Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kuna wakati ulipokuwa NECTA ulilalamikiwa kwamba hutumii weledi huku baadhi ya wadau wakitaka ung'olewe , tulikutetea sana kuliko maelezo , Kwa taarifa yako sisi ndio tulikupendekeza uteuliwe Waziri wa Elimu ili ukaweze kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini Tanzania ikiwemo changamoto ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu , angalia nyuzi zetu humu kabla ya uteuzi wako .
Lakini sasa mimi binafsi naanza kujuta kwa kushiriki kukupigia debe kutokana na matendo yako baada ya kulewa madaraka , madai halali ya wanafunzi umeamua kuyageuza kuwa ni makosa makubwa ya kufukuza watoto wa watu chuoni badala ya kutumia weledi , umeamua kutumia bunduki kuua mbu !
Utavuna unachopanda .