Nakula bila kujisaidia.msaada tafadhali.

Hajiii

Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
8
Reaction score
1
Nina tatizo la kukosa haja kubwa,tatizo lililodumu kwa muda mrefu sasa.huwa nakosa hata zaidi ya wiki moja bila maumiv yeyote ya tumbo.
 
Kula mboga za majani kila siku milo yote miwili pamoja na Matunda nusu ya mlo wako iwe mboga za majani na matunda daily. Asubuhi breakfast yako isikose matunda. Matunda pendelea kutumia yenye fibers kama papai, tango, embe, parachichi. Pia kunywa maji ya kutosha angalau kila siku unywe fluids lita 2. Kama ukifanya hivi bado itaendelea kuwepo basi mwone Dr au nipm
 
Labda utwambie mwanzoni ilkuwaje!
Kuna style ya maisha umebadilisha?
Ulikuwa unakunywa pombe?
Eleza ilikuwaje?

Huduma ya kwanza!
Kula ndizi mbivu, parachichi na papai
mchicha ama juice ya kabichi itasaidia.
Then tupe majibu
 
Pole mkuu kutia vidole vipi nayo imegoma manake ingeshtua maini ya ndani embu jaribu.
 
Nina tatizo la kukosa haja kubwa,tatizo lililodumu kwa muda mrefu sasa.huwa nakosa hata zaidi ya wiki moja bila maumiv yeyote ya tumbo.

Ukilab uwe unakula na matunda kama ndizi, mapapai na mboga mboga lazima uende haja.
 
Enema,huo ndio msaada wako,enema. I have never tried it,but then,I do not have a serious problem.
 
Mkuu usisumbuke sana na kuumiza kichwa juu ya tatizo hilo na kujitia kwenye garama zisizo kuwa na ufumbuzi wowote hebu chek life style yako kama umechange?
Maji ,mboga za majani na matunda yenye nyuzi nyuzi (fibre) ni muhimu sana.

Dawa kiboko ya ugonjwa huo ni hii ya UKWAJU piga juice ya ukwaju original fresh ya kujitengenezea mwenyewe yenye kiwango kidogo cha maji kama utaweza baada ya kuweka sukari changanya na asali mbichi.

Hakika ukinywa ndani ya dk 5 lazima utafute choo kiko wapi.

Angalizo kunywa maji mengi kadri uwezavyo iliukisha kunywa dawa hiyo ushushe mzigo laini lasivyo unaweza chana ndogo
 
Tafuta ducolax 15mg/24hrs on day 1, then 10mg on day 2, once a day! Warning: kuharisha nje nje
 
Ulishawahi kula mke wa mtu??haya ni moja ya maradhi husika kwa inapotokea kumpitia mke wa mtu na bahati mbaya akakujua ...else nenda hospt achana na porojooza huku
 
Nina tatizo la kukosa haja kubwa,tatizo lililodumu kwa muda mrefu sasa.huwa nakosa hata zaidi ya wiki moja bila maumiv yeyote ya tumbo.

Pole sana mkuu, tumia juisi ya ukwaju na tunda la papai kwa sana + mara kwa mara. Tatizo lako litaisha haraka sana
 
ukwaju ushajibu, au? Tuambie kama vipi tukubadilishie dozi. Feedback ni muhimu ili tuweke kwa hansad kwa matumizi ya baadaye.
 
UKOSEFU WA CHOO: Soma tiba rahisi

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa

damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku,

unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja

kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema,

kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa

kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali.

Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa

virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
kwa ushauri wa mzizimkavu nao ukishindikana kwakweli itabidi tukufanyie operation maana kafunga mjadala. ukiremba shauri yako.
kwenye red; HATARIIIIII

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…