Nakumbuka jinsi Marando alivyomuokoa Mnyika

Nakumbuka jinsi Marando alivyomuokoa Mnyika

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Mnyika alishaingia Kingi,

Alishatengenezewa zengwe na Mkuu wa Green Guard, Field Marshal Jemedari. Zengwe lenyewe ni kuwa Mnyika alitumia Meseji Jemedari kuwa atamuua.

Field Marshal akaleta ujumbe wa Simu kwa Spika Anna. Spika Anna akawaka sana kuwa tumefanya siasa zote lakini siasa za kuuana hatujafikia.

Mnyika akawekwa mtu Kati. Uchunguzi ukaanza, maonyo yakatolewa kuwa Mnyika atafungwa. Kwa sababu ni kweli namba iliyotoa vitisho ni ya Mnyika kwenda kwa Field Marshal.

Hali ilikua ngumu sana, wabunge wote wa CCM wakamchna Sana mnyika na CHADEMA yake. Hofu ikatamalaki, Huenda Mnyika atafungwa kwa kutishia kuua. Na pia huenda Chadema ikfutwa. Hali ikawa tete.

Mabere Nyaucho Marando former Spy akaibuka,akaingia kitaa,akafanya ujasusi wake,akagundua kuwa ni kweli Field Marshal katumiwa Meseji ya vitisho vya kuuliwa na Mnyika na ni kweli namba iliyotuma ni ya Mnyika.

Mabere alimhoji Mnyika kwa viapo na Mnyika almhakikishia kabisa kuwa hakumtumia kabisa Meseji ya kumuua Field Marshal.

Mabere alitumia mbinu zake zote za kiintelijensia kutaka kujua ni nini kilichofanyika maana simu ya Mnyika haikuwahi kuibiwa wala kupotea.

Aaah bwana eeh!
Marando aligundua kuwa kumbe Meseji alijitumia mwenyewe kwa kutumia kifaa maalumu kinachoitwa TELEPHONE SPUFFING.

Marando akaitisha Press conference na kueleza yote juu ya kifaa hicho, kilikopatikana, malengo yake na kinavyotumika.

Hali hiyo ni kwamba sio tu ilimuokoa Mnyika hapana, bali pia ilibadilisha kabisa kibao na kuleta hofu upande wa pili.
Upande wa pili Ukawa sasa uko katika hali ya kujitetea.

Asante Mabere Nyaucho Marando.

Uko wapi kaka?
 
Huyu mwamba mara ya mwisho kusikia habari zake alikuwa mgonjwa miaka ya 2017 mpaka Sasa sijui habari zake.
Ha ha has Mwamba alikua mtu mwenye Biti kali Sana.
Uchaguzi Mkuu uliohusisha UKAWA alipigwa Biti kuwa yeye binafsi kama Wakili atatangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu kama mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi atasita kufanya hivyo.

Inasemekana baada ya mkwala huo Mwamba aliugua Sana.
 
Ha ha has Mwamba alikua mtu mwenye Biti kali Sana.
Uchaguzi Mkuu uliohusisha UKAWA alipigwa Biti kuwa yeye binafsi kama Wakili atatangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu kama mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi atasita kufanya hivyo.

Inasemekana baada ya mkwala huo Mwamba aliugua Sana.
Nadhani angali hai ila huenda afya yake ni dhoofu Sana maana huyu mwamba wa TISS amepotea sana au System ilimurudisha kazini.
 
Hiyo ndio ilikuwa chadema halisi, Sio chadema hii mdebwedo, chadema hiyo ukiona Slaa katokeza kwenye kwenye mkutano na wandishi wa habari,jua CCM wanaanza kutafutana,

ilikuwa akimwaga data, mpaka CCM yenyewe inaogopa,kila siku siku katibu wa ccm ilikuwa ni kujibu tuhuma, mpaka akina Mkama na Makamba,

wakapoteza kazi kwa kushindwa kuimili mikiki ya akina Slaa,enzi hizi ukisikia chadema ni chadema Kweli kweli,. Baada ya gia ya angani,ukawa mwisho wa chadema, wakaanza kulamba matapishi yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom