DeMostAdmired
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 1,579
- 3,798
Hello how are you all!!!!!
Leo nimekumbuka hiki kisa.
Ilikuwa mnamo mwaka 2012 nimemaliza darasa la 7. Ilikuwa mwezi wa 10 kama sijasahau, huko mkoa mashughuli kwa ulimaji wa tumbaku.
Baba yangu ni mkulima pia wa tumbaku toka kitambo sana.
Huwa tuna utaratibu wa kuendea wasaidizi wa kazi mkoani kigoma au burundi kabisa.
Sasa hiyo miezi, mwezi wa 9 mpka wa 10 miaka ile ilikuwa ndo miezi ya vitalu (mabedi) ikielekea miezi ya kupanda tumbaku kwenye matuta shambani.
Sasa mimi ndo nilikuwa (nipo) benet sana na Mzee hata familia katika jambo lolote ni lazima wanione mimi japo mimi ndo last born kuna wakubwa zangu lakini katika issue yoyote ni mandatory kuniona.
Sasa katika umri huo mdogo bado Mzee alinipa jukumu la kuwasimamia wasaidizi wetu. Na baadhi ya mambo mengine baba alikuwa anarefer kwangu.
Sasa basi, kila msimu ni lazima ukaguzi ufanyike shambani hasa kwenye nyumba za kulala wasaidizi na ma bani (furnaces) ya kukaushia tumbaku.
Hii ni hatua muhimu sana ukiwa unajiandaa kulikama fegi.
Baba alinituma niende shambani (hapo bado wasaidizi wetu tunaishi nao home).
Ilinibido nikakague kwa umakini sana mazingira ya shambani, nilivoenda nilikuta nyumba zimeharibika sana zinahitaj marekebisho kabla ya kuanza kutumiwa. Na ma bani pia yanahitaji kurekebishwa pia.
Nilirudisha mrejesho kwa Baba na nikashauri zile nyumba hazifai kukaliwa watu mpka zilekebishwe. Baba ni kama hakuwa satisfied na mrejesho ikabidi atafute muda aende kukagua nayeye.
Aliporudi akaniita tulikaa wawili akanambia ni kweli kunahitaji marekebisho lakini hawa wasaidizi wanahitajika kuhamia shambani ili wajiandae na kuanza kuandaa mashamba.
Nikauliza watakaa wapi? Akajibu watakaa kwenye mabani. Hii kitu sikuipenda sio kwamba hayafai kivile No ni kwasababu na mabani pia yalikuwa katika hali hatarishi. Katika emergency wale wasaidizi wangeweza kujihifadhi kwenye mabani kwa siku kadhaa wakisubiri nyumba zao kurekebishwa the wahamie humo.
Sikukubaiana na mawazo ya Baba na nikamwambia palepale kwamba haitakiwi wale wasaidizi wahamie kule shamba kwasas mpka kurekebishwe nilisisitiza (Huwa nipo free kuongea chochote na baba na mama na ndugu yoyote pasi na kuvuka mipaka).
Sasa ni kama hatukufikia common agreement kila mmoja aliondoka na lake. Sasa baadaye Baba aliwaita wale jamaa walikuwa wa3. Akawapa maelekezo kwamba kesho yake walitakiwa wahamie shambani. Nikastuka nikajiuliza hivi mfano wakihamia kule shamba then usiku bani lianguke si watakufa wote huko ndani? Baba alikagua sawa lakini hakuwa na objective decision alikuwa subjective na alidecide pia by experience hakuamini kuwa kuna uwezekano wa bani kuanguka na kuwauwa.
Palepale nikasogea karibu kwa upole tu nikamwambia baba kwamba inambidi wasubiri kidogo kama week na nusu hivi tutafute mafundi wakarekebishe mabani pamoja na nyumba ili wakaishi bila wasiwasi nasis pia tutaishi bila wasiwasi.
Baba alidakia akasema hakuna shida yoyote wao waende tu tutarekebisha nyumba huku wakiwa katika mabani.
Mimi nikasema hakuna shida, baadaye jioni nikawafata nikamwambia inabidi wasubiri kwanza wasiende shambani mpka niwape taarifa kamili. Baba kesho yake alikuwa na safari ambayo alienda na kukaa takriban siku 2.
Baba alijua kuwa asubuhi yake wale jamaa wangehamia shambani lakini nilikuwa nishawazuia. Basi nikawa naanza kutafuta mafundi waende kurekebisha kule shambani.
Baada ya siku mbili baba alivorudi aliwakuta wale jamaa pale home akawaka lakini wakamwambia kuwa wamepewa maelekezo namimi kwamba wasihamie shambani kwanza mpk kurekebishwe.
Baba aliniita akanilaumu sana akanambia shughuli zinakufa shambani an siku zinaenda, mimi nilimuomba msamaha na nikamwambia kuwa nishaanza kutafuta mafundi wakarekebishe.
Kesho yake tulienda shambani asubuhi mimi, Baba na mafundi kwenda kutathimini na waanze kazi.
Ile tunafika shambani tukakuta lile bani baba alilowaelekeza jamaa wakakae limeanguka lote lipo chini.
Baba aliishiwa nguvu akabaki anamshukuru Mungu tu na aliniangalia kwa kama sekunde 30 hivi akanambia nashukuru sana mwanangu umeniokoa na kesi za vifo maana sielewi maiti za hawa watu ningezifanya nini au nigewaeleza nini ndugu zake.
Wale jamaa waliishi home mpka mafundi wakamaliza kazi ndo wakahamia shambani.
Nakumbuka Baba alinizawadia fursa ya kwenda kusoma private school (skul Moja mashughuli sana wilaya moja kati ya wilaya zilizopo mkoani humo)