Pemba ni mahali pazuri sana kutembelea na hata kuishi, watu wake hawana makuu, maisha ni rahisi, kuna mandhari nzuri sana, hali ya hewa ni nzuri, sehemu kubwa ya kisiwa ina rutuba na unaweza kulima chochote. Gharama za vyakula ni nafuu na vyakula vingi ni vya asili.
Bahari na fukwe zake hazijachafuliwa, hakuna msongamano wa watu wala magari. Masuala ya imani ni ya mtu binafsi, ni dhahiri kwamba idadi ya waislamu ni kubwa lakini kila mtu na maisha yake. Kuna wengi wasio waislamu na wanaendesha maisha yao bila usumbufu wowote.
Changamoto ya Pemba ni usafiri wake, usafiri wa uhakika ni ndege lakini bei zake zimechangamka, hivyo wengi hutumia usafiri nafuu wa meli kutokea Dar, Unguja au Tanga.
Nilikuwa huko mwishoni mwa mwaka jana na natamani sana nirudi tena.