Nakosea kuajiri Mwanaume duka la vipodozi?

Stability

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
306
Reaction score
706
Kuna dogo wa kiume hapa, ni kijana nimemfahamu muda mrefu na ameshanifanyia vitu vingi kwa uaminifu. Ningemuajiri mdada ila sina ninayemfahamu kwa ukaribu.

Nafikiria ni afadhali nimuajiri huyu kijana wa kiume ninayemuamini ili angalau labda nikwepe risk ya wizi kuliko kuajiri mdada ambae simfahamu kiundani.

Nafikiria kumuajiri katika duka la vipodozi, ila naona kama kibiashara itazingua coz wasichana/wakike ndio wateja wengi katika hii business. Sasa kumkuta kijana wa kiume ni kama watakuwa hawaendani kiuteja na labda lugha ya kidada katika urembo.

Mnanishaurijie wakuu, ni hofu yangu tu au ni vizuri niajiri mdada katika duka la vipodozi.
 
mwambie awatongoze lakini asihonge duka πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ awe na kuwasifia kidogo warembo anawajalibisha hereni mteja ananunu kirahisi anaona anajaliwa kesho kutwa akienda kudanga lazima aje tena kununua lotion kwa mkaka..
Utasikia naenda mkaka mcheshi yuleeee nampenda bure

Izo mbinu nakupa maisha haya ni ujanja lakini angalia asifilisi mwanaume kwenye pesa bwana kama mwaminifu freshi kama unakaa nae nyumba 1 ni vzr zaidi
 
hahahah, aisee msemo wako inatakiwa jamaa awe mchemshi na mchangamfu kwa kweli,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahah, aisee msemo wako inatakiwa jamaa awe mchemshi na mchangamfu kwa kweli,

Sent using Jamii Forums mobile app
Eeeeeeeh biashara za wanawake haitaki hasira ni wasumbufu ndio maana wanawake wenyewe hawawezani saana kwenye biashara, wanapenda kumteka muuzaji kwaiyo nayeye muuzaji asitekwe basi unafanyia utani kidogo mtu anunue maisha yaendelee
Hasira kwenu kwenye biashara cheka na kila mtu watakuita mchawi
 
Yah..kwa maelezo yako, wadada wanapenda kuhudumia na wavulana coz wanakuwa wanachukuliana poa wao kwa wao muda mwingine..so akipata mkaka..anakuwa anajitanua haha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake hawataki huduma kutoka kwa wanawake wenzao.
 
sababu wanawake wanakua na jeuri na muda mwingine customer care mbovu ukichagua vitu vingapi tu kuangalia ataona umamsumbua kupanga, Mwanaume kama ni mcheshi anakufanya uwe huru
sure, muda mwingine wanaoneana wivu..anaweza kuja mteja mzuri zaidi yake akawa anamuhudumia kwa jeuri..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…