Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nakuita wewe chanda,
Uliye wangu nyonda
Pekee ninakupenda
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita habiba
Uloichomoa miiba
Ukantuliza shurba
Mimi nakuita hivi; au vile!
Nakuita waridi
Ewe ua la ahadi
Pendo lako ni zawadi
Mimi nakuita hivi; au vile!
Nakuita Malkia
Mtawala ulonijia
Na moyo kuniachia!
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita Faraja
Ulochagua umoja
Ya penzi letu la haja!
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita wangu
Wangu peke yangu
Kwa ardhi na kwa mbingu
Mimi nakuita hivi; au vile!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Uliye wangu nyonda
Pekee ninakupenda
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita habiba
Uloichomoa miiba
Ukantuliza shurba
Mimi nakuita hivi; au vile!
Nakuita waridi
Ewe ua la ahadi
Pendo lako ni zawadi
Mimi nakuita hivi; au vile!
Nakuita Malkia
Mtawala ulonijia
Na moyo kuniachia!
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita Faraja
Ulochagua umoja
Ya penzi letu la haja!
Mimi nakuita hivi; au vile!
Ninakuita wangu
Wangu peke yangu
Kwa ardhi na kwa mbingu
Mimi nakuita hivi; au vile!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)