Hakuna shaka kwamba hali ya Tanzania kwa sasa ni tete,kiuchumi na hata kisiasa.Takwimu tunazopewa za kukua kwa uchumi sisi lolote ni danganya toto.Haingii akilini kwamba uchumi wa nchi ukue halafu maisha ya watu yazidi kuwa duni.Hata 'simple economics' zinakataa.Kwa hiyo sababu za mtu kuwa na mawazo ya kumuengua Rais zipo.Kwa hiyo nisemalo mimi ni kwamba, kwa vile kuna uwezekano wa mtu kuwa na mawazo kama hayo', ni vema serikali ikachukue hatua za makusudi kabisa ya kuchunguza madai ya Mwanahalisi.Hapo pawe mahali pa kuanzia.Sioni mantiki yeyote ya kuwaza kwamba maoni ya Mwanahalisi ni ya uchochezi,kama tupo 'positive.'Tu ione kwamba hiyo ni 'tip' nzuri, mahali pa kuanzia,halafu tuchunguze kwa kina.'Infact' kwa mtazamo wangu mimi ni kwamba' tungewashukuru Mwanahalisi kwa 'tip' hiyo.Watu hawa wa Mwanahalisi wamejijengea hadhi ya kuwa watafiti wazuri,kwa kila hali, kwa hiyo tusiwakatishe tamaa.Sidhani kama wamekurupuka.Watu hawa ni makini sana.