najutia moyo yangu

Najutia moyo wangu, ulofanya uteuzi
Nakiri moyoni mwangu, haukuwa mteuzi
................. Usiulaumu sana moyo, angalau umekupa fundisho!
 
Pole Milcah..

Hukufanya kosa ila huyo baba ndiye wa kulaumu kwa kutothamini jinsi ulivyomuami na kumpa ukweli wako kwake...

Kuna wakati wanaume wanakuwa watu wabaya sana...
 
Pole dada; hiyo ndio dilema kubwa tuipatayo kizazi cha sasa! Ukiuachia moyo, utaumizwa kwani mwenzako ataku-take for granted; ukibania mapenzi, atakuacha kwani ataona humpendi na huenda akadhani una mtu mwingine!
 
Duh! Pole, ni kawaida kama ambavyo wewe uliwatosa wanaume walioonesha hisia za kweli. Usiruhusu mateso ya moyo bidada.
 
pole sana
namshangaa huyo ulompa moyo wako akakudharau na kukupuuza
mbona wengine hatuna hiyo bahati wajamini?
asie na bahati habahatiki
 
pole sana kila tunapotoa hatutegemei kupokea
 
Pole sana, Ulipaswa kusoma alama za nyakati kujua kama nae ana muelekeo wa kukubali kuzipokea hisia zako, kwa kosa hili umepitia darasa na utakuwa umefuza sector hiyo muhimu ya hisia na mahusiano
 
Pole mpenzi wangu milcah.
Ila naomba nikueleze ukweli,hata kama utauma au hutaupenda.
NDIO UMEFANYA KOSA KUMUELEZA MWANAUME HISIA ZAKO,kwa lugha nyingine ni kwamba umemtongoza mwanaume.
Mwanaume ni kama simba,akitaka nyama nzuri inayomvutia ni lazima atoke jasho kuiwinda,muindaji anapopata kitoweo chake kwa shida hukidhamini na kukiona kitamu sana na ndio maana mwanamke unapowindwa hata kama unajua utakubali lazima uringe kidogo,uweke vipozi vya hapa na pale.

Kitoweo kinachopatikana bila kuwindwa huo ni mzoga na simba hali mizoga anamuachia fisi mla mizoga,simba anataka ahangaike na chake chenye uhai akiue mwenyewe na anywe damu fresh.

Wanaume wengi wakitongozwa na mwanamke wanamuona mwanamke huyo ni kimeo,malaya,anajirahisisha na kama ni wale wenye heshima zake anakukataa tena anakuogopa kama ni wale mafisi wasiojali mizoga anakukubali akishakufunua anakuacha na anakusema kwa wenzie.

Sijasema umefanya dhambi au vibaya bali nimesema umefanya kosa.
Wanawake hatutongozi bali tunasubiri tutongozwe.
Siku nyingine ukimpenda mwanaume,usifungue kinywa chako kumtongoza bali kama unaweze mtege yeye ndo aanze kukutongoza halafu ujifanye hata hukuwa na mpango naye ili upate nafasi ya kumringia kidogo,kijasho kkimtoka kidogo ndo unamkubali huku ukimwacha akiamin kuwa umemsumbua kweli kumbe ulimtega.
 
Pole dada.

Lakini hongera kwa kushinda stigma ya mwanamke kumtongoza mwanamme.

Ukiachilia mbali kukataliwa na uliyemtaka, hebu jiulize, wewe umeshakataa wangapi waliokutongoza?

Unadhani mwanamme hana haki ya kukukataa kama hajisikii kukubali?

Na kama akikubali kila anayemtongoza, atakuwa na wangapi?

Haina haja ya kujuta, ni mapito tu. Shida ni kama aligonga mzigo afu akasepa.
 
Pole kosa la kwanza sio kosa bali kurudia kosa. Itakusaidia kuwa makini siku zijazo
 
Nahisi bado nahitaji maelezo ya ziada! Ni kwamba amekukatalia tu au kuna lingine linalokuumiza zaidi?
 
Kuwa na moyo mgumu kwa mwanamke c rahis espcl ukiwa umependa na kama unatumia akil zako bila msaada wa Mungu utateseka,.
Never say Never,utapenda tu,but u keep in'yo mind,wanaume woote wamezaliwa kwa mama mmoja ktabia!so b careful, Kuwa Na Kiasi ktk kila kitu!
Inawezekena ulitanguliza hisia za moyo zaid kwa uyo mtu instead of kutumia akili yako na kumshrksha Mungu!pole dear,bt never ..say..never..na uwe na Kiasi ktk kila kitu!
 
pole sana
namshangaa huyo ulompa moyo wako akakudharau na kukupuuza
mbona wengine hatuna hiyo bahati wajamini?
asie na bahati habahatiki

we unasema tu ndugu, nyie wanaume mkitongozwa na wadada ndo mnawashusha thamani kabisa na kuwaona ni bwelele!!
 
we unasema tu ndugu, nyie wanaume mkitongozwa na wadada ndo mnawashusha thamani kabisa na kuwaona ni bwelele!!

umeona eeh! Bora mtu ufe nalo moyoni kama anashindwa kusoma alama za nyakati.
 
Hivi kuna ubaya kwa msichana kumueleza mwanaume hisia zako.Nujutia nafsi yangu kwa kumuonyesha hisia za kweli mwanaum

pole sana dada.... wala usihofu, tatizo ni kwa sababu ni mara yako ya kwanza bado hujawa mzoefu wa haya maswala ya kutongoza. fomula ni moja kabla hujaanza kumwaga sela jua unaenda kucheza mechi ya mtoano hapo hakuna droo eidha ushinde au ushindwe, mchezaji kabla ya kuanza shindano unatakiwa kuamini kwamba ukishindwa sio udhaifa au makosa bali bahati mbaya!!

Try this please hope will work out with u 2!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…