idoyo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2013
- 3,051
- 1,416
siku mbili zilizopita nilitembelea nakumatt pugu rd kwa ajili ya manunuzi. nilishikwa na butwaa kuona baadhi ya bidhaa zimeisha muda wake na nyingine zikiwa zimebaki siku mbili tu. mbaya zaidi kuna nyingine zilikuwa zimefutika 'expiry date', sikujua nini sababu ya kufutika huko.
suala jingine ni mitambo inayotumika kutunza bidhaa kama mboga mboga kuwa katika hali mbaya. mboga zimekaa hadi zimebadilika rangi. nikamuuliza kijana aliyekuwa jirani kwa nini zina hali ile, akanijibu (kwa lafudhi ya kikenya), "ni hii machine kuna wakati inazima, ni mbovu. tuliikuta humu baada ya shoprite kuondoka". "unajua hawa jamaa (nakumatt) wame-force kufungua na matengenezo hayajaisha", aliongeza. kwa mujibu wake (sikujua jina lake) ni kwamba bado wanaendelea na matengenezo.
kuna bidhaa hazikubandikwa bei japokuwa kulikuwa na bei sehemu nilipoichagua. nilienda kulipia wanashindwa kupata bei mpaka waingize manually. nyingine nikasubiri hadi wakalete sticker ya bei ambayo ingetakiwa kuwepo wakati nachagua bidhaa.
nilishindwa kuonana na uongozi kwa kuwa hapakueleweka nani ni nani. kama mnaipata hii, jitahidini kuondoa hizo kasoro chache ili biashara iwe njema.
cc TBS TFDA

Last edited by a moderator: