BTW; Weka picha ili tulione na pia tuambie bei/siku. Unapatikana wapi pamoja na je ni lazima kumtumia dereva wako ama mkodishaji anakuwa huru kwa uchaguzi?
Hujanielewa. Naposema unauza ni kuiuza huduma hiyo kwa wateja. Hivyo ni vema ukaelezea yafuatayo:
1. Bei ya kukodisha kwa siku
2. Mahali inapopatikana huduma (gari
3. Terms za ukodishaji km dreva, mafuta, muda et al
4. Dhamana nk
5. Ubora wa gari na
6. Mwisho tupia picha mbili tatu hivi kaliiii hata mteja akiona apate shauku ya kuiona gari na kuhitaji huduma.
Usiichukulie vyepesi kihivyo biashara yako kwani tambua kuna washindani wako ambao nao wanawaza wataweza vipi kuwavuta wateja hao hao ambao na wewe unawahitaji. Fursa zipo kibao ila namna gani unaiboresha na kuwashinda washindani wako ndio ishu. Creativity matters Mkuu😁😀