Nakumatt Pugu Road rekebisheni hizi kasoro

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,416
siku mbili zilizopita nilitembelea nakumatt pugu rd kwa ajili ya manunuzi. nilishikwa na butwaa kuona baadhi ya bidhaa zimeisha muda wake na nyingine zikiwa zimebaki siku mbili tu. mbaya zaidi kuna nyingine zilikuwa zimefutika 'expiry date', sikujua nini sababu ya kufutika huko.

suala jingine ni mitambo inayotumika kutunza bidhaa kama mboga mboga kuwa katika hali mbaya. mboga zimekaa hadi zimebadilika rangi. nikamuuliza kijana aliyekuwa jirani kwa nini zina hali ile, akanijibu (kwa lafudhi ya kikenya), "ni hii machine kuna wakati inazima, ni mbovu. tuliikuta humu baada ya shoprite kuondoka". "unajua hawa jamaa (nakumatt) wame-force kufungua na matengenezo hayajaisha", aliongeza. kwa mujibu wake (sikujua jina lake) ni kwamba bado wanaendelea na matengenezo.

kuna bidhaa hazikubandikwa bei japokuwa kulikuwa na bei sehemu nilipoichagua. nilienda kulipia wanashindwa kupata bei mpaka waingize manually. nyingine nikasubiri hadi wakalete sticker ya bei ambayo ingetakiwa kuwepo wakati nachagua bidhaa.

nilishindwa kuonana na uongozi kwa kuwa hapakueleweka nani ni nani. kama mnaipata hii, jitahidini kuondoa hizo kasoro chache ili biashara iwe njema.

cc TBS TFDA
 
Last edited by a moderator:
Hajui kwamba na sisi siku hizi tumestuka, walisha zoea kuwa watanzania ununua bila kuangalia exp date!! mmeingia choo cha kike. jirekebishen haraka la sivyo duka lita doda!!
 
siku mbili zilizopita nilitembelea nakumatt pugu rd kwa ajili ya manunuzi. nilishikwa na butwaa kuona baadhi ya bidhaa zimeisha muda wake na nyingine zikiwa zimebaki siku mbili tu. mbaya zaidi kuna nyingine zilikuwa zimefutika 'expiry date', sikujua nini sababu ya kufutika huko.

suala jingine ni mitambo inayotumika kutunza bidhaa kama mboga mboga kuwa katika hali mbaya. mboga zimekaa hadi zimebadilika rangi. nikamuuliza kijana aliyekuwa jirani kwa nini zina hali ile, akanijibu (kwa lafudhi ya kikenya), "ni hii machine kuna wakati inazima, ni mbovu. tuliikuta humu baada ya shoprite kuondoka". "unajua hawa jamaa (nakumatt) wame-force kufungua na matengenezo hayajaisha", aliongeza. kwa mujibu wake (sikujua jina lake) ni kwamba bado wanaendelea na matengenezo.

kuna bidhaa hazikubandikwa bei japokuwa kulikuwa na bei sehemu nilipoichagua. nilienda kulipia wanashindwa kupata bei mpaka waingize manually. nyingine nikasubiri hadi wakalete sticker ya bei ambayo ingetakiwa kuwepo wakati nachagua bidhaa.

nilishindwa kuonana na uongozi kwa kuwa hapakueleweka nani ni nani. kama mnaipata hii, jitahidini kuondoa hizo kasoro chache ili biashara iwe njema.

cc TBS TFDA
Hivi mtu uko Afrika tena Dar halafu unaenda kununua mboga supermarket? Ili iweje? Uonekane umeendelea? Ni ulimbukeni tu! Mboga fresh zimejaa mtaani. Mimi ni bidhaa chache sana zitakazonipeleka super market.... hapa bongo
 
Yaani unaenda kununua mbogamboga au matunda supamaket? Huo ni ulimbukeni wa hali ya juu.
 
wa tz nao wameanza kupotezea investment zao kama wao wanavo tupotezea zetu kule kwao. go to hell
 
Hivi mtu uko Afrika tena Dar halafu unaenda kununua mboga supermarket? Ili iweje? Uonekane umeendelea? Ni ulimbukeni tu! Mboga fresh zimejaa mtaani. Mimi ni bidhaa chache sana zitakazonipeleka super market.... hapa bongo

mtu unatoka ofisini saa 1 unafikiri utanunua wapi mboga? wakati masoko mengi saa 11 tu yamefungwa. afu pia usafi, ukienda sokoni wametandaza chini, mara wazishikeshike, wazimwagie maji hata hujui yakoje. sijaona point yako kwa nini mtu yupo dar asiende supermarket kununua mboga.
 
Hili ni tatizo la kuwa na ile dhana kwamba supermarket ipo kwaajili ya kundi fulani au maalumu kwa bidhaa fulani ili hali ukweli halisia maduka yote ya bidhaa za viwango tena hususani vyakula yalipaswa kuwa katika hali nzuri ili kulinda afya ya mlaji. Nazani wengine huogopeshwa sana na hilo neno Super
 
Yaani unaenda kununua mbogamboga au matunda supamaket? Huo ni ulimbukeni wa hali ya juu.

wacha ukosefu wa fikra. verified user afu unapost upopompo! kwan watu wa amerika, ulaya, asia ya mashariki, mashariki ya mbali wote ni malimbukeni? huko mpaka maharagwe yalochemshwa wananunua supermarket. utasema tunaiga umagharibi, sehemu zote hizo nlizokutajia wana HDI kubwa kuliko tanzania. btw supermarket ni sehemu ya kawaida sana, na ndo sehemu yangu rahisi kununua vitu kwa kuwa napata vitu vingi sehemu moja at a reduced retail price. this city is busy, bro!
 
Hivi mtu uko Afrika tena Dar halafu unaenda kununua mboga supermarket? Ili iweje? Uonekane umeendelea? Ni ulimbukeni tu! Mboga fresh zimejaa mtaani. Mimi ni bidhaa chache sana zitakazonipeleka super market.... hapa bongo

Kukurupuka kubaya sana...

Mleta mada hajasema ameenda kununua mboga...Yeye karipoti hali halisi na alichokiona hapo NAKUMAT...
 
Hili ni tatizo la kuwa na ile dhana kwamba supermarket ipo kwaajili ya kundi fulani au maalumu kwa bidhaa fulani ili hali ukweli halisia maduka yote ya bidhaa za viwango tena hususani vyakula yalipaswa kuwa katika hali nzuri ili kulinda afya ya mlaji. Nazani wengine huogopeshwa sana na hilo neno Super

hapo umenena. kwanza bidhaa nyingi kwenye supermarkets zina bei nafuu kuliko maduka ya mtaani. mfano maji ya k'njaro 1.5 lt mtaani yanauzwa 1500, ila nakumatt na wengine wanauza 900 mpaka 1200. watu wakoina kuna taa, ac, basi wanaogopa.
 
Kukurupuka kubaya sana...

Mleta mada hajasema ameenda kununua mboga...Yeye karipoti hali halisi na alichokiona hapo NAKUMAT...

tena inachangiwa na dhana potofu ya kuogopa supermarkets.
 
Barabara ya mbezi beach huku kawe ina sehemu kibao za kuuza mboga mboga tena sio zile za mto msimbazi. Kwanini uende huko supernarket mboga zilizolalla?
Nakumatt sijaona kama iko poa sana bora uchumi mara 100
 
Take note. Supermarkets/malls na maduka yanauza expired products. Kuna siku niliingia Imalaseko pamba house dsm kununua bidhaa. Nikataka kununua packet ya pipi na chocolate. Kuangalia expiry date ya pipi over 2 months ago. Nikanwita supervisor akatetemeka ikabidi manager aje. Tukaendeshana ila akaziondoa packets pale na kuchukua kwa nguvu ile niliyokuwa nayo. Bahati mbaya sikuwa na namba ya TFDA. Si walikimbiza evidence.
 
Yaani unaenda kununua mbogamboga au matunda supamaket? Huo ni ulimbukeni wa hali ya juu.
Duh! Tuna safari ndefu sana... Wengine kama ninyi itabidi tuwabebe mgongoni ili tufike
 
Hivi mtu uko Afrika tena Dar halafu unaenda kununua mboga supermarket? Ili iweje? Uonekane umeendelea? Ni ulimbukeni tu! Mboga fresh zimejaa mtaani. Mimi ni bidhaa chache sana zitakazonipeleka super market.... hapa bongo

Badirika ndugu... Acha ushamba...
 
Barabara ya mbezi beach huku kawe ina sehemu kibao za kuuza mboga mboga tena sio zile za mto msimbazi. Kwanini uende huko supernarket mboga zilizolalla?
Nakumatt sijaona kama iko poa sana bora uchumi mara 100

hahaha.. unafikiri kila mtu anakaa unapokaa?
 
Back
Top Bottom