Nakula ila Sipati choo msaada jamani

Am For Real

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
323
Reaction score
770
Kama wewe ni wale ambao tunakunya Kwa neema Njoo hapa haraka Sana. Imefikia hatua nakula nikilala usiku nasali kesho nipate choo.

Nakula Sana lakini sijui chakula kinaenda wapi. Tumbo linauma pia na limekuwa likitambi. Kuna muda naamua kunywa uji siku nzima ilimradi kupunguza maumivu.

Nakula kidogo nashiba haraka Sana. Na maumivu ya mgongo Kwa chini ambayo nahisi yametokana na taka vyakula kutotoka.

Nakumbuza enzi zile mfumo wa mmeng'enyo ulikuwa vizuri sikuwahi para shida kama hizi.

##Soso Take my pain###
 
Hospital umekwenda?,wamekwambia nini?
 
Kula embe bivu na maganda yake.
 
Kula mboga mboga za majani kwa wingi na matunda kama mapapai,parachichi,mtindi kwa sana!Bila kusahau maji na mazoezi kwa sana ,utakuja kunishukuru.
 
Ni muhimu sana kumuona daktari mapema...

Kinyumbani nyumbani,
Japo binafsi sipendi, lakini nilijaribu ikafanya kazi 100% kesho yake tena asubuh sana...

nilifundishwa na kuelekezwa hivi tumia kachumbari ya kutosha, yaani nyanya 2, kitunguu ki1, hoho kama ipo, karoti, pilipili kama unatumia ukamulie ndimu au limao.
Kula hiyo kitu ya kutosha kama mboga yako ya usiku,
Asubuhi kesho Lazima utarepoti kwa choo....

Kumbuka chanzo mojawapo cha minyoo ni kachumbari
 
Ukiweka ndimu minyoo hakuna mkuu Wala taifodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…