Nakujuza tu kama hujui hivi; Ukipoteza ufunguo wa nyumbani kwako hutakiwi kuvunja komeo/mlango wako bila Ripoti ya Polisi (Loss Report)

Nakujuza tu kama hujui hivi; Ukipoteza ufunguo wa nyumbani kwako hutakiwi kuvunja komeo/mlango wako bila Ripoti ya Polisi (Loss Report)

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Tunakumbushana tu wadau, ni hivi:

Kama ukipotelewa na funguo wa mlango nyumba yako, ofisi yako au ofisi ya umma au sehemu inayofunguliwa kwa ufunguo!

Huruhusiwi kuvunja hilo komeo/kitasa bila kutoa taarifa polisi! (Loss report) ni utaratibu wa kawaida kabisa wadau nawakumbusha!

Pili; Hata kama unamiliki silaha kihalali ukiwa nayo kibindoni/kwenye mkoba Huruhusiwi kumpiga mtu mliyetofautiana katika mazungumzo hata kama mtajibizana hadi akakupiga Kofi inabidi either upambane bila silaha au ukimbie! Lakini huruhusiwi kumpiga risasi wala kumtishia bastola mtu huyo! (NI MARUFUKU)

Pia hurusiwi kumtishia silaha mke, mtoto, Mme au jirani au mtu yoyote mliyetofautiana kwenye migogoro yenu katika mahusiano yenu!

Sehemu pekee unaporuhusiwa kutumia silaha ni kwenye matukio ya uhalifu mfano; Ujambazi, uvamizi/Shambulio la kushtukiza au shambulio dhidi ya mnyama mkali!
 
Kwahio nikifanya kinyume na ulivyo Ni kosa linaloweza kunitia hatiani? Haswa hilo la kupoteza funguo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano ukivunja komeo lako halafu ukamkuta mpenzi wako chumbani coincident kajinyonga au kanywa sumu! Au ukakuta humo ndani vitu vimeibiwa kwa mtu mwingine kufoji funguo kabla ya wewe kuvunja ...mwizi atayegeuziwa kibano ni wewe mwenyewe uliye vunja
 
Huruhusiwi kuvunja hilo komeo/kitasa bila kutoa taarifa polisi! (Lost report) ni utaratibu wa kawaida kabisa wadau nawakumbusha!
Nyumba ni yangu, hasara ni yangu, hao polisi walinichangia nini hata niwashirikishe, tena kwa kuwalipa ada ya loss report, si bora hiyo pesa nimlipe fundi?
 
Sehemu pekee unaporuhusiwa kutumia siraha ni kwenye matukio dhidi ya uharifu mfano; Ujambazi, uvamizi/Shambulio la kushtukiza au shambulio dhidi ya mnyama mkali!
Nimeongeza hilo neno in red kwa nia njema tu
 
Nyumba ni yangu, hasara ni yangu, hao polisi walinichangia nini hata niwashirikishe, tena kwa kuwalipa ada ya loss report, si bora hiyo pesa nimlipe fundi?
Wewe na huyo fundi mtakamatwa ikitokea kuna uchunguzi unahitajika!
Na mafundi walioelimishwa juu ya hili unapompa kazi ya kuvunja mlango anatakiwa ahoji lost report! Vinginevyo atawajibishwa kama mharifu!
 
Tunakumbushana tu wadau ni hivi!!

Kama ukipotelewa na funguo wa mlango nyumba yako, ofisi yako au ofisi ya umma au sehemu inayofunguliwa kwa ufunguo!

Huruhusiwi kuvunja hilo komeo/kitasa bila kutoa taarifa polisi! (Lost report) ni utaratibu wa kawaida kabisa wadau nawakumbusha!

Pili; Hata kama unamiliki silaha kihalali ukiwa nayo kibindoni/kwenye mkoba Huruhusiwi kumpiga mtu mliyetofautiana katika mazungumzo hata kama mtajibizana hadi akakupiga Kofi inabidi either upambane bila silaha au ukimbie! Lakini huruhusiwi kumpiga risasi wala kumtishia bastola mtu huyo! (NI MARUFUKU)

Pia hurusiwi kumtishia silaha mke, mtoto, Mme au jilani au mtu yoyote mliyetofautiana kwenye migogoro yenu katika mahusiano yenu!

Sehemu pekee unaporuhusiwa kutumia silaha ni kwenye matukio ya uharifu mfano; Ujambazi, uvamizi/Shambulio la kushtukiza au shambulio dhidi ya mnyama mkali!
Hata kujenga banda la kuku tu kwenye kiwanja chako/eneo la nyumba yako huruhusiwi (kinyume cha seheria) hadi upate kibali maalum kutoka mamlaka husika
 
Kwa nini sharia zisibandikwe mababarani ili watu wengi wazimanye
Barabarani zinazotakiwa kubandikwa ni alama za matumizi ya barabara pekee (road signs)

Sheria ya msalani utaikuta msalani!
 
Pia ni kinyume cha sheria kumkonyeza mwanamke na kumpigia miluzi hairuhusiwi kabisa na ni kosa kubwa la jinai.
 
Hairuhusiwi kabisa dereva kusimamisha gari watu wavuke ispokuwa sehemu husika kama zebra /pedestrian crossing!
 
Hairuhusiwi kabisa dereva kusimamisha gari watu wavuke ispokuwa sehemu husika kama zebra /pedestrian crossing!
Pia ni marufuku kufungulia mziki mkubwa kwenye gari yako kiasi cha kutokusikia yanayojili inje! Unaweza kupigiwa honi na ambulance au tren na usisikie ukasababisha ajali
 
Back
Top Bottom