mashiko kiasi fulani ebu jaribu kuufanyia kazi mara moja ingawa kuna wanawake wengine vichaa ukifika hiyo hatua ya pili na tatu wanaweza kukumwagia uji wa moto.Pole sana ndugu yangu hali uliyonayo hakuna mwanaume mwanandoa atakayeitamani labda kichaa.

 
Last edited by a moderator:
Sikia kijana anza anza kupiga story na mke wako namna hii.

Jidai una rafiki yako ndo kafanya vile afu some majibu ya mke wako, mke wako akisema kama rafiki yako amwambie tu mke wake, basi geuza kibao pale plae useme kwa kweli sio rafiki yangu...ni mimi ndo nilio fanya hayo.
 
nilijua tu watu wenye mitazamo hasi kama huyu watacoment tu, kabla sijamaliza kuwaza, comment ya kwanza ndo mulemule..........
sasa wewe Zipuwawa ndo umemsaidiaje na iyo comment yako.........?

Unafikiri kumwambia akaombe msamha kwa mkwe wake si ushauri? au ulitaka nisemaje hapo zaidi ya kukemea tabia za kizinzi zifanywazo na wana Ndoa?
 

biblia inasema tusichangie wazinzi;HAPO HAPO INASEMA ANASAMEHE SASA BASI kwa kuwa sijaona sehemu uliyomwomba MUNGU msamaha kwa kitendo cha kutoka nje ya ndoa nashindwa hata kuendelea ;labda ushauri tu kama ulivyoandika yooote naomba uandike unaomwomba mungu akusamehe si kwa kuzaa nje ya ndoa bali kwa kutembea nje ya ndoa yako
nahisi hata mawazo yanayokuja baada ya hapa yatakuwa ya hekima kuliko hayo 75 naushee niliyyaona
mungu akubariki
 
Kwanza kabisa pole sana, na nakushukuru kwa kuleta hili suala mezani, kwa sababu inakuwa ni fundisho kwa jamii yetu kwa ujumla. kwanza kabisa unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutubu makosa ya kuzini kwa mola wako, Pili, kama mama yupo hai, ongea na wazazi wako kuhusu suala hilo walijue, na ili itakapotokea wale watoto unataka kuwachukua basi uwapeleke kwa wazazi wako, lkn wazazi wako wape precaution wasifujishe siri hiyo kwa mkeo. hapo watoto wake wa nje watakuwa na wewe karibu kwa kila kitu. kama wewe ni muislamu na unahisi yule mama watoto wa pembeni anakufaa kuwa mke muoe, lkn kabla ya kufanya hivyo inabidi umuandae mkeo kisaikolojia pamoja na kumpa somo la dini ili hali itakapojitokeza aweze kuikubali, pia mkeo ni mwanadamu, in the longrun kama unataka kunusuru watoto wako mapacha jenga mazingira ambayo hata ukimwambia mkeo atakuelewa. kila la heri mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…